Font Size
Matendo Ya Mitume 24:22-24
Neno: Bibilia Takatifu
Matendo Ya Mitume 24:22-24
Neno: Bibilia Takatifu
22 Ndipo Feliksi ambaye alikuwa anafahamu vizuri habari za Njia, akaamua kuahirishwa kwa kesi, akasema, “Mara jemadari Lisia atakapofika nitatoa hukumu yangu juu ya kesi hii.” 23 Akaamuru askari amweke Paulo kizuizini chini ya ulinzi lakini awe na uhuru kiasi, na marafiki zake wasizuiwe kumhudumia. 24 Baada ya siku chache Feliksi akaja na mkewe Drusila ambaye alikuwa Myahudi. Akatuma Paulo aitwe, wakamsikiliza akizungumza juu ya kumwamini Kristo Yesu.
Read full chapter
Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Copyright © 1989 by Biblica