1 Wakorintho 1:1-11:13
Neno: Bibilia Takatifu
1 Kutoka kwa Paulo, aliyeitwa kwa mapenzi ya Mungu kuwa mtume wa Yesu Kristo, na Sosthene ndugu yetu.
2 Kwa kanisa la Mungu lililoko Korintho, kwa wote waliota kaswa katika Kristo Yesu, wakaitwa wawe watakatifu, pamoja na wengine wote ambao kila mahali wanalikiri jina la Bwana wetu Yesu Kristo, Bwana wao na Bwana wetu. 3 Nawatakieni neema na amani kutoka kwa Mungu Baba yetu na Bwana Yesu Kristo.
Baraka Zitokazo Kwa Kristo
4 Ninamshukuru Mungu wakati wote kwa ajili yenu, kwa sababu ya neema aliyowapa ndani ya Kristo Yesu. 5 Kwa kuwa katika Kristo mmetajirishwa kwa kila hali, katika kunena kwenu, katika maarifa yote, 6 kama ushuhuda wetu kumhusu Yesu ulivyothibitishwa ndani yenu. 7 Kwa hiyo hamjapungukiwa na karama yo yote ya kiroho wakati mnangoja kudhihirishwa kwa Bwana wetu Yesu Kristo. 8 Yeye atawafanya imara mpaka mwisho, ili msiwe na hatia siku ile ya Bwana wetu Yesu Kristo. 9 Mungu ni mwaminifu ambaye aliwaita muwe na ushirika na Mwanae, Yesu Kristo, Bwana wetu.
Mgawanyiko Ndani Ya Kanisa
10 Nawasihi ndugu zangu, katika jina la Bwana wetu Yesu Kristo, kwamba mpatane ninyi kwa ninyi, na pasiwepo na utengano kati yenu. Muungane pamoja kikamilifu katika kuwaza na katika kuamua. 11 Kwa maana ndugu zangu, nimepata habari kutoka kwa watu wa nyumbani kwa Kloe kwamba kuna ugomvi kati yenu. 12 Maana yangu ni kwamba: mmoja wenu anasema, “Mimi ni wa Paulo,” mwin gine, “Mimi ni wa Apolo,” mwingine, “Mimi ni wa Kefa,” na mwingine, “Mimi ni wa Kristo.”
13 Je, Kristo amegawanyika? Je, ni Paulo aliyewafia msala bani? Au mlibatizwa kwa jina la Paulo? 14 Namshukuru Mungu kwa sababu sikumbatiza mtu ye yote isipokuwa Krispo na Gayo. 15 Kwa hiyo hakuna mtu kati yenu anayeweza kusema kwamba mlibatizwa kwa jina langu. 16 Ndiyo nakumbuka, pia niliwabatiza Stefano na watu wa nyumbani kwake. Lakini zaidi ya hao sikumbuki kama nilimbatiza mtu mwingine. 17 Kwa maana Kristo hakunituma kubatiza bali kuhu biri Injili na nifanye hivyo pasipo kutumia maneno ya hekima ya kibinadamu, ili nguvu ya kifo cha Kristo msalabani iwe dhahiri.
Kristo Ni Hekima Na Nguvu Ya Mungu
18 Kwa maana ujumbe wa msalaba ni upuuzi kwa watu wanaopo tea. Lakini kwetu sisi tunaookolewa ni nguvu ya Mungu. 19 Maan diko yanasema, “Nitaharibu hekima ya watu wenye hekima na kuzi kataa akili za wenye akili.” 20 Yuko wapi mwenye hekima? Yuko wapi mwandishi? Yuko wapi bingwa wa mjadala wa nyakati hizi? Je, Mungu hakufanya hekima ya ulimwengu huu kuwa ni ujinga? 21 Kwa maana katika hekima ya Mungu, wanadamu hawakuweza kumjua Mungu kwa kutumia hekima yao; badala yake, ilimpendeza Mungu kuwaokoa wote waaminio kwa upuuzi wa lile neno linalohubiriwa. 22 Way ahudi wanataka ishara, Wagiriki wanatafuta hekima. 23 Lakini sisi tunamhubiri Kristo aliyesulubiwa msalabani, ujumbe ambao ni kikwazo kwa Wayahudi, na kwa Wagiriki ni upuuzi. 24 Lakini kwa walioitwa, Wayahudi kwa Wagiriki, Kristo ni nguvu ya Mungu na hekima ya Mungu. 25 Kwa maana huu ‘ujinga’ wa Mungu una hekima zaidi kuliko hekima ya wanadamu, na ’udhaifu’ wa Mungu una nguvu ipitayo nguvu ya wanadamu.
26 Ndugu zangu, kumbukeni mlivyokuwa Mungu alipowaita. Si wengi mlikuwa na hekima kwa kipimo cha kibinadamu. Si wengi mli kuwa na vyeo na si wengi mlikuwa wa jamaa za kifahari. 27 Lakini Mungu alichagua vitu ambavyo huhesabiwa kuwa vya kijinga ulimwen guni ili awaaibishe wenye hekima; Mungu alichagua vitu vidhaifu vya ulimwengu huu ili awaaibishe wenye nguvu. 28 Mungu alichagua vitu vya chini na vinavyodharauliwa humu duniani, vitu ambavyo si kitu, ili avibatilishe vile ambavyo vinaonekana kuwa vya maana; 29 ili mtu ye yote asijisifu mbele yake. 30 Mungu ndiye chanzo cha uhai wenu ndani ya Kristo Yesu. Amemfanya yeye kuwa hekima yetu, haki yetu na utakaso na ukombozi 31 Kwa hiyo, kama Maan diko yasemavyo: “Mtu ye yote anayetaka kujisifu, basi ajisifu kwa ajili ya Bwana.”
Ujumbe Wa Msalaba
2 Nilipokuja kwenu ndugu zangu, sikuja kuhubiri siri ya mpango wa Mungu kwa kutumia ufasaha wa kuzungumza au hekima ya binadamu.
2 Kwa kuwa niliamua kwamba wakati nikiwa nanyi nitasahau kila kitu isipokuwa Yesu Kristo; Kristo aliyesulubiwa msalabani. 3 Nilikuja kwenu nikiwa mdhaifu, mwenye woga na nikitetemeka sana. 4 Kuhubiri kwangu na ujumbe wangu haukuwa na hekima na maneno ya kuwashawishi watu, bali ujumbe wangu ulidhihirisha wazi nguvu za Roho, 5 ili imani yenu isiwe imejengwa katika hekima ya wanadamu bali ijengwe katika nguvu ya Mungu.
Hekima Ya Mungu
6 Lakini miongoni mwa watu waliokua kiroho, tunafundisha maneno ya hekima, hii si hekima ya ulimwengu huu au ya watawala wa nyakati hizi ambao watatoweka. 7 Hekima tunayofundisha ni hekima ya siri ya Mungu ambayo imefichwa kwa wanadamu, na ambayo Mungu aliipanga kabla ulimwengu kuwepo, kwa ajili ya utukufu wetu. 8 Watawala wa nyakati zetu hawakuielewa hekima hii. Kwa maana kama wangeliijua, wasingalimsulubisha Bwana wa Utukufu.
9 Lakini, kama Maandiko yasemavyo, “Hakuna aliyeona, hakuna aliyesikia, hakuna aliyewaza, kile ambacho Mungu amekiandaa kwa ajili ya watu wampendao.” 10 Lakini Mungu amekidhihirisha kwetu kwa njia ya Roho wake. Roho huchunguza kila kitu, hata mambo ya ndani ya Mungu. 11 Kwa maana ni nani anajua mawazo ya mtu isipo kuwa roho aliye ndani ya huyo mtu? Vivyo hivyo hakuna mtu anayeelewa mawazo ya Mungu isipokuwa Roho wa Mungu. 12 Sisi hat ukupokea roho ya dunia hii bali Roho aliyetoka kwa Mungu ili tuweze kuelewa yale ambayo Mungu ametupatia bure. 13 Haya ndio tunayozungumzia, lakini si kwa maneno tuliyofundishwa na hekima ya wanadamu bali kwa maneno tuliyofundishwa na Roho, nasi tunafa fanua mambo ya kiroho kwa watu wa kiroho. 14 Mtu ambaye hana Roho wa Mungu hawezi kupokea mambo yanayotoka kwa Roho wa Mungu kwa sababu mambo hayo ni upuuzi kwake; na hawezi kuyaelewa kwa kuwa hayo yanaeleweka tu kwa msaada wa Roho.
15 Mtu wa kiroho anao uwezo wa kupima kila kitu, lakini yeye hapimwi na mtu. 16 “Kwa maana ni nani amefahamu mawazo ya Bwana ili apate kumshauri?” Lakini sisi tunayo nia ya Kristo.
Mgawanyiko Katika Kanisa
3 Lakini ndugu zangu, mimi sikuweza kusema nanyi kama watu wa kiroho, bali kama watu wa mwili, na kama watoto wachanga katika Kristo. 2 Niliwalisha maziwa, sio chakula kigumu; kwa kuwa mli kuwa hamjawa tayari kukipokea. 3 Kwa maana ninyi bado mnatawaliwa na mambo ya mwili. Je, wakati kuna wivu na kugombana kati yenu, ninyi si watu wa mwili wenye tabia kama za watu wa kawaida? 4 Kwa maana mmoja anaposema, “Mimi ni wa Paulo,” na mwingine, “Mimi ni wa Apolo” hamfanyi kama watu wa kawaida?
5 Hata hivyo, Apolo ni nani? Na Paulo ni nani? Sisi ni watum ishi tu ambao kama Bwana alivyotupangia kila mmoja kazi yake, mliamini kwa msaada wetu. 6 Mimi nilipanda mbegu, na Apolo akaimwagilia maji, lakini ni Mungu aliyefanya mbegu iote. 7 Kwa hiyo anayepanda mbegu na anayemwagilia maji si kitu, bali Mungu pekee ndiye aliyefanya mbegu iote. 8 Anayepanda mbegu ni sawa na yule anayemwagilia maji. Kila mmoja wao atapokea malipo yake kulingana na kazi yake. 9 Sisi ni wafanyakazi pamoja na Mungu; ninyi ni shamba la Mungu; ninyi ni jengo la Mungu.
10 Kwa neema niliyopewa na Mungu nilijenga msingi kama mjenzi hodari, na mtu mwingine ana jenga juu ya msingi huo. Lakini kila mmoja awe mwangalifu anavyojenga juu yake. 11 Kwa maana hakuna mtu anayeweza kuweka msingi mwingine isipokuwa ule uliokwisha jengwa, ambao ni Yesu Kristo. 12 Kama mtu ye yote atajenga juu ya msingi huu akitumia dhahabu, fedha, mawe ya tha mani, mbao, majani au nyasi, 13 kazi yake itaonekana; kwa kuwa ile siku itaidhihirisha kazi yake. Itadhihirishwa kwa moto, na moto utapima ubora wa kazi ya kila mtu. 14 Kama alichojenga hakitaharibiwa kwa moto, atapokea tuzo. 15 Kama kazi ya mtu itateketea, atapata hasara, ila yeye mwenyewe ataokolewa, lakini kama mtu aliyenusurika kwenye moto.
16 Je, hamjui kwamba ninyi ni Hekalu la Mungu, na kwamba Roho wa Mungu anakaa ndani yenu? 17 Kama mtu ye yote akiliharibu Hekalu la Mungu, Mungu atamharibu mtu huyo. Kwa sababu Hekalu la Mungu ni takatifu, na ninyi ni Hekalu hilo. 18 Mtu asijidanganye mwenyewe. Kama kuna mtu miongoni mwenu anadhani kuwa yeye ana hekima kwa kipimo cha nyakati hizi, basi afadhali awe mjinga ili apate kuwa na hekima ya kweli. 19 Kwa maana hekima ya ulimwengu huu ni upuuzi mbele za Mungu. Kama Maandiko yasemavyo, “Mungu huwanasa wenye hekima katika hila yao.’ ’ 20 Na tena, “Bwana anajua kwamba mawazo ya wenye hekima ni bure.”
21 Kwa hiyo mtu asijivune kwa sababu ya watu. Kwa kuwa vitu vyote ni vyenu, 22 kama ni Paulo au Apolo au Petro au dunia au maisha au kifo, au wakati uliopo au wakati unaokuja, haya yote ni yenu; 23 na ninyi ni wa Kristo, na Kristo ni wa Mungu.
Mitume Wa Kristo
4 Basi, mtuhesabu sisi kuwa watumishi wa Kristo na mawakili wa siri za Mungu. 2 Zaidi ya hayo, mawakili wanatakiwa wawe waaminifu. 3 Mimi sijali kama ninyi mkinihukumu au nikihukumiwa na mahakama ya wanadamu; kwa kweli hata mimi mwenyewe sijihukumu 4 Dhamiri yangu hainishitaki; lakini hilo halinifanyi nisiwe na hatia. Bwana ndiye anayenihukumu. 5 Kwa hiyo msitoe hukumu kabla ya wakati wake, kabla Bwana hajaja. Yeye atafichua mambo yaliyof ichwa gizani na kwa kuweka wazi nia za mioyo ya watu. Ndipo kila mtu atapokea sifa anayostahili kutoka kwa Mungu.
6 Basi ndugu zangu nimetumia mfano wa Apolo na mimi kwa faida yenu ili muweze kujifunza kutoka kwetu maana ya usemi, “Usivuke mpaka wa yale yaliyoandikwa.” Na hivyo hamtajivunia mtu fulani na kumdharau mwingine. 7 Ni nani aliyewafanya kuwa tofauti na watu wengine wote? Mna kitu gani ambacho hamkupokea? Basi ikiwa mmepokea, mbona mnajivuna kana kwamba hayo mliyonayo si zawadi?
8 Mmekwisha pata kila kitu mnachohitaji! Mmekuwa matajiri! Mmekuwa wafalme pasipo msaada wetu! Lakini laiti kama mngekuwa wafalme kweli ili na sisi tuwe wafalme pamoja nanyi! 9 Kwa sababu inaonekana kwamba Mungu ametuweka sisi mitume katika nafasi ya mwisho kabisa katika msafara wa maonyesho kama watu waliohukumiwa kufa hadharani, kwa sababu tumekuwa maonyesho kwa ulimwengu wote, kwa malaika na kwa wanadamu pia.
10 Kwa ajili ya Kristo sisi ni wajinga, lakini ninyi mna hekima ndani ya Kristo. Sisi ni dhaifu, lakini ninyi mna nguvu. Tunadharauliwa, lakini ninyi mnaheshimiwa. 11 Mpaka wakati huu tuna njaa na kiu, tumevaa matambara, tumeteswa, hatuna makao. 12 Tunafanya kazi ngumu kwa mikono yetu. Tunapolaaniwa, tunabar iki; tunapoteswa tunavumilia. 13 Tunaposingiziwa tunajibu kwa maneno ya upole. Tumekuwa kama takataka ya dunia hii, na uchafu wa ulimwengu mpaka leo hii.
14 Nawaandikia mambo haya, si kwa sababu nataka muone aibu, bali nataka niwaonye kama wanangu wapendwa. 15 Ingawa mnao viongozi wasiohesabika katika Kristo, lakini hamna baba wengi. Mimi nilikuwa baba yenu katika Kristo Yesu kwa kuwaletea Injili. 16 Basi nawasihi mfuate mfano wangu. 17 Kwa sababu hii ninam tuma Timotheo, mwanangu mpendwa na mwaminifu katika Bwana. Yeye atawakumbusha kuhusu maisha yangu katika Kristo ambayo yanakubal iana na mafundisho yangu katika kila kanisa ninalotembelea.
18 Baadhi yenu mmekuwa na kiburi mkidhani kuwa sitafika kwenu. 19 Lakini kama Bwana akipenda, nitafika kwenu mapema, nami nitapenda kujua, zaidi ya maneno yao hawa watu wenye kiburi wana uwezo gani? 20 Kwa kuwa Ufalme wa Mungu si maneno matupu bali ni nguvu. 21 Ninyi amueni. Nije kwenu na fimbo kuwaadhibu, au nije na upendo kwa roho ya upole?
Mwasherati Atengwe
5 Kuna habari thabiti kwamba miongoni mwenu kuna uasherati unaotendeka; tena ni uasherati wa aina ambayo hata watu wasiomjua Mungu hawafanyi. Nimesikia kwamba kuna mtu anazini na mama yake wa kambo! 2 Mnawezaje basi kujivuna! Badala yake mngepaswa kuom boleza. Huyo aliyefanya tendo hili afukuzwe na kutengwa nanyi. 3 Japokuwa sipo nanyi katika mwili, lakini nipo nanyi katika roho. Na nimekwisha toa hukumu kuhusu huyo mtu aliyetenda jambo hili, kama vile ningekuwapo. 4 Mnapokutana katika jina la Bwana wetu Yesu nami nikiwepo katika roho, na nguvu ya Bwana wetu Yesu ikiwepo, 5 mtoeni mtu huyu kwa shetani, ili asili yake ya dhambi iangamizwe lakini roho yake iokolewe siku ile ya Bwana.
6 Kiburi chenu hakifai. Hamjui kwamba hamira kidogo tu huumua donge lote la unga? 7 Ondoeni chachu ya zamani ili mpate kuwa donge lisilo na chachu, kama mnavyotakiwa kuwa. Kwa maana Kristo ambaye ndiye Mwana-kondoo wetu wa Pasaka amekwisha tolewa kama dhabihu. 8 Kwa hiyo, tusherehekee sikukuu hii, sio kwa chachu ya zamani, chachu ya nia mbaya na uovu bali kwa mkate usiotiwa hamira, wa moyo safi na kweli.
9 Niliwaandikia katika barua yangu kuwa msishirikiane na waasherati. 10 Sikuwa na maana kwamba msishirikiane na watu wa dunia walio waasherati, au wenye tamaa mbaya, wanyang’anyi au waabudu sanamu. Kufanya hivyo ingewabidi mtoke duniani. 11 Lakini nilikuwa namaanisha kwamba msishirikiane na mtu ye yote anayejiita ndugu lakini ni mwasherati, mwenye tamaa mbaya, mwabudu sanamu, mtukanaji, mlevi na laghai. Wala msile na mtu kama huyo.
12 Si kazi yangu kuhukumu watu walio nje ya kanisa. Je, si hao walio ndani ya kanisa mnaopaswa kuwahukumu? 13 Mungu anawa hukumu walio nje ya kanisa. “Mfukuzeni mtu mwovu atoke kutoka katika ushirika wenu.”
Kushtakiana Kati Ya Ndugu
6 Kama mmoja wenu ana mashtaka kumhusu ndugu, anathubutuje kupeleka mashtaka yake mbele ya mahakimu wasio mcha Mungu, badala ya kuyapeleka mbele ya watu wa Mungu? 2 Hamjui kwamba watu wa Mungu watahukumu ulimwengu? Na kama ninyi mtahukumu ulimwengu, hamwezi kuhukumu mambo madogo madogo? 3 Hamjui kwamba tutawahu kumu malaika? Je, si zaidi mambo ya maisha haya? 4 Kwa hiyo kwa nini kama kuna kutokuelewana kati yenu kuhusu mambo kama haya, mnachagua kama mahakimu watu ambao hata hawaheshimiwi na kanisa? 5 Nasema hivi ili muone aibu. Je, inawezekana kuwa hakuna mtu kati yenu mwenye hekima ya kutosha kuamua mashtaka kati ya ndugu mmoja na mwenzake? 6 Badala yake ndugu mmoja anampeleka ndugu mwingine mahakamani, tena mbele ya watu wasioamini!
7 Kwamba mnashtakiana kati yenu ni dalili kuwa mmeanguka. Badala ya kushtakiana, kwa nini msikubali kutendewa ubaya? Kwa nini msikubali kudanganywa? 8 Lakini ninyi wenyewe mnakoseana na kudhulumiana, na mnafanya hivyo hata kwa ndugu zenu!
9 Je, hamjui kwamba wasio na haki hawataurithi Ufalme wa Mungu? Msidanganyike, waasherati hawataurithi Ufalme wa Mungu, wala waabudu sanamu, wala wazinzi, wala wapotoshaji; 10 wala wezi, wala wenye tamaa mbaya, wala walevi, wala wanaodhihaki, wala wanyang’anyi. 11 Na baadhi yenu mlikuwa kama hao. Lakini mlioshwa, mlitakaswa, mlihesabiwa haki kwa jina la Bwana Yesu Kristo na katika Roho wa Mungu wetu.
Dhambi Za Zinaa
12 “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini si kila kitu kina faida. “Kila kitu ni halali kwangu,”lakini sitatawaliwa na cho chote. 13 “Chakula ni kwa ajili ya tumbo, na tumbo ni kwa ajili ya chakula,” lakini Mungu ataviharibu vyote viwili. Mwili wa mwanadamu haukuumbwa kwa ajili ya zinaa bali kwa ajili ya Bwana, na Bwana kwa ajili ya mwili.
14 Mungu alimfufua Bwana na atatufufua na sisi pia kwa uwezo wake. 15 Je, hamjui ya kwamba miili yenu ni sehemu ya Kristo? Je, naweza kuchukua sehemu ya mwili wa Kristo na kuiunganisha na mwili wa kahaba? Hata kidogo! 16 Hamjui kwamba mtu aushirikishaye mwili wake na kahaba ana kuwa mmoja naye kimwili? Maandiko yanasema, “Hao wawili watakuwa mwili mmoja.” 17 Lakini mtu anayejiunga na Bwana ana kuwa mmoja naye kiroho.
18 Kimbieni dhambi ya zinaa. Dhambi nyingine zote anazotenda mwanadamu hufanyika nje ya mwili wake, lakini anayezini, ana tenda dhambi juu ya mwili wake mwenyewe. 19 Hamjui kwamba miili yenu ni Hekalu la Roho Mtakatifu anayekaa ndani yenu, ambaye mme pewa na Mungu? Ninyi si mali yenu wenyewe; 20 mmenunuliwa kwa bei kubwa. Kwa hiyo mtukuzeni Mungu katika miili yenu.
