Matokeo yake ni kwamba, kwa muda wa maisha yake yaliyobakia hapa duniani, haishi tena kwa kufuata tamaa mbaya za mwili bali anaishi kwa kufuata mapenzi ya Mungu. Maana mmekwisha kutumia muda wa kutosha katika maisha yenu yaliyopita mkifanya yale ambayo watu wasiomjua Mungu hupenda kutenda: uasherati, tamaa mbaya, ulevi, karamu za ulevi na ibada ovu za sanamu. Wanaona ajabu kwamba sasa hamshi riki tena pamoja nao katika ufisadi wao wa kinyama, nao huwatu kana.

Read full chapter