Basi, acheni kabisa uovu wote, hila yote, unafiki, wivu na masingizio yote. Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu wenu, kwa maana mmekwisha kuonja fadhili za Bwana.

Jiwe Hai Na Taifa Takatifu

Basi, njooni kwake yeye aliye Jiwe lililo hai, ambalo lili kataliwa na watu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kubwa. Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, ninaweka jiwe kuu la msingi huko Sayuni; jiwe la pembeni teule na la thamani kubwa, na kila amwaminiye hataaibika.” Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani kubwa. Lakini kwao wasioamini, “Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi,” na, “Jiwe ambalo litawafanya watu wajik wae; mwamba ambao utawafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawatii lile neno, kama walivyopangiwa tangu mwanzo.

Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa taka tifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu. 10 Hapo mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Hapo mwanzo mlikuwa hamjapata rehema, lakini sasa mme pata rehema.

11 Rafiki wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho zenu. 12 Muwe na mwenendo mwema kati ya watu wasiomjua Mungu, ili kama watawasema kuwa wakosaji, wayaone matendo yenu mema na wamtukuze Mungu siku ile atakapotujia.

Kuwatii Wenye Mamlaka

13 Jinyenyekezeni kwa ajili ya Bwana chini ya mamlaka yote ya wanadamu: ikiwa ni mfalme ambaye ana mamlaka ya mwisho; 14 au ikiwa ni wakuu wengine ambao amewateua kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema myazime maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru lakini msitumie uhuru wenu kama kisin gizio cha kutenda uovu; bali muishi kama watumishi wa Mungu. 17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu waamini. Mcheni Mungu. Mheshimuni mfalme. 18 Ninyi watumwa, watiini mabwana wenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wapole na wema peke yao, bali hata wale walio wakali. 19 Maana ni jambo jema kwa mtu kuvumilia taabu za maonevu kwa kukumbuka kuwa Mungu yupo. 20 Maana ni sifa gani kwa mtu kustahimili kupigwa kwa kuwa ametenda uovu? Lakini kama mkis tahimili mateso kwa kutenda wema, mnapata kibali mbele za Mungu. 21 Ninyi mmeitwa kwa ajili hiyo, kwa sababu Kristo naye aliteseka kwa ajili yenu akawaachia kielelezo, mzifuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi wala neno la udanganyifu haliku pita kinywani mwake. 23 Walipomtukana, yeye hakuwarudishia matu kano; alipoteswa, hakuwatishia, bali alimtegemea Mungu ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizibeba juu mtini dhambi zetu mwil ini mwake, ili tuwe wafu kwa mambo ya dhambi na tupate kuishi katika haki. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.

25 Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmer udi kwa Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.