Kuhusu Ndoa
7 Na sasa kuhusu mambo mliyoniandikia. Ni vizuri mtu asioe. 2 Lakini kwa kuwa dhambi ya zinaa imeenea, kila mwanamume awe na mke wake mwenyewe, na kila mwanamke awe na mume wake mwenyewe.
3 Mume atimize wajibu wake wa ndoa kwa mkewe; na hali kadhal ika mke kwa mumewe. 4 Kwa maana mke hatawali mwili wake mwe nyewe, bali mume wake ndiye autawalaye. Vivyo hivyo, mume hata wali mwili wake mwenyewe, bali mkewe ndiye anayeutawala. 5 Msiny imane, isipokuwa kama mmekubaliana kufanya hivyo kwa muda mfupi ili muwe na nafasi nzuri ya maombi. Lakini baada ya muda huo rudianeni tena shetani asije akapata nafasi ya kuwajaribu kwa sababu ya kushindwa kujizuia. 6 Nasema haya kama ushauri, na si sheria. 7 Ningalipenda wote wawe kama mimi nilivyo. Lakini kila mtu amepewa karama yake kutoka kwa Mungu, mmoja ana karama hii na mwingine ana karama ile.
8 Na sasa nasema kwa wale wasioolewa na kwa wajane. Ingekuwa vizuri kama wangeendelea kuishi bila kuoa au kuolewa kama mimi. 9 Lakini kama hawawezi kujizuia, basi waoe. Ni afadhali kuoa kuliko kuwaka kwa tamaa.
10 Kwa wale waliooana ninayo amri, si amri yangu ila ni ya Bwana. Mke asimwache mumewe. 11 Lakini kama akimwacha, ni lazima akae bila kuolewa, ama sivyo apatane tena na mumewe. Na mume asimpe mkewe talaka.
12 Lakini kwa wengine nasema, si Bwana ila ni mimi: kama ndugu ana mke asiyeamini, na huyo mke amekubali kuishi pamoja naye, basi asimpe talaka. 13 Na kama mwanamke mwamini ameolewa na mwanaume asiyeamini, na huyo mwanaume amekubali kuishi naye, basi huyo mwanamke asimpe talaka. 14 Kwa maana huyo mwanaume asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mkewe naye mwanamke asiyeamini anatakaswa kwa ajili ya mumewe anayeamini. Kama isingalikuwa hivyo watoto wao wangalikuwa si safi, lakini ilivyo sasa wao ni watakatifu. 15 Lakini kama yule asiyeamini akitaka kuachana na mwenzake anayeamini, basi na iwe hivyo. Katika hali hiyo mke au mume ambaye ni mwamini hafungwi. Kwa sababu Mungu ametuita tuishi kwa amani. 16 Wewe mke, unajuaje kama hutamwokoa mumeo? Wewe mume unajuaje kama hutamwokoa mkeo?
Kuishi Kama Mlivyoitwa
17 Kila mtu aishi maisha aliyopangiwa na Bwana, na ambayo ameitiwa na Mungu. Hii ndio amri ninayotoa kwa makanisa yote.
18 Kama mtu alikuwa ametahiriwa alipoitwa, basi asijaribu kuondoa alama za kutahiriwa kwake. Na kama mtu alikuwa hajatahi riwa alipoitwa, basi, asitafute kutahiriwa. 19 Kwa kuwa kutahi riwa au kutotahiriwa si kitu. Jambo lililo muhimu ni kutii amri za Mungu . 20 Kila mtu abaki katika nafasi ambayo alikuwa nayo alipoitwa kuamini. 21 Je, wewe ulipoitwa ulikuwa mtumwa? Jambo hilo lisikusumbue. Lakini kama unaweza kuwa huru, utumie nafasi hiyo. 22 Kwa maana aliyeitwa kwa Bwana akiwa mtumwa ni mtu huru wa Bwana. Hali kadhalika mtu aliyekuwa huru alipoitwa ni mtumwa wa Kristo. 23 Mmenunuliwa kwa gharama; msikubali kuwa watumwa wa watu. 24 Kwa hiyo ndugu zangu, kila mmoja wenu akae na Mungu katika nafasi aliyokuwa nayo alipoitwa.
Kwa Hali Ya Sasa, Afadhali Kutokuoa
25 Sasa, kuhusu wale walio bikira. Sina amri yo yote kutoka kwa Bwana, lakini mimi natoa ushauri kama mtu aliyemwaminifu kwa rehema ya Bwana.
26 Kwa sababu ya dhiki iliyopo, nadhani itakuwa vyema mki baki kama mlivyo. 27 Je, umeoa? Basi usitake talaka. Kama hujaoa usitafute mke. 28 Lakini kama ukioa, hujatenda dhambi; na kama bikira akiolewa hajatenda dhambi. Lakini wanaooa watakabil iana na matatizo mengi katika maisha haya, nami ningependa myaep uke kwa kubaki mlivyo.
29 Nikisema hivyo ndugu zangu, nina maana kwamba muda uliobaki ni mfupi. Tangu sasa waliooa waishi kama hawakuoa; 30 na wana oomboleza kama hawaoombolezi; wenye furaha kama hawana furaha; wanaonunua kama walivyonunua si mali yao; 31 na wanaoshughulika na vitu vya dunia hii, kama hawahusiki navyo. Kwa maana dunia hii kama tunavyoiona sasa inatoweka.
