Maisha Mapya

Basi kwa kuwa Kristo aliteseka katika mwili, ninyi pia jiimarisheni kwa nia hiyo hiyo kwa maana mtu aliyekwisha kuteseka katika mwili hana uhusiano tena na dhambi. Matokeo yake ni kwamba, kwa muda wa maisha yake yaliyobakia hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za mwili bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Maana mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu yaliyopita mkifanya yale ambayo watu wasiomjua Mungu hupenda kutenda: uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulevi na ibada ovu za sanamu. Wanaona ajabu kwamba sasa hamshi riki tena pamoja nao katika ufisadi wao wa kinyama, nao huwatu kana. Lakini itawabidi kujieleza mbele zake yeye aliye tayari kuwahukumu walio hai na waliokufa. Kwa maana hii ndio sababu Injili ilihubiriwa hata kwa hao waliokufa: wahukumiwe kama wana damu wengine kuhusu maisha yao katika mwili, bali wapate kuishi katika roho kama Mungu aishivyo.

Kuja Kwa Kristo Kumekaribia

Mwisho wa mambo yote umekaribia. Kwa hiyo muwe na akili timamu na wenye kiasi ili mweze kuomba. Zaidi ya yote, pen daneni kwa moyo wote, maana upendo hufunika dhambi nyingi sana. Karibishaneni pasipo manung’uniko. 10 Kila mmoja na atumie kipawa alichopewa kuwahudumia wengine, kama mawakili waaminifu wa neema mbalimbali za Mungu. 11 Mtu akisema kitu, basi na awe kama anayesema maneno halisi ya Mungu. Mtu anayetoa huduma na ahudumu kwa nguvu apewayo na Mungu; ili katika mambo yote, Mungu atukuzwe kwa njia ya Yesu Kristo. Yeye ni mwenye utukufu na uweza, milele na milele. Amina.

Kuteseka Kwa Mkristo

12 Wapendwa, msishangae kwa ajili ya mateso makali yanayowa pata kana kwamba ni kitu kigeni kinawatokea. 13 Bali furahini kwamba mnashiriki katika mateso ya Kristo, ili mpate kufurahi na kushangilia wakati utukufu wake utakapofunuliwa. 14 Kama mkilau miwa kwa ajili ya jina la Kristo, mmebarikiwa, kwa sababu Roho wa Utukufu, yaani Roho wa Mungu, anakaa juu yenu. 15 Lakini asiwepo mtu ye yote kati yenu ambaye atateswa kwa kuwa ni mwuaji, au mwizi, au mhalifu au anayejiingiza katika mambo ya watu wengine. 16 Lakini kama mtu akiteseka kwa kuwa ni mkristo asione haya, bali amtukuze Mungu kwa jina hilo. 17 Kwa maana wakati umefika wa hukumu kuanza katika nyumba ya watu wa Mungu; na kama itaanza na sisi, mwisho wa hao ambao hawatii Injili ya Mungu utakuwaje? 18 Na, “Kama ni vigumu kwa mtu wa haki kuokolewa, itakuwaje kwa mtu asiyemcha Mungu na mwenye dhambi?” 19 Basi wale wanaoteswa kufuatana na mapenzi ya Mungu, wajikabidhi kwa Muumba wao aliye mwaminifu.