Mathayo 11:2-19
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
2 Yohana alipokuwa gerezani, alisikia kuhusu mambo yaliyokuwa yanatokea; mambo ambayo Masihi angefanya. Hivyo akawatuma baadhi ya wafuasi wake kwa Yesu. 3 Wakamuuliza, “Wewe ni yule tuliyekuwa tunamngojea, au tumsubiri mwingine?”
4 Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mliyosikia na kuona: 5 Vipofu wanaona. Viwete wanatembea. Watu wenye magonjwa ya ngozi wanaponywa. Wasiyesikia wanasikia. Wafu wanafufuliwa. Na habari njema inahubiriwa kwa maskini. 6 Heri ni kwa wale wasio na shida kunikubali.”
7 Wafuasi wa Yohana walipoondoka, Yesu alianza kuongea na watu kuhusu Yohana. Alisema, “Ninyi watu mlikwenda jangwani kuona nini? Mtu aliye dhaifu, kama unyasi unaoyumbishwa na upepo? 8 Hakika, ni nini mlichotarajia kuona? Aliyevaa mavazi mazuri? Hakika si hivyo. Watu wote wanaovaa mavazi mazuri wanapatikana katika ikulu za wafalme. 9 Hivyo mlitoka kuona nini? Nabii? Ndiyo, Yohana ni nabii. Lakini ninawaambia, Yeye ni zaidi ya hilo. 10 Andiko hili liliandikwa kuhusu Yohana:
‘Sikiliza! Nitamtuma mjumbe mbele yako.
Yeye ataandaa njia kwa ajili yako.’(A)
11 Ukweli ni kuwa Yohana Mbatizaji ni mkuu kuliko yeyote aliyewahi kuja katika ulimwengu huu. Lakini hata mtu asiye wa muhimu katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu wakati wa Yohana Mbatizaji ulipokuja mpaka sasa, Ufalme wa Mungu umekabiliwa na mashambulizi. Watu wenye nguvu wamejaribu kuudhibiti ufalme huu.[a] 13 Kabla ya Yohana kuja, Sheria ya Musa na manabii wote wamesema kuhusu mambo ambayo yangetokea. 14 Na ikiwa mnaamini waliyosema, basi Yohana ni Eliya. Ndiye waliyesema angekuja. 15 Ninyi watu mnaonisikia, sikilizeni!
16 Ninaweza kusema nini kuhusu watu wanaoishi leo? Watu siku ya leo ni kama watoto wanaokaa katika masoko. Kundi moja la watoto linaliambia kundi lingine,
17 ‘Tuliwapigia filimbi,
lakini hamkucheza;
tuliimba wimbo wa maziko,
lakini hamkuhuzunika.’
18 Kwa nini ninasema watu wako hivyo? Kwa sababu Yohana alikuja na hakula vyakula vya kawaida na kunywa divai, na watu walisema, ‘Ana pepo ndani yake.’ 19 Mwana wa Adamu amekuja akila na kunywa, na watu husema, ‘Mwangalie! Hula sana na kunywa divai nyingi. Ni rafiki wa wakusanya kodi na wenye dhambi wengine.’ Lakini hekima inaonesha kuwa sahihi kutokana na yale inayotenda.”
Read full chapterFootnotes
- 11:12 Herode Antipa alimkamata na kisha kumwua Yohana Mbatizaji na pia alijaribu kumzuia Yesu na wanafunzi wake kwa nguvu. Tazama Herode katika Orodha ya Maneno.
Matayo 11:2-19
Neno: Bibilia Takatifu
2 Basi Yohana Mbatizaji aliposikia akiwa gere zani mambo ambayo Yesu alikuwa akifanya, aliwatuma wanafunzi wake 3 wakamwulize, “Wewe ni yule anayekuja, au tumngojee mwin gine?” 4 Yesu akawajibu, “Nendeni mkamweleze Yohana yale mnayo sikia na kuona: 5 vipofu wanapata kuona, viwete wanatembea, wenye ukoma wanatakaswa, viziwi wanasikia, wafu wanafufuliwa na maskini wanahubiriwa Habari Njema. 6 Amebarikiwa mtu ambaye hapotezi imani yake kwangu.”
7 Wale wanafunzi wa Yohana walipoondoka, Yesu akaanza kuwaam bia ule umati wa watu kuhusu Yohana Mbatizaji. Akawauliza, “Mli pokwenda kule nyikani, mlikwenda kuona nini? Unyasi ukitikiswa na upepo? 8 Kama sivyo, mlikwenda huko kuona nini basi? Mtu aliyevaa mavazi maridadi? Lakini wanaovaa nguo maridadi wanakaa katika majumba ya wafalme. 9 Basi kwa nini mlikwenda huko? Kumwona nabii? Naam, nawaambieni yeye ni zaidi ya nabii. 10 Huyo ndiye ambaye anaelezwa katika Maandiko kwamba: ‘ Angalia namtuma mjumbe mbele yako, ambaye atakuandalia njia.’ 11 Nawaambieni kweli kwamba kati ya watu wote waliozaliwa na wanawake, hajatokea mtu aliye mkuu zaidi ya Yohana Mbatizaji. Lakini hata hivyo aliye mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni, ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu siku za Yohana Mbatizaji hadi sasa, Ufalme wa Mungu umekuwa ukishambuliwa vikali; na watu wenye jeuri wanajaribu kuuteka kwa nguvu. 13 Kwa maana manabii wote na sheria walita biri mpaka wakati wa Yohana. 14 Na kama mko tayari kusadiki uta biri wao, basi Yohana ndiye Eliya ambaye kuja kwake kulitabiriwa. 15 Mwenye nia ya kusikia na asikie.
16 “Kizazi hiki nikilinganishe na nini?” Kinafanana na waliokaa masokoni wakiwaita wenzao na kuwaambia, 17 ‘Tuliwapigia filimbi, lakini hamkucheza; tuliwaimbia nyimbo za msiba, lakini hamkuomboleza.’ 18 Kwa maana Yohana Mbatizaji alikuja na akawa hali wala hanywi nao wanasema, ‘Amepagawa na pepo’. 19 Mimi mwana wa Adamu nimekuja nikila na kunywa, nao wanasema, ‘Mta zameni mlafi na mlevi; rafiki wa watoza kodi na wenye dhambi!’ Lakini hekima huthibitishwa kwa matendo yake.”
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica