Basi, askofu awe mtu asiye na lawama. Awe mume wa mke mmoja, mwenye kiasi na busara, mtaratibu, mkarimu na aju aye kufundisha. Asiwe mlevi, wala mgomvi bali awe mpole; asiwe mbishi wala mtu apendaye fedha. Aweze kuisimamia nyumba yake vizuri akiwafanya watoto wake kuwa wanyenyekevu na wenye heshima katika hali zote. Kwa maana kama mtu hawezi kuitawala nyumba yake mwenyewe atawezaje kuliangalia kanisa la Mungu? Asiwe mtu aliyeongoka karibuni asije akajiona na kuhukumiwa kama shetani alivyohukumiwa. Kadhalika, awe mwenye sifa njema kati ya watu wa nje ya kanisa, asije akalaumiwa na kuanguka katika mtego wa shetani.

Read full chapter