Mathayo 5:1-12
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mafundisho ya Yesu Mlimani
(Lk 6:20-23)
5 Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda kwenye kilima na kukaa chini. Wanafunzi wake walimjia Yesu. 2 Kisha Yesu akaanza kuwafundisha watu kwa akasema:
3 “Heri[a] kwa walio maskini na wenye kujua kwamba wanamhitaji Mungu.[b]
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
4 Heri kwa wenye huzuni sasa.
Kwa kuwa watafarijiwa na Mungu.
5 Heri kwa walio wapole.
Kwa kuwa watairithi nchi.[c]
6 Heri kwa wenye kiu na njaa ya kutenda haki.[d]
Kwa kuwa Mungu ataikidhi kiu na njaa yao.
7 Heri kwa wanaowahurumia wengine.
Kwa kuwa watahurumiwa pia.
8 Heri kwa wenye moyo safi,[e]
Kwa kuwa watamwona Mungu.
9 Heri kwa wanaotafuta amani.[f]
Kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.
10 Heri kwa wanaoteswa kwa sababu ya kutenda haki.
Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
11 Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi. 12 Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.
Read full chapterFootnotes
- 5:3 Heri Maana yake ni baraka kuu.
- 5:3 maskini … wanamhitaji Mungu Kwa maana ya kawaida, “maskini wa roho”, ama wenye uhitaji wa kiroho.
- 5:5 watairithi nchi Wataurithi ulimwengu ujao yaani ufalme wa Mungu unaokuja.
- 5:6 wenye kiu na njaa ya kutenda haki Kwa maana ya kawaida, “wenye njaa na kiu ya kutenda haki zaidi ya kitu kingine chochote”.
- 5:8 wenye moyo safi Au wenye mawazo safi ama wenye kukusudia mema moyoni, ama wenye nia njema moyoni.
- 5:9 wanaotafuta amani Au “wapatanishi wa watu waliofarakana”.
Matayo 5:1-12
Neno: Bibilia Takatifu
Yerusalemu, Yudea na kutoka ng’ambo ya mto Yordani.
5 Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, 2 naye akaanza kuwafundisha akisema:
3 “Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. 4 Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. 5 Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. 6 Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. 7 Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. 8 Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. 9 Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.
11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica