Kwa mfano, mwanamke aliyeolewa hufungwa kisheria kwa mumewe wakati wote mumewe akiwa hai. Lakini mumewe akifa mwanamke huyo hafungwi tena na sheria ya ndoa. Endapo mwanamke huyo ataishi namwanaume mwingine wakati mumewe yu hai, ataitwa mzinzi. Lakini mumewe akifa, mwanamke huyo hafungwi tena na she ria ya ndoa, na akiolewa na mtu mwingine haitwi mzinzi.

Kazi Ya Sheria

Kadhalika ndugu zangu, ninyi pia mmekufa kuhusu maagizo ya sheria kwa njia ya mwili wa Kristo. Sasa ninyi ni mali yake yeye aliyefufuliwa kutoka kwa wafu, ili tumzalie Mungu matunda.

Read full chapter