19 Na kama imani yetu ndani ya Kristo ni kwa ajili ya maisha haya tu, basi sisi tunastahili kuhurumiwa kuliko watu wengine wo wote duniani. 20 Lakini ukweli ni kwamba Kristo amefufuliwa kutoka kwa wafu, matunda ya kwanza ya wote waliolala. 21 Kwa maana kama vile kifo kilivyokuja kwa njia ya mtu mmoja, vivyo hivyo, ufufuo wa wafu umekuja kwa njia ya mtu mmoja.

Read full chapter