32 Ningependa msiwe na wasiwasi. Mwanamume ambaye hajaoa anajishughulisha na mambo ya Bwana, jinsi ya kumpendeza. 33 Lakini mwanamume aliyeoa anajishughulisha na mambo ya dunia hii, jinsi ya kumfurahisha mke wake. 34 Kwa sababu hiyo, ana vutwa huku na huko. Mwanamke asiyeolewa au msichana bikira anaj ishughulisha na kazi ya Bwana, jinsi ya kuwa mtakatifu kimwili na kiroho. Lakini mwanamke aliyeolewa anajishughulisha na mambo ya dunia, jinsi ya kumfurahisha mume wake. 35 Ninasema haya kwa faida yenu na sio kuwawekea vikwazo. Napenda muishi sawa na kumpa Bwana maisha yenu yote. 36 Kama mtu anafikiri kwamba mwenendo wake kwa mchumba wake si sawa, na hasa kama mchumba wake anaanza kuzeeka, na anaona anawajibika kumuoa, basi afanye anavyoona vyema; waoane, si dhambi. 37 Lakini kama mwanamume ameshaamua moyoni mwake kuto kuoa bila kulazimishwa na mtu; kama anaweza kujitawala kabisa, basi anafanya vyema kutokumuoa mchumba wake. 38 Kwa hiyo mwana mume anayeamua kumuoa mchumba wake anafanya vizuri, lakini yule anayeamua kutokumuoa anafanya vizuri zaidi.
39 Mwanamke aliyeolewa amefungwa kwa mume wake maadamu anaishi. Kama mumewe akifa, basi mwanamke huyo yuko huru kuolewa na mume mwingine ampendaye, ila iwe katika Bwana. 40 Lakini kwa upande wangu naona kuwa angekuwa na furaha zaidi akibaki alivyo.
Chakula Kilichotolewa Sadaka Kwa Sanamu
8 Sasa kuhusu chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu. Tuna jua kwamba ‘sisi sote tuna ujuzi.’ Lakini ‘ujuzi’ huleta maji vuno, ila upendo hujenga. 2 Mtu anayedhania kwamba anajua kitu, basi hajafahamu kama inavyompasa kujua. 3 Lakini kama mtu anam penda Mungu, mtu huyo anajulikana na Mungu.
4 Kwa hiyo basi, kuhusu kula chakula kilichotolewa sadaka kwa sanamu: tunajua kwamba ‘sanamu haina uhai wa kweli’ na kwamba ‘kuna Mungu mmoja tu.’ 5 Kwa maana hata kama wapo hao wanaoitwa ‘miungu,’ kama ni mbinguni au duniani; na kwa kweli wapo ‘miungu’ wengi na ‘mabwana’ wengi; 6 sisi tunajua kwamba kuna Mungu mmoja, aliye Baba, ambaye vitu vyote vinatoka kwake, na sisi tunaishi kwa ajili yake; na kuna Bwana mmoja, Yesu Kristo, ambaye vitu vyote vimekuwepo kupitia kwake na tunaishi kutokana naye.
7 Lakini si wote wanajua mambo haya. Watu wengine mpaka leo bado wamezoea miungu ya sanamu kiasi ambacho wanapokula chakula hicho wanadhani ni chakula kilichotolewa kwa sanamu, na kwa kuwa dhamiri yao ni dhaifu, inadhurika. 8 Lakini chakula hakitusaidii kuwa karibu zaidi na Mungu. Hatupotezi cho chote tusipokula, wala hatupati faida yo yote kama tukila.
9 Lakini hata hivyo tuwe waangalifu jinsi tunavyotumia uhuru wetu tusije tukawakwaza walio dhaifu katika imani. 10 Kwa maana kama mtu mwenye dhamiri dhaifu akiwaona ninyi wenye ujuzi mkila katika hekalu la sanamu, je, si atavutwa kula chakula kilichoto lewa kwa sanamu? 11 Kwa njia hiyo, huyo ndugu mwenye dhamiri dhaifu, ambaye Kristo alimfia, atateketea kwa sababu ya ujuzi wako. 12 Mnapowatenda dhambi ndugu zenu kwa njia hii na kuharibu dhamiri zao dhaifu, mnamkosea Kristo. 13 Kwa hiyo kama chakula kitamfanya ndugu yangu aanguke katika dhambi, sitakula nyama kamwe, nisije nikamfanya ndugu yangu aanguke.
Haki Za Mtume
9 Je, mimi si huru? Je, mimi si mtume? Je, mimi sikumwona Yesu, Bwana wetu? Je, ninyi si matunda ya kazi yangu katika Bwana? 2 Hata kama mimi si mtume kwa wengine, hakika mimi ni mtume kwenu, kwa maana ninyi ni uthibitisho wa utume wangu katika Bwana. 3 Huu ndio utetezi wangu kwa hao wanaokaa kunihukumu. 4 Je? hatuna haki ya kupewa chakula na cha kunywa? 5 Je, hatuna haki ya kusafiri na mke anayeamini kama wanavyofanya mitume wengine na ndugu zake Bwana na Kefa? 6 Au ni Barnaba na mimi tu ambao tunal azimika kufanya kazi ili tuweze kupata mahitaji yetu?
