Add parallel Print Page Options

16 Mwe na furaha daima. 17 Msiache kuomba. 18 Shukuruni kwa kila jambo. Hivi ndivyo Mungu anavyotutaka tuishi katika Kristo Yesu.

19 Msiizimishe kazi ya Roho Mtakatifu. 20 Msiuchukulie unabii kama kitu kisicho cha muhimu. 21 Lakini pimeni kila kitu. Lishikeni lililo jema, 22 na mkae mbali na kila aina ya ovu.

23 Tunaomba kwamba Mungu mwenyewe, Mungu wa amani, atawafanya muwe watakatifu mkiwa wake. Tunaomba kwamba katika roho yote, nafsi yote, na mwili mzima mtahifadhiwa salama pasipo lawama Bwana wetu Yesu Kristo atakapokuja. 24 Yeye awaitae atawatendea haya. Mnaweza kumtumainia.

25 Kaka na dada zangu, tafadhali mtuombee. 26 Wasalimuni ndugu wote kwa salamu maalum ya watu wa Mungu.[a] 27 Ninawaagiza kwa mamlaka ya Bwana kuusoma walaka huu kwa waamini wote huko. 28 Neema ya Bwana wetu Yesu kristo iwe nanyi nyote.

Read full chapter

Footnotes

  1. 5:26 salamu maalum ya watu wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “busu takatifu”.