1 Petro 1-3
Neno: Bibilia Takatifu
1 Kutoka kwa Petro, mtume wa Yesu Kristo. Kwa wateule wa Mungu ambao wametawanyika, wanaoishi ugenini huko Ponto, Galatia, Kapadokia, Asia na Bithinia. 2 Ninyi mlichaguliwa tangu mwanzo na Mungu Baba na kutakaswa na Roho, mpate kumtii Yesu Kristo na kunyunyiziwa damu yake. Nawatakieni neema na amani tele.
Tumaini Lenye Uzima
3 Asifiwe Mungu, Baba wa Bwana wetu Yesu Kristo! Kwa rehema yake kuu ametufanya tuzaliwe upya ili tupate tumaini lenye uzima kwa kufufuka kwa Bwana wetu Yesu Kristo kutoka kwa wafu; 4 na tupokee urithi usioharibika, usiooza na usiochuja, ambao umewekwa mbinguni kwa ajili yenu. 5 Nanyi, kwa imani, mnalindwa na nguvu ya Mungu mpaka utakapofika wokovu ambao uko tayari kufunuliwa wakati wa mwisho.
6 Furahini sana katika hilo, ingawa sasa kwa kitambo kidogo ni lazima mpate majaribu ya kila aina. 7 Majaribu yataifanya imani yenu, ambayo ina thamani kuliko dhahabu, iwe imepimwa na kuthibitishwa kuwa ya kweli kama vile dhahabu ambayo ingawa ni kitu kiharibikacho, hupimwa kwa moto. Ndipo mtapata sifa, utukufu na heshima siku ile Yesu Kristo atakapofunuliwa. 8 Ingawa hamja pata kumwona, mnampenda. Na ingawa hamumwoni sasa mnamwamini na kujawa na furaha tukufu isiyoelezeka. 9 Maana mnapokea wokovu wa roho zenu, ambao ndio lengo la imani yenu.
10 Manabii waliotabiri kuhusu neema hiyo ambayo ninyi mnge pewa, walitafuta sana na kwa makini habari za wokovu huu. 11 Walijaribu kutafuta kujua ni nani au ni wakati upi uliomaan ishwa na Roho wa Kristo aliyekuwa akisema ndani yao alipotabiri kuhusu mateso ya Kristo na utukufu utakaofuata. 12 Walidhihir ishiwa kuwa kazi waliyokuwa wakifanya si kwa faida yao bali ni kwa ajili yenu. Kwa maana walinena nanyi habari za mambo ambayo sasa mmekwisha elezwa na wale waliowahubiria Injili kwa uwezo wa Roho Mtakatifu aliyetumwa kutoka mbinguni. Hata malaika wanata mani kufahamu mambo haya.
Mwito Wa Kuishi Maisha Matakatifu
13 Kwa hiyo, ziandaeni nia zenu, muwe na kiasi, wekeni tumaini lenu lote katika neema ile mtakayopewa wakati ule Yesu Kristo atakapodhihirishwa. 14 Kama watoto watiifu, msikubali kutawaliwa na tamaa mbaya mlizokuwa nazo wakati mkiishi katika ujinga. 15 Bali kama yeye aliyewaita alivyo mtakatifu, kadhalika ninyi muwe watakatifu katika mwenendo wenu; 16 maana imeandikwa: “Muwe watakatifu kwa sababu mimi ni mtakatifu.”
17 Kwa kuwa mnamwita “Baba” yeye ahukumuye matendo ya kila mtu pasipo upendeleo, ishini maisha yenu hapa duniani kama wageni, kwa kumcha Mungu. 18 Maana mnafahamu kwamba mlikombolewa kutokana na maisha duni yasiyofaa ambayo mlirithi kutoka kwa baba zenu. Hamkukombolewa kwa kutumia vitu viharibikavyo kama fedha na dhahabu, 19 bali mlikombolewa kwa damu ya thamani ya Kristo, Mwana-Kondoo asiye na dosari wala doa. 20 Yeye alichaguliwa kabla ya dunia kuumbwa lakini akadhihirishwa katika siku hizi za mwisho kwa ajili yenu. 21 Kwa ajili yake ninyi mnamwamini Mungu aliyemfufua kutoka kwa wafu akampa utukufu, na kwa hiyo imani yenu na matumaini yenu yako kwa Mungu.
