Warumi 12
Neno: Bibilia Takatifu
Ibada Ya Kiroho
12 Kwa hiyo ndugu zangu nawasihi kwa sababu ya huruma zake Mungu, jitoeni kwake muwe sadaka hai, takatifu na inayompendeza Mungu, ambayo ndio ibada yenu ya kiroho. 2 Msiige tabia na mien endo ya dunia hii bali mbadilishwe, nia zenu zikifanywa kuwa mpya, ili mpate kuwa na hakika ni nini mapenzi ya Mungu: yaliyo mema, yanayopendeza machoni pake na makamilifu.
3 Kwa sababu ya neema niliyopewa nawaambia kila mmoja wenu: Msijifikirie kuwa watu wa juu kuliko mlivyo. Badala yake, muwe na kiasi katika mawazo yenu, kila mmoja wenu ajipime kutokana na kiasi cha imani aliyopewa na Mungu. 4 Kama vile ambavyo kila mmoja wenu ana mwili mmoja wenye viungo vingi, na kila kiungo kina kazi yake, 5 hali kadhalika, ndani ya Kristo sisi tulio wengi tunakuwa mwili mmoja na kila mmoja wetu ni sehemu ya we ngine wote. 6 Tumepewa vipawa tofauti kulingana na neema tuliy opokea kutoka kwa Mungu. Kama mtu ana kipawa cha kutoa unabii basi akitumie kulingana na imani yake. 7 Kama kipawa chake ni kuwahudumia wengine, basi awahudumie. Kama ni kufundisha, basi na afundishe. 8 Kama kipawa chake ni kuwatia moyo wengine, na afanye hivyo. Kama ni ukarimu, basi na atoe kwa moyo. Mwenye kipawa cha uongozi na afanye hivyo kwa bidii. Mwenye kipawa cha huruma na aonyeshe huruma yake kwa furaha.
Upendo Wa Kweli
9 Upendo wenu uwe wa kweli. Chukieni uovu, mshikilie yaliyo mema. 10 Pendaneni ninyi kwa ninyi kwa upendo wa kindugu. Waheshimuni wengine kuliko mnavyojiheshimu wenyewe. 11 Juhudi yenu isipungue, moto wenu wa kiroho uendelee kuwaka mkimtumikia Mungu. 12 Muwe na furaha katika tumaini lenu, na katika dhiki muwe na subira. Ombeni wakati wote. 13 Wasaidieni watu wa Mungu walio na shida. Muwe wakarimu kwa matendo.
14 Waombeeni baraka za Mungu wanaowatesa. Wabarikini wala msiwalaani. 15 Furahini pamoja na wenye furaha; huzunikeni pamoja na wenye huzuni. 16 Muishi kwa amani ninyi kwa ninyi. Msitake makuu bali muwe tayari kushirikiana na wanyonge. Kamwe msiwe watu wenye majivuno.
17 Msimlipe mtu uovu kwa uovu. Jitahidini kutenda yaliyo mema machoni pa watu wote. 18 Kama ikiwezekana, kaeni kwa amani na watu wote. 19 Wapendwa, msijilipizie kisasi, bali mtoe nafasi kwa ghadhabu ya Mungu, maana imeandikwa:“Kisasi ni juu yangu; Mimi nitalipa, asema Bwana. 20 Badala yake, adui yakoakiwa na njaa, mpe chakula; akiwa na kiu, mpe kitu anywe. Maana ukifanya hivyo, utampalia mkaa wa moto kichwani pake. 21 Usishindwe na ubaya, bali uushinde ubaya kwa wema.
罗马书 12
Chinese New Version (Simplified)
献上自己当作活祭
12 所以弟兄们,我凭着 神的仁慈劝你们,要把身体献上,作圣洁而蒙 神悦纳的活祭;这是你们理所当然的事奉(“理所当然的事奉”或译:“属灵的敬拜”)。 2 不要模仿这个世代,倒要借着心意的更新而改变过来,使你们可以察验出甚么是 神的旨意,就是察验出甚么是美好的、蒙他悦纳的和完全的事。
信徒行事为人的准则
3 我凭着所赐给我的恩典,对你们各人说,不可自视太高,高于所当看的,反而应该照着 神分给各人信心的大小,看得适中。 4 就像一个身体有许多肢体,各肢体都有不同的功用; 5 照样,我们大家在基督里成为一个身体,也是互相作肢体。 6 照着所赐给我们的恩典,我们各有不同的恩赐:说预言的,就应当照着信心的程度去说; 7 服事人的,就应当照着恩赐去服事;教导的,就应当照着恩赐教导; 8 劝慰的,就应当照着恩赐劝慰;把财物分给人的要真诚;领导的要殷勤;行善的要乐意。
9 爱,不可虚伪;恶,要厌恶;善,要持守。 10 要以手足之爱彼此相亲,用恭敬的心互相礼让。 11 殷勤不可懒惰,心灵要火热,常常服事主; 12 在盼望中要喜乐,在患难中要坚忍,祷告要恒切。 13 圣徒有缺乏的,就要接济;客旅要热诚地款待。 14 迫害你们的,要为他们祝福;只可祝福,不可咒诅。 15 要与喜乐的人一同喜乐,与哀哭的人一同哀哭。 16 要彼此同心,不可心高气傲,倒要俯就卑微的。不可自以为聪明。 17 不可以恶报恶。大家以为美的事,要努力去作。 18 可能的话,总要尽你们的所能与人和睦。 19 亲爱的啊,不要为自己伸冤,宁可等候主的忿怒,因为经上记着,主说:“伸冤在我,我必报应。” 20 相反地,“如果你的仇敌饿了,就给他吃;如果渴了,就给他喝。因为你这样作,就是把炭火堆在他的头上。” 21 不可被恶所胜,反要以善胜恶。
Copyright © 1989 by Biblica
Chinese New Version (CNV). Copyright © 1976, 1992, 1999, 2001, 2005 by Worldwide Bible Society.