Yesu Abadilika Sura Mlimani

17 Baada ya siku sita, Yesu akawachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo, wakaenda peke yao juu ya mlima mrefu. Na wakiwa huko, Yesu akabadilika sura mbele yao, uso wake ukang’aa kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama mwanga. Na mara Musa na Eliya wakawatokea, wakawa wakizungumza na Yesu. Kisha Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri kwamba sisi tuko hapa. Ukiniruhusu, nitatengeneza vibanda vitatu hapa: kimoja chako, kingine cha Musa na kingine cha Eliya.”

Petro alipokuwa bado akizungumza, ghafla, wingu linalong’aa likatanda juu yao na sauti ikatoka kwenye wingu hilo ikasema, “Huyu ni mwanangu mpendwa, ambaye nimependezwa naye; msikilizeni yeye.” Wanafunzi waliposikia haya walianguka chini kifudifudi wakajawa na hofu. Lakini Yesu akaja, akawagusa, akawaambia, “Inukeni. Msiogope.” Walipoinua macho yao hawakumwona mtu mwingine isipokuwa Yesu peke yake.

Walipokuwa wakishuka mlimani, Yesu akawaambia, “Msimwambie mtu ye yote maono haya mpaka mimi Mwana wa Adamu nitakapofufuliwa kutoka kwa wafu.” 10 Wale wanafunzi wakamwuliza, “Kwa nini basi walimu wa sheria wanasema kwamba lazima Eliya aje kwanza?”

11 Akawajibu, “Ni kweli, Eliya lazima aje kwanza kurekeb isha mambo yote. 12 Lakini nawaambia, Eliya amekwisha kuja, lakini hawakumtambua, bali walimtendea walivyotaka. Na mimi Mwana wa Adamu pia watanitesa.” 13 Ndipo wale wanafunzi wakaelewa kuwa alikuwa anazungumza kuhusu Yohana Mbatizaji.

Yesu Amponya Kijana Mwenye Kifafa

14 Alipofikia ulipokuwa umati wa watu, mtu mmoja alimjia Yesu akapiga magoti mbele yake akasema, 15 “Bwana, mwonee huruma mwanangu. Yeye ana kifafa na anateseka sana. Mara nyingi huan guka motoni na kwenye maji. 16 Nimemleta kwa wanafunzi wako laki ni hawakuweza kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi kizazi kipotovu msioamini, nitakaa nanyi mpaka lini na nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa kwangu.” 18 Yesu akamkemea yule pepo mchafu, akamtoka yule kijana, naye akapona tangu wakati huo. 19 Kisha wanafunzi wakam wendea Yesu kwa siri wakamwuliza, “Kwa nini sisi hatukuweza kum toa? ” 20 Akawajibu, “Kwa sababu ya imani yenu ndogo. Nina waambieni kweli, mkiwa na imani kama punje ndogo ya haradali, mtauambia mlima huu, ‘Ondoka hapa uende pale’ nao utaondoka; na hakuna ambalo halitawezekana kwenu.” [ 21 “Lakini pepo wa aina hii hatoki ila kwa kuomba na kufunga.”]

22 Siku moja walipokuwa pamoja Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Adamu atawekwa mikononi mwa watu. 23 Nao watamwua na siku ya tatu atafufuka.” Wakasikitika sana.

Yesu Na Petro Watoa Kodi Ya Hekalu

24 Yesu na wanafunzi wake walipofika Kapernaumu, wakusanyaji kodi ya Hekalu walimjia Petro wakamwuliza, “Je, mwalimu wako hulipa kodi ya Hekalu?” 25 Petro akajibu, “Ndio, analipa.” Petro aliporudi nyumbani, Yesu akawa wa kwanza kusema, akamwuli za, “Unaonaje Simoni’ wafalme wa ulimwengu hupokea ushuru na kodi kutoka kwa nani? Unadhani kutoka kwa jamaa zao au kutoka kwa wageni?” 26 Petro akamjibu, “Kutoka kwa wageni.” Yesu akam wambia, “Kwa hiyo jamaa zao wamesamehewa. 27 Lakini ili tusi waudhi, nenda baharini ukatupe ndoana. Mchukue samaki wa kwanza utakayemkamata; mfungue kinywa chake nawe utakuta fedha zinazo tosha kulipia kodi yangu na yako; ichukue ukawalipe.”

Yesu Aonekana Akiwa na Musa na Eliya

(Mk 9:2-13; Lk 9:28-36)

17 Siku sita baadaye, Yesu aliwachukua Petro, Yakobo na Yohana ndugu yake Yakobo na akapanda nao kwenye mlima mrefu. Walikuwa peke yao huko. Wafuasi wake hawa walipokuwa wakimwangalia, Yesu alibadilika. Uso wake ukawa angavu kama jua na nguo zake zikawa nyeupe kama mwanga. Ndipo wanaume wawili waliozungumza naye wakaonekana wakiwa pamoja naye. Walikuwa Musa na Eliya.

Petro akamwambia Yesu, “Bwana, ni vizuri tuko hapa. Ukitaka, nitajenga vibanda vitatu,[a] kimoja kwa ajili ya heshima yako, kingine kwa ajili ya heshima ya Musa na kingine kwa ajili ya heshima ya Eliya.”

Petro alipokuwa akizungumza, wingu jeupe liliwafunika. Sauti ikatoka katika wingu na akasema, “Huyu ni Mwanangu, ninayempenda, ninafurahishwa naye. Mtiini yeye!”

Wafuasi waliokuwa na Yesu walipoisikia sauti hii waliogopa sana na wakaanguka chini. Lakini Yesu akawaendea na kuwagusa. Akasema, “simameni, msiogope.” Wafuasi wakatazama juu, wakaona kuwa Yesu yuko peke yake.

Yesu na wafuasi wake walipokuwa wanateremka kutoka mlimani, akawaamuru akisema: “Msimwambie mtu yeyote yale mliyoyaona mlimani. Subirini mpaka Mwana wa Adamu atakapofufuliwa kutoka kwa wafu. Ndipo mtaweza kuwaambia watu juu ya kile mlichokiona.”

10 Wafuasi wakamwuliza Yesu, “Kwa nini walimu wa sheria wanasema ni lazima Eliya aje[b] kabla ya Masihi kuja?”

11 Yesu akajibu, “Wako sahihi kusema ni lazima Eliya aje, na ni kweli kuwa Eliya ataweka mambo yote kama yanavyopaswa kuwa. 12 Lakini ninawaambia, Eliya amekwisha kuja. Watu hawakumjua yeye ni nani, na walimtendea vibaya, wakafanya kama walivyotaka. Ndivyo itakavyokuwa hata kwa Mwana wa Adamu. Watu hao punde tu watamletea mateso Mwana wa Adamu.” 13 Ndipo wafuasi wakaelewa kuwa Yesu aliposema kuhusu Eliya, alikuwa anazungumza juu ya Yohana Mbatizaji.

Yesu Amweka Huru Mvulana Kutoka Pepo Mchafu

(Mk 9:14-29; Lk 9:37-43a)

14 Yesu na wafuasi walirudi kwa watu. Mtu mmoja akamjia Yesu na kuinama mbele zake. 15 Akasema, “Bwana, umwonee huruma mwanangu. Anateswa sana na kifafa alichonacho. Anaangukia kwenye moto au maji mara kwa mara. 16 Nilimleta kwa wafuasi wako, lakini wameshindwa kumponya.”

17 Yesu akajibu, “Ninyi watu mnaoishi katika nyakati hizi cha kizazi kisicho na imani. Maisha yenu ni mabaya sana! Nitakaa nanyi mpaka lini? Nitawavumilia mpaka lini? Mleteni kijana hapa.” 18 Yesu akamwamuru pepo aliye ndani ya kijana, na pepo akamtoka na yule kijana akapona.

19 Kisha wafuasi wakamjia Yesu wakiwa peke yao. Wakasema, “Tulijaribu kumtoa pepo kwa kijana, lakini tulishindwa. Kwa nini tulishindwa kumtoa pepo?”

20 Yesu akajibu, “Mlishindwa kumtoa pepo kwa sababu imani yenu ni ndogo sana. Niaminini ninapowaambia, imani yenu ikiwa na ukubwa wa mbegu ya haradali mtaweza kuuambia mlima huu, ‘Ondoka hapa na uende kule,’ nao utaondoka. Nanyi mtaweza kufanya jambo lolote.” 21 [c]

Yesu Azungumza Kuhusu Kifo Chake

(Mk 9:30-32; Lk 9:43b-45)

22 Baadaye, wafuasi walipokusanyika pamoja Galilaya, Yesu aliwaambia, “Mwana wa Adamu atakabidhiwa kwenye mamlaka ya watu wengine, 23 watakaomwua. Lakini atafufuliwa kutoka kwa wafu siku ya tatu.” Wafuasi waliposikia kuwa Yesu angeuawa walihuzunika sana.

Yesu Afundisha Kuhusu Kulipa Kodi

24 Yesu na wafuasi wake walikwenda Kapernaumu. Walipofika huko watu waliokuwa wakikusanya ushuru wa Hekalu[d] wakamwendea Petro na kumwuliza, “Je, mwalimu wenu hulipa kodi ya Hekalu?”

