Marko 8:14-21
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Wafuasi Washindwa Kumwelewa Yesu
(Mt 16:5-12)
14 Wakati huo huo wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate yo yote, na hawakuwa na kitu kingine isipokuwa mkate mmoja. 15 Yesu akawaonya, akasema, “Mwe mwangalifu! Jilindeni na chachu ya Mafarisayo na ile ya Herode.”
16 Nao wakaanza kujadiliana haya miongoni mwao: “Labda alisema hivi kwa sababu hatukuwa na mkate wowote.”
17 Akijua walichokuwa wakikisema, akawaambia, “Kwa nini mnajadiliana juu ya kutopata mkate? Je! Bado hamwoni na kuelewa? Je! Mmezifunga akili zenu. 18 Mnayo macho; Je! Hamwoni? Mnayo masikio; Je! Hamwezi kusikia? Mnakumbuka? 19 Nilipomega na kugawa mikate mitano kwa watu 5,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?”
Wakasema “Kumi na viwili”.
20 “Nilipomega na kugawa mikate saba kwa watu 4,000, mlikusanya vikapu vingapi vilivyojaa masalia ya mikate?”
Wakasema “Saba”.
21 Kisha akawaambia, “Bado hamwelewi?”
Read full chapter
Marko 8:14-21
Neno: Bibilia Takatifu
Chachu Ya Mafarisayo Na Ya Herode
14 Wanafunzi walikuwa wamesahau kuleta mikate ya kutosha. Walikuwa na mkate mmoja tu kwenye mashua. 15 Yesu akawaonya: “Jihadharini na chachu ya Mafarisayo na ya Herode.”
16 Wakaanza kujadiliana wao kwa wao wakasema,“Anasema hivi kwa kuwa hatukuleta mikate.”
17 Yesu alifahamu majadiliano yao, akawauliza: “Mbona mna zungumzia kuhusu kutokuwa na mikate? Bado hamtambui wala kuelewa? Je, mbona mioyo yenu ni migumu kiasi hicho? 18 Mbona mna macho lakini mnashindwa kuona, na masikio lakini mnashindwa kusikia? Je hamkumbuki? 19 Nilipoimega mikate mitano kuwalisha watu elfu tano, mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Kumi na viwili.” 20 “Na nilipomega mikate saba kuwalisha watu elfu nne mlikusanya mabaki vikapu vingapi?” Wakamjibu, “Saba.” 21 Aka wauliza, “Je, bado tu hamwelewi?”
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica