13 Je, hii ina maana kwamba sheria ambayo ni njema ilinile tea kifo? La, sivyo. Lakini ili dhambi itambuliwe kuwa ni dhambi, iliniletea kifo kwa njia ya sheria ambayo ni nzuri; kusudi kwa njia ya sheria, dhambi ionekane kuwa mbaya kabisa.

Mgongano Kati Ya Mwili Na Roho

14 Tunafahamu kwamba sheria ni ya kiroho. Lakini mimi si wa kiroho; mimi nimeuzwa utumwani, ni mtumwa wa dhambi. 15 Sielewi nitendalo: kwa maana lile ninalotaka kulifanya, sifanyi; badala yake, ninafanya lile ambalo nachukia kulifanya.

Read full chapter