7 Ni askari yupi anayelipa gharama zake mwenyewe akiwa kam bini? Ni mkulima gani anayepanda mizabibu na hali matunda yake? Ni mfugaji yupi asiyekunywa maziwa ya kundi la wanyama wake? 8 Mnadhani nasema haya kwa kutumia mifano ya kila siku tu? Je, sheria haisemi vivyo hivyo? 9 Kwa maana sheria ya Musa inasema, “Usimfunge ng’ombe kinywa wakati anapopura nafaka.” Je? Mnad hani ni ng’ombe ambaye Mungu anamfikiria? 10 Je, Mungu hasemi haya hasa kwa ajili yetu? Kwa kweli haya yalisemwa kwa ajili yetu kwa sababu mtu anapolima na mwingine akapura nafaka, wote wana paswa kufanya hivyo wakiwa na matumaini ya kupata sehemu ya mavuno. 11 Je, ikiwa sisi tumepanda mbegu ya kiroho kati yenu, itakuwa ni kitu kikubwa sana iwapo tutavuna mahitaji ya mwili kutoka kwenu? 12 Kama wengine wana haki ya kupata msaada kutoka kwenu, sisi je, isingepasa tuwe na haki hiyo hata zaidi? Lakini sisi hatukupenda kutumia haki hii, bali tunavumilia kila kitu ili tusije tukaweka kizuizi kwenye Injili ya Kristo.
13 Hamjui kwamba, watu walioajiriwa kazi Hekaluni wanapata chak ula chao hekaluni, na wale wanaohudumu madhabahuni wanapata sehemu ya sadaka zinazotolewa? 14 Vivyo hivyo, Bwana aliagiza kwamba wale wanaohubiri Injili watapata chakula chao kutokana na Injili. 15 Lakini mimi sikutumia haki hizi, na wala siandiki haya ili kudai haki zangu. Ni afadhali nife, kuliko mtu aniondolee haki hii ya kujisifu. 16 Ninapohubiri Injili, siwezi kujisifu kwa sababu ninalazimika kuhubiri. Ole wangu nisipohubiri Injili! 17 Nikihubiri kwa hiari ningetegemea kupata tuzo; lakini ikiwa nalazimika kufanya hivyo, basi ninachofanya ni kutekeleza wajibu wangu. 18 Kwa hali hii tuzo yangu ni nini? Tuzo yangu ni hii, kwamba katika kuhubiri kwangu, nitangaze Injili pasipo kudai cho chote na hivyo nisitumie haki zangu katika kuhubiri Injili.
19 Ingawa mimi ni huru, na si mtumwa wa mtu ye yote, nimeji fanya kuwa mtumwa wa wote, ili niweze kuwavuta wengi iwezeka navyo. 20 Kwa Wayahudi, nilikuwa kama Myahudi ili niweze kuwa vuta Wayahudi. Kwa watu wanaotawaliwa na sheria, nilikuwa kama niliye chini ya sheria, ingawa mimi siko chini ya sheria, ili niweze kuwavuta walio chini ya sheria. 21 Kwa watu wasioijua sheria nilikuwa kama nisiye na sheria, ingawa hii haina maana kwamba sizishiki amri za Mungu, bali niko chini ya sheria ya Kristo, ili niweze kuwavuta wasio na sheria. 22 Kwa wadhaifu nilikuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mdhaifu ili niweze kuwavuta wadhaifu. Nimekuwa mtu wa hali zote kwa watu wote ili kwa njia zote nipate kuwaokoa baadhi yao. 23 Nafanya haya yote kwa ajili ya Injili, ili nishiriki baraka zake.
24 Mnajua kwamba katika mashindano ya riadha wote wanao shindana hukimbia, lakini ni mmoja wao tu anayepata tuzo. Kwa hiyo kimbieni katika mashindano kwa njia itakayowapatia tuzo. 25 Kila mwana-riadha anayeshiriki katika michezo ya mashindano hufanya mazoezi makali. Wanafanya hivyo ili kupokea tuzo ambayo haidumu, lakini sisi tunafanya hivyo ili kupata tuzo isiyohari bika kamwe. 26 Mimi sikimbii pasipo kuwa na lengo. Sipigani kama mtu anayepiga hewa; 27 lakini nauimarisha mwili wangu na kuutawala, ili baada ya kuwahubiria wengine, mimi mwenyewe nisije nikakataliwa.
Mafundisho Kutoka Historia Ya Wayahudi
10 Nataka mkumbuke ndugu zangu, kwamba baba zetu wote wali kuwa wakiongozwa na wingu, na wote walipita katikati ya bahari ya Shamu. 2 Wote walibatizwa kama wafuasi wa Musa katika lile wingu na ndani ya ile bahari. 3 Wote walikula kile chakula cha kiroho, 4 na wote walikunywa kile kinywaji cha kiroho. Kwa maana waliku nywa kutoka katika ule mwamba wa kiroho uliofuatana nao; na mwamba huo ulikuwa ni Kristo. 5 Hata hivyo Mungu hakupendezwa na wengi wao, kwa hiyo maiti zao zilitapakaa jangwani.
6 Basi mambo haya ni onyo kwetu, tusitamani uovu kama wao walivyofanya. 7 Msiwe waabudu sanamu, kama baadhi yao walivyofa nya. Kama Maandiko yasemavyo, “Watu walikaa chini wakala na kunywa, kisha wakainuka kucheza.” 8 Wala tusifanye uasherati kama baadhi yao walivyofanya, wakafa watu elfu ishirini na tatu kwa siku moja. 9 Pia tusimjaribu Bwana, kama wengine walivyofa nya, wakafa kwa kuumwa na nyoka. 10 Msilalamike, kama wengine walivyofanya, wakaangamizwa na malaika wa kifo.
11 Mambo haya yote yaliwapata wao ili yawe mifano kwa wen gine, nayo yaliandikwa ili yatuonye sisi ambao mwisho wa nyakati umetufikia.
