路加福音 16
Chinese Contemporary Bible (Traditional)
善用錢財
16 耶穌又對門徒說:「某財主有個管家,有人控告這管家浪費主人的財物。 2 財主便把管家召來,對他說,『聽說你浪費我的財物,到底是怎麼回事?把帳目交代清楚,你不能再當管家了。』
3 「管家私下盤算,『主人要辭退我了,怎麼辦呢?鋤地我沒有力氣,討飯我又感到羞恥。 4 我知道該怎麼辦了!就算被辭退了,也會有人照應我。』 5 於是,他把欠他主人債的一個一個召來,問第一個,『你欠了我主人多少?』
6 「他回答說,『一百桶油。』
「管家說,『這是你的帳,快坐下,改成五十吧!』
7 「管家又問另一個,『你欠多少?』
「他回答說,『一百石麥子。』
「管家說,『這是你的帳,改成八十石吧。』
8 「主人誇獎這個不義的管家精明。因為今世的兒女在處理世事方面比光明的兒女更精明。
9 「我告訴你們,要善用今世[a]的錢財,廣結朋友。這樣,當錢財不管用時,他們會接你們到永遠的居所。
見微知著
10 「一個人在小事上忠心,在大事上也會忠心;在小事上靠不住,在大事上更靠不住。 11 如果你們不能忠心地處理今世的財富,誰會把真正的財富交託給你們呢? 12 如果你們不能忠心地處理別人的產業,誰會把你們名下的產業交給你們呢? 13 一個僕人不能服侍兩位主人,因為他不是恨這位、愛那位,就是重這位、輕那位。你們不能又事奉上帝,又崇拜金錢。」
警戒貪財的法利賽人
14 法利賽人向來貪財,他們一面聽一面嗤笑耶穌。 15 耶穌對他們說:「你們在人面前自以為義,但上帝能看透你們的心。因為世人所看重的東西在上帝看來卻是可憎的。 16 約翰還沒有來以前,律法書和先知書是你們的準則。他出來後,上帝國的福音開始廣傳,人人都在努力進上帝的國。 17 不過,就是天地都消失,律法的一點一劃也不會失效。 18 任何人休妻另娶,就是犯通姦罪,娶被休的女子也是犯通姦罪。」
財主和乞丐
19 耶穌又說:「有個財主天天衣著華麗,生活奢侈。 20 又有一個名叫拉撒路的乞丐身上長滿了膿瘡,被人放在財主家門口。 21 他渴望吃到財主桌上掉下來的食物殘渣,卻只有狗來舔他的瘡。
22 「後來,乞丐死了,天使帶他到亞伯拉罕身邊。財主也死了,被人埋葬了。 23 他在陰間受折磨,抬頭遠遠地看見亞伯拉罕和他身邊的拉撒路, 24 就喊著說,『我的先祖亞伯拉罕啊!求你可憐我,派拉撒路用指尖蘸點水來潤潤我的舌頭吧!我在這火中實在痛苦不堪。』
25 「亞伯拉罕說,『孩子啊!你要想想,你生前享福,而拉撒路受苦;如今他在這裡得到安慰,而你受折磨。 26 況且,在你我中間隔著一道深淵,這邊的人不能到你那邊去,你那邊的人也不能到這裡來。』
27 「財主說,『我的先祖啊,那麼求你派拉撒路去我父親家裡, 28 因為我有五個弟兄。讓拉撒路去警告他們,以免他們也來到這痛苦的地方。』
29 「但是亞伯拉罕卻說,『他們可以聽從摩西和眾先知的話呀!』
30 「財主回答說,『我的先祖亞伯拉罕啊!他們不會聽的。但如果有一個死而復活的人去警告他們,他們肯定會悔改!』
31 「亞伯拉罕說,『如果他們不聽從摩西和眾先知的話,即使一個人從死裡復活,他們也不會信服。』」
Footnotes
- 16·9 「今世」希臘文是「不義」。
Luka 16
Neno: Bibilia Takatifu
16 Akawaambia wanafunzi wake, “Palikuwa na tajiri mmoja na meneja wake. Ilisemekana kwamba huyo meneja alikuwa anatumia vibaya mali ya tajiri yake. 2 Basi huyo tajiri akamwita meneja wake akamwuliza, ‘Ni mambo gani haya ninayosikia kukuhusu? Nitay arishie hesabu ya mapato na matumizi ya mali yangu kwa maana hutaendelea kuwa meneja tena.’
3 “Yule meneja akawaza moyoni mwake, ‘Nitafanya nini sasa? Bwana wangu anataka kuniondoa katika kazi yangu. Sina nguvu za kulima, na ninaona aibu kuombaomba! 4 Najua nitakalofanya ili nikipoteza kazi yangu hapa, watu wanikaribishe nyumbani kwao.’
5 “Kwa hiyo akawaita wadeni wote wa tajiri wake, mmoja mmoja. Akamwuliza wa kwanza, ‘Deni lako kwa bwana wangu ni kiasi gani?’ 6 Akajibu, ‘Galoni mia nane za mafuta ya alizeti.’ Meneja akamwambia, ‘Chukua hati hii ya deni lako, ibadilishe upesi, uan dike mia nne.’ 7 Kisha akamwuliza wa pili, ‘Na wewe deni lako ni kiasi gani?’ Akajibu, ‘Vipimo elfu moja vya ngano.’ Yule meneja akamwambia, ‘ Chukua hati yako, uandike mia nane.’
8 “Yule tajiri akamsifu yule meneja mjanja kwa jinsi alivy otumia busara. Kwa maana watu wanaojishughulisha na mambo ya dunia hii hutumia busara zaidi kuliko watu wa nuru kukamilisha mambo yao. 9 Nami nawaambieni, tumieni mali ya dunia hii kujipa tia marafiki, ili itakapokwisha mkaribishwe katika makao ya milele.
10 “Mtu ambaye ni mwaminifu katika mambo madogo, atakuwa mwaminifu hata katika mambo makubwa; na mtu ambaye si mwaminifu katika mambo madogo hatakuwa mwaminifu katika mambo makubwa. 11 Na ikiwa hamkuwa waaminifu katika kutunza mali ya dunia hii, ni nani atakayewaamini awakabidhi mali ya kweli? 12 Na kama ham kuwa waaminifu na mali ya mtu mwingine, ni nani atakayewapa mali yenu wenyewe? 13 Hakuna mtumishi awezaye kuwatumikia mabwana wawili. Ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine; au atamheshimu mmoja na kumdharau mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na mali.”
14 Basi Mafarisayo, ambao wenyewe walipenda fedha, waliyasi kia hayo yote wakamcheka. 15 Yesu akawaambia, “Ninyi mnajifa nya kuwa wenye haki mbele za wanadamu, lakini Mungu anaijua mioyo yenu. Kwa maana vile vitu ambavyo wanadamu wanavithamini sana, kwa Mungu havina thamani yo yote.”
Sheria Na Ufalme Wa Mungu
16 “Sheria ya Musa na Maandiko ya manabii yalitumiwa mpaka wakati wa Yohana Mbatizaji. Tangu wakati huo Habari Njema za Ufalme wa Mungu zinahubiriwa na kila mtu anafanya bidii kuingia huko. 17 Lakini ni rahisi zaidi kwa mbingu na nchi kutoweka kuliko hata herufi moja katika sheria kufutwa.
18 Mtu ye yote anayempa mke wake talaka na kumwoa mke mwin gine anazini, na mwanamume amwoaye mwanamke aliyeachwa na mumewe, ewe, anazini.”
Mfano Wa Tajiri Na Maskini Lazaro
19 Akasema, “Palikuwa na tajiri mmoja aliyevaa nguo za rangi ya zambarau na kitani safi, nguo za gharama kubwa, kila siku. 20 Na maskini mmoja, jina lake Lazaro, mwenye vidonda mwili mzima, alikuwa akiletwa mlangoni kwa huyo tajiri kila siku. 21 Lazaro alikuwa akitamani kula makombo yaliyodondoka mezani kwa tajiri. Hata mbwa walikuwa wakiramba vidonda vyake.
22 “Hatimaye, yule maskini alikufa. Malaika wakamchukua akakae pamoja na Ibrahimu mbinguni. Yule tajiri naye pia akafa, akazikwa. 23 Alipokuwa kuzimuni ambapo alikuwa akiteseka, alita zama juu, akamwona Ibrahimu kwa mbali na Lazaro karibu yake. 24 Akaita, ‘Baba Ibrahimu, nionee huruma umtume Lazaro achovye japo ncha ya kidole chake katika maji aupoze ulimi wangu maana ninateseka kwenye moto huu.’ 25 Lakini Ibrahimu akamjibu, ‘Mwa nangu, kumbuka kwamba ulipokuwa hai ulipata kila kitu kizuri uli chotaka, ambapo Lazaro alipokea mabaya. Lakini sasa anafarijika hapa na wewe unateseka. 26 Isitoshe, kati yetu na ninyi huko, kumewekwa bonde kubwa lisilopitika ili wale wanaotaka kutoka huku kuja huko au kutoka huko kuja huku wasiweze.’ 27 Akasema, ‘Basi, baba, tafadhali umtume Lazaro aende nyumbani kwa baba yangu, 28 awaonye ndugu zangu, wasije wao pia wakaletwa mahali hapa pa mateso watakapokufa.’ 29 Ibrahimu akamjibu, ‘Ndugu zako wanazo sheria za Musa na maandiko ya Manabii. Itawapasa watii hayo.’ Lakini yule tajiri akazidi kumsihi, 30 ‘Hapana baba Ibrahimu, ndugu zangu hawatashawishiwa na hayo. Lakini mtu kutoka kuzimu akitumwa kwao watatubu na kuziacha dhambi zao.’
31 “Ibrahimu akamwambia, ‘Wasiposikiliza na kutii sheria za Musa na Maandiko ya manabii, hawatashawishika kutubu hata kama mtu akifufuka kutoka kuzimu.”’
Copyright © 1989 by Biblica