25 Petro akajibu, “Ndiyo, hulipa.”

Petro akaingia katika nyumba alimokuwa Yesu. Kabla Petro hajazungumza jambo lolote, Yesu akamwambia, “Wafalme wa dunia huchukua kila aina ya kodi kutoka kwa watu. Lakini ni akina nani ambao hutoa kodi? Je, ni jamaa wa familia ya mfalme? Au watu wengine ndiyo hulipa kodi? Unadhani ni akina nani?”

26 Petro akajibu, “Watu wengine ndiyo hulipa kodi.”

Yesu akasema, “Basi wana wa mfalme hawapaswi kulipa kodi. 27 Lakini kwa kuwa hatutaki kuwaudhi watoza ushuru hawa, basi fanya hivi: Nenda ziwani na uvue samaki. Utakapomkamata samaki wa kwanza, mfungue kinywa chake. Ndani ya kinywa chake utaona sarafu nne za drakma mdomoni mwake. Ichukue sarafu hiyo mpe mtoza ushuru. Hiyo itakuwa kodi kwa ajili yangu mimi na wewe.”

Footnotes

  1. 17:4 vibanda vitatu Au “mahema matatu.” Neno hilo limetafsiriwa “hema takatifu” katika Agano la Kale. Hapa limetumika kwa maana ya mahali pa ibada.
  2. 17:10 lazima Eliya aje Tazama Mal 4:5-6.
  3. 17:21 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza mstari wa 21: “Lakini pepo wa aina hii hutoka kwa kufunga na kuomba.”
  4. 17:24 ushuru wa Hekalu Sarafu za kiyunani, drakma Mbili (pia katika mstari wa 27).

The Transfiguration(A)(B)

17 After six days Jesus took with him Peter, James and John(C) the brother of James, and led them up a high mountain by themselves. There he was transfigured before them. His face shone like the sun, and his clothes became as white as the light. Just then there appeared before them Moses and Elijah, talking with Jesus.

Peter said to Jesus, “Lord, it is good for us to be here. If you wish, I will put up three shelters—one for you, one for Moses and one for Elijah.”

While he was still speaking, a bright cloud covered them, and a voice from the cloud said, “This is my Son, whom I love; with him I am well pleased.(D) Listen to him!”(E)

When the disciples heard this, they fell facedown to the ground, terrified. But Jesus came and touched them. “Get up,” he said. “Don’t be afraid.”(F) When they looked up, they saw no one except Jesus.

As they were coming down the mountain, Jesus instructed them, “Don’t tell anyone(G) what you have seen, until the Son of Man(H) has been raised from the dead.”(I)

10 The disciples asked him, “Why then do the teachers of the law say that Elijah must come first?”

11 Jesus replied, “To be sure, Elijah comes and will restore all things.(J) 12 But I tell you, Elijah has already come,(K) and they did not recognize him, but have done to him everything they wished.(L) In the same way the Son of Man is going to suffer(M) at their hands.” 13 Then the disciples understood that he was talking to them about John the Baptist.(N)

Jesus Heals a Demon-Possessed Boy(O)

14 When they came to the crowd, a man approached Jesus and knelt before him. 15 “Lord, have mercy on my son,” he said. “He has seizures(P) and is suffering greatly. He often falls into the fire or into the water. 16 I brought him to your disciples, but they could not heal him.”

17 “You unbelieving and perverse generation,” Jesus replied, “how long shall I stay with you? How long shall I put up with you? Bring the boy here to me.” 18 Jesus rebuked the demon, and it came out of the boy, and he was healed at that moment.

19 Then the disciples came to Jesus in private and asked, “Why couldn’t we drive it out?”

20 He replied, “Because you have so little faith. Truly I tell you, if you have faith(Q) as small as a mustard seed,(R) you can say to this mountain, ‘Move from here to there,’ and it will move.(S) Nothing will be impossible for you.” [21] [a]

Jesus Predicts His Death a Second Time

22 When they came together in Galilee, he said to them, “The Son of Man(T) is going to be delivered into the hands of men. 23 They will kill him,(U) and on the third day(V) he will be raised to life.”(W) And the disciples were filled with grief.

The Temple Tax

24 After Jesus and his disciples arrived in Capernaum, the collectors of the two-drachma temple tax(X) came to Peter and asked, “Doesn’t your teacher pay the temple tax?”

25 “Yes, he does,” he replied.

When Peter came into the house, Jesus was the first to speak. “What do you think, Simon?” he asked. “From whom do the kings of the earth collect duty and taxes(Y)—from their own children or from others?”

26 “From others,” Peter answered.

“Then the children are exempt,” Jesus said to him. 27 “But so that we may not cause offense,(Z) go to the lake and throw out your line. Take the first fish you catch; open its mouth and you will find a four-drachma coin. Take it and give it to them for my tax and yours.”

Footnotes

  1. Matthew 17:21 Some manuscripts include here words similar to Mark 9:29.