Add parallel Print Page Options

Ni wazaliwa wa mababa zetu wakuu, na ni familia ya kidunia ya Masihi,[a] ambaye ni Mungu aliye juu ya vyote. Yeye asifiwe milele![b] Amina.

Sina maana kuwa Mungu alishindwa kutimiza ahadi yake kwa Wayahudi. Lakini kwa hakika ni baadhi tu ya Waisraeli ndiyo watu wa Mungu[c]. Na hivyo ni baadhi tu ya watoto wa Ibrahimu ndiyo wazaliwa wake halisi. Hivi ndivyo Mungu alimwambia Ibrahimu: “Wazaliwa wako halisi watakuwa wale waliotoka kwa Isaka.”(A)

Read full chapter

Footnotes

  1. 9:5 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Kristo”, tafsiri ya Kiyunani kwa neno “Masihi”. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno.
  2. 9:5 Masihi, ambaye … milele Au “Masihi. Mungu, anayevitawala vitu vyote, asifiwe milele!”
  3. 9:6 watu wa Mungu Kwa maana ya kawaida, “Israeli”, watu aliowachagua Mungu ili kuleta baraka ulimwenguni.