34 Lakini Yesu akawajibu, “Chakula changu ni kufanya mapenzi ya Mungu ambaye amenituma, na kuikamilisha kazi yake. 35 Si mnao msemo kwamba, ‘Bado miezi minne tutavuna’? Hebu yaangalieni mashamba, jinsi mazao yalivyoiva tayari kuvunwa! 36 Mvunaji hupokea ujira wake, naye hukusanya mavuno kwa ajili ya uzima wa milele. Kwa hiyo aliyepanda mbegu na anayevuna, wata furahi pamoja.

Read full chapter