20 Lakini uraia wetu uko mbinguni. Nasi tunangoja kwa hamu Mwokozi kutoka huko, yaani Bwana wetu Yesu Kristo, 21 ambaye, kwa uwezo unaomwezesha kutawala kila kitu, atabadilisha miili yetu midhaifu ili iwe na utukufu kama alionao yeye.

Read full chapter