22 Na sasa kwa kuwa mmekwisha kujitakasa kwa kuitii ile kweli na kuwapenda ndugu zenu kwa kweli, pendaneni kwa moyo wote. 23 Maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa mbegu isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele. 24 Maana, “Binadamu wote ni kama nyasi na utukufu wao ni kama ua la mwituni. Nyasi hunyauka na ua huanguka, 25 lakini neno la Mungu hudumu milele.” Na neno hilo ni Habari Njema ambayo mlihubiriwa. 2 1 Basi, acheni kabisa uovu wote, hila yote, unafiki, wivu na masingizio yote. 2 Kama watoto wachanga, mtamani maziwa safi ya kiroho, ili kwa hayo mpate kukua katika wokovu wenu, 3 kwa maana mmekwisha kuonja fadhili za Bwana.
Jiwe Hai Na Taifa Takatifu
4 Basi, njooni kwake yeye aliye Jiwe lililo hai, ambalo lili kataliwa na watu bali kwa Mungu ni teule na la thamani kubwa. 5 Ninyi pia, kama mawe hai mjengwe kuwa nyumba ya kiroho, mpate kuwa makuhani watakatifu, mkitoa sadaka za kiroho zinazokubaliwa na Mungu kwa njia ya Yesu Kristo. 6 Kwa maana imeandikwa katika Maandiko: “Tazama, ninaweka jiwe kuu la msingi huko Sayuni; jiwe la pembeni teule na la thamani kubwa, na kila amwaminiye hataaibika.” 7 Kwenu ninyi mnaoamini, yeye ni wa thamani kubwa. Lakini kwao wasioamini, “Lile jiwe walilokataa waashi limekuwa jiwe kuu la msingi,” 8 na, “Jiwe ambalo litawafanya watu wajik wae; mwamba ambao utawafanya waanguke.” Wanajikwaa kwa sababu hawatii lile neno, kama walivyopangiwa tangu mwanzo.
9 Lakini ninyi ni uzao mteule, ukuhani mtukufu, taifa taka tifu, watu pekee wa Mungu mlioteuliwa kutangaza matendo makuu ya aliyewaita kutoka gizani na kuwaingiza katika nuru yake ya ajabu. 10 Hapo mwanzo ninyi mlikuwa si taifa, lakini sasa ninyi ni watu wa Mungu. Hapo mwanzo mlikuwa hamjapata rehema, lakini sasa mme pata rehema.
11 Rafiki wapendwa, ninawasihi, mkiwa kama wageni na wapi taji njia hapa duniani, epukeni tamaa mbaya za mwili ambazo hupi gana vita na roho zenu. 12 Muwe na mwenendo mwema kati ya watu wasiomjua Mungu, ili kama watawasema kuwa wakosaji, wayaone matendo yenu mema na wamtukuze Mungu siku ile atakapotujia.
Kuwatii Wenye Mamlaka
13 Jinyenyekezeni kwa ajili ya Bwana chini ya mamlaka yote ya wanadamu: ikiwa ni mfalme ambaye ana mamlaka ya mwisho; 14 au ikiwa ni wakuu wengine ambao amewateua kuwaadhibu wahalifu na kuwasifu watendao mema. 15 Kwa maana ni mapenzi ya Mungu kwamba kwa kutenda mema myazime maneno ya kijinga ya watu wapumbavu. 16 Ishini kama watu huru lakini msitumie uhuru wenu kama kisin gizio cha kutenda uovu; bali muishi kama watumishi wa Mungu. 17 Waheshimuni watu wote. Wapendeni ndugu waamini. Mcheni Mungu. Mheshimuni mfalme. 18 Ninyi watumwa, watiini mabwana wenu kwa heshima yote, si wale mabwana walio wapole na wema peke yao, bali hata wale walio wakali. 19 Maana ni jambo jema kwa mtu kuvumilia taabu za maonevu kwa kukumbuka kuwa Mungu yupo. 20 Maana ni sifa gani kwa mtu kustahimili kupigwa kwa kuwa ametenda uovu? Lakini kama mkis tahimili mateso kwa kutenda wema, mnapata kibali mbele za Mungu. 21 Ninyi mmeitwa kwa ajili hiyo, kwa sababu Kristo naye aliteseka kwa ajili yenu akawaachia kielelezo, mzifuate nyayo zake. 22 Yeye hakutenda dhambi wala neno la udanganyifu haliku pita kinywani mwake. 23 Walipomtukana, yeye hakuwarudishia matu kano; alipoteswa, hakuwatishia, bali alimtegemea Mungu ahukumuye kwa haki. 24 Yeye mwenyewe alizibeba juu mtini dhambi zetu mwil ini mwake, ili tuwe wafu kwa mambo ya dhambi na tupate kuishi katika haki. Kwa majeraha yake, ninyi mmeponywa.
