30 Na wale ambao Mungu aliwateua tangu awali pia ali waita; na wale aliowaita pia aliwahesabia haki; na wale aliowahesabia haki aliwapa utukufu wake.

Upendo Wa Mungu

31 Tuseme nini basi kuhusu haya yote? Ikiwa Mungu yuko upande wetu ni nani atakayetupinga? 32 Ikiwa Mungu hakumwacha Mwanae bali alimtoa kwa ajili yetu sote, hatatupatia pamoja na Mwanae, vitu vyote?

Read full chapter