Endapo mwanamke huyo ataishi namwanaume mwingine wakati mumewe yu hai, ataitwa mzinzi. Lakini mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na she ria ya ndoa, na akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

Kazi Ya Sheria

Kadhalika ndugu zangu, ninyi pia mmekufa kuhusu maagizo ya sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili tumzalie Mungu matunda. Tulipokuwa tukitawaliwa na hali yetu ya dhambi, tamaa zetu za dhambi zikiwa zinachochewa na sheria, zilikuwa zikifanya kazi katika miili yetu, tukatumikishwa katika huduma ya dhambi ambayo matunda yake ni kifo.

Read full chapter