25 Kwa maana mlikuwa mmepotea kama kondoo, lakini sasa mmer udi kwa Mchungaji na Mlinzi wa roho zenu.
Mafundisho Kwa Wake Na Waume
3 Kadhalika ninyi wake, jinyenyekezeni chini ya waume zenu, ili kama wako wasioliamini neno, wapate kuamini kwa kuvutiwa na mwenendo wa wake zao. Hawatahitaji kuambiwa neno 2 kwa sababu wataona maisha yenu safi na ya kumcha Mungu.
3 Kujipamba kwenu kusiwe kwa nje, yaani: kwa kusuka nywele, kujipamba kwa dhahabu na kuvaa mavazi maridadi. 4 Bali kujipamba kwenu kuwe katika utu wa ndani wa moyoni, kwa uzuri usioharibika, wa roho ya upole na utulivu. Uzuri wa namna hii ni wa thamani sana mbele za Mungu. 5 Maana ndivyo walivyojipamba wanawake wata katifu wa zamani, waliomtumaini Mungu na kuwa wanyenyekevu kwa waume zao. 6 Kama Sara alivyomtii mumewe Ibrahimu, akamwita ‘bwana’. Ninyi sasa ni binti zake Sara kama mkitenda mema pasipo kuogopa tishio lo lote.
7 Kadhalika ninyi waume, ishini na wake zenu kwa kuwahurumia, mkitambua ya kuwa wao ni dhaifu na hivyo muwape heshima, kwa maana ninyi ni warithi pamoja nao wa neema ya uzima. Fanyeni hivyo ili sala zenu zisizuiliwe.
Msilipe Ovu Kwa Ovu
8 Hatimaye, ninyi nyote muwe na nia moja, mhurumiane, mpen dane kama ndugu, muwe na mioyo ya upole na ya unyenyekevu. 9 Msi lipe ovu kwa ovu, au tusi kwa tusi; ila barikini kwa maana hili ndilo mliloitiwa na Mungu, mpate kurithi baraka. 10 Kwa maana, “Mtu anayependa kufurahia maisha, na anayetamani kuona siku njema, basi auzuie ulimi wake usinene mabaya na midomo yake isi seme uongo. 11 Mtu huyo aepuke maovu, na atende mema; atafute amani na kuifuatilia sana. 12 Kwa maana macho ya Bwana huwaele kea wenye haki, na masikio yake husikiliza sala zao. Bali Bwana huwapa kisogo watenda maovu.”
Kuvumilia Mateso
13 Basi, ni nani atakayewadhuru ikiwa mna juhudi katika kutenda mema? 14 Lakini hata kama mtateseka kwa ajili ya haki, mtabarikiwa. Msiogope vitisho vyao wala msiwe na wasiwasi, 15 bali mioyoni mwenu mtukuzeni Kristo Bwana. Kila wakati muwe tayari kumjibu mtu ye yote atakayewauliza kuhusu tumaini lililomo ndani yenu. Lakini fanyeni hivyo kwa upole na kwa unyenyekevu.
16 Dhamiri zenu ziwe safi ili mnapotukanwa, hao wanaotukana mwenendo wenu mwema katika Kristo, waone haya. 17 Maana ni afad hali kupata mateso kwa kutenda mema kama hayo ndio mapenzi ya Mungu, kuliko kuteseka kwa kutenda maovu. 18 Maana Kristo pia alikufa mara moja tu kwa wakati wote; mwenye haki kwa ajili ya wasio na haki, ili atulete kwa Mungu. Mwili wake uliuawa lakini akafanywa hai katika roho yake. 19 Naye akiwa katika roho alik wenda kuhubiria roho zilizofungwa kifungoni. 20 Roho hizo zamani hazikutii, siku zile Mungu aliposubiri, wakati Noe alipojenga safina, watu wachache, yaani watu wanane, wakaokolewa katika ile gharika ya maji. 21 Maji hayo ni kielelezo cha ubatizo ambao sasa unawaokoa ninyi, si kwa kuondoa uchafu kwenye miili yenu, bali kama dhamana ya kuwa na dhamiri njema kwa Mungu kwa ajili ya kufufuka kwa Yesu Kristo. 22 Yeye amekwenda mbinguni, na amekaa upande wa kulia wa Mungu pamoja na malaika, mamlaka na nguvu zote zikiwa chini yake.

Copyright © 1989 by Biblica