12 Kwa hiyo mtu anayejidhania kwamba anasimama, awe na tahadhari asije akaanguka. 13 Hakuna jaribu lo lote lililowapata ambalo si la kawaida kwa wanadamu. Na Mungu ni mwaminifu; hata- ruhusu mjaribiwe kupita uwezo wenu. Lakini mnapojaribiwa atawapa na njia ya kutokea ili mweze kustahimili.
14 Kwa hiyo rafiki zangu, msishiriki katika ibada za sanamu. 15 Nasema nanyi kama na watu wenye ufahamu. Amueni wenyewe kuhusu haya niyasemayo. 16 Je? Kikombe cha baraka ambacho tuna kibariki, si ushirika katika damu ya Kristo? Na mkate tuumegao, si ushirika wa mwili wa Kristo? 17 Kwa kuwa kuna mkate mmoja, sisi tulio wengi, tu mwili mmoja, kwa kuwa tunashiriki mkate mmoja. 18 Fikirini kuhusu Waisraeli, je, Wanaokula kilichotolewa sadaka hawashiriki katika madhabahu? 19 Je, nikisema hivyo nina taka kusema kwamba sadaka iliyotolewa kwa sanamu au kwamba sanamu ina maana yo yote? 20 La, sivyo. Lakini sadaka inayotolewa kwa sanamu inatolewa kwa mashetani, na sio kwa Mungu. Nami sitaki ninyi muwe na ushirika na mashetani. 21 Hamwezi kunywa katika kikombe cha Bwana na kunywa katika kikombe cha mashetani pia. Hamwezi kushiriki katika meza ya Bwana na katika meza ya mashe tani. 22 Je, tunataka kujaribu kumfanya Bwana awe na wivu? Je, sisi tuna nguvu kuliko yeye?
Uhuru Wa Mwamini
23 Vitu vyote vinaruhusiwa, lakini si vitu vyote vina faida. ‘Vitu vyote ni halali,’ lakini si vyote vinajenga. 24 Mtu asita fute yale yanayomfaa yeye peke yake, bali atafute yale yanayomfaa jirani yake.
25 Kuleni cho chote kinachouzwa katika masoko ya nyama bila kuuliza maswali kuhusu dhamiri. 26 Kwa maana, ‘Dunia na vyote vilivyomo ni mali ya Bwana.’ 27 Kama ukikaribishwa chakula na mtu asiyeamini nawe ukikubali kwenda, kula kitakachokuwa mezani bila kuuliza maswali kwa ajili ya dhamiri. 28 Lakini kama ukiam biwa, “Hiki kimetolewa sadaka kwa sanamu,” basi kwa ajili ya huyo aliyekuambia juu ya hicho chakula, na kwa ajili ya dhamiri, usile. 29 Namaanisha dhamiri ya huyo aliyekuambia, si kwa ajili ya dhamiri yako. Lakini kwa nini uhuru wangu uhukumiwe na dhamiri ya mtu mwingine? 30 Kama nakula kwa shukrani, kwa nini nashutu miwa kwa kile ambacho ninatoa shukrani?
31 Basi, lo lote mfanyalo, kama ni kula au ni kunywa, fanyeni mambo yote kwa ajili ya utukufu wa Mungu. 32 Msiwe kik wazo kwa Wayahudi au kwa Wagiriki, au kwa kanisa la Mungu; 33 kama mimi ninavyojaribu kumridhisha kila mtu katika kila kitu ninachofanya. Kwa maana sitafuti kujiridhisha mwenyewe bali nata futa faida ya walio wengi, ili waweze kuokolewa.
Utaratibu Wa Kuabudu
11 Niigeni mimi, kama mimi ninavyomuiga Kristo. 2 Ninawasifu kwa sababu mnanikumbuka katika kila jambo na kwa kuwa mnashika mafundisho niliyowakabidhi. 3 Lakini napenda muelewe kwamba Kristo ni kichwa cha kila mwanamume, kama vile mume alivyo kichwa cha mkewe, na Mungu ni kichwa cha Kristo. 4 Kwa hiyo mwanamume anayeomba au kutoa unabii akiwa amefunika kichwa chake, anaaib isha kichwa chake. 5 Na mwanamke anayeomba au kutoa unabii pasipo kufunika kichwa chake, anaaibisha kichwa chake, ni sawa kama ame nyoa nywele zote kichwani. 6 Kama mwanamke hataki kufunika kichwa chake, nywele zake zinyolewe; na kama ni aibu kwa mwanamke kunyoa kichwa chake, au kukata nywele zake, basi afunike kichwa chake. 7 Mwanamume asifunike kichwa chake kwa sababu yeye ni mfano na utukufu wa Mungu. Lakini mwanamke ni utukufu wa mwanamume. 8 Kwa maana mwanamume hakuumbwa kutoka kwa mwanamke, bali mwanamke ame toka kwa mwanamume. 9 Wala mwanamume hakuumbwa kwa ajili ya mwa namke, bali mwanamke aliumbwa kwa ajili ya mwanamume. 10 Hii ndio sababu inampasa mwanamke afunike kichwa chake na kwa ajili ya malaika. 11 Lakini katika Bwana mwanamke hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamume, wala mwanamume hawezi kufanya lo lote pasipo mwanamke. 12 Kwa maana kama vile mwanamke alivyoumbwa kutoka kwa mwanamume, vivyo hivyo sasa mwanamume anazaliwa na mwanamke. Lakini vitu vyote vinatoka kwa Mungu.
13 Amueni wenyewe, je, ni sawa kwa mwanamke kumwomba Mungu akiwa hakufunika kichwa chake?
Copyright © 1989 by Biblica