Marko 15:16-20
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
16 Maaskari wakamwongoza Yesu hadi ndani ya baraza la jumba la gavana (lililojulikana kama Praitorio). Huko wakakiita pamoja kikosi cha maaskari. 17 Wakamvalisha Yesu joho la zambarau na wakafuma taji ya miiba na kumvisha kichwani. 18 Kisha wakaanza kumpigia saluti wakisema: “Heshima kwa Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga tena na tena kichwani kwa fimbo na wakamtemea mate. Kisha wakapiga magoti mbele yake na kujifanya wanampa heshima kama mfalme. 20 Walipomaliza kumkejeli walimvua joho lile la kizambarau, na kumvisha mavazi yake mwenyewe. Baada ya hapo wakamtoa nje ili waweze kumsulubisha.
Read full chapter
Marko 15:16-20
Neno: Bibilia Takatifu
Maaskari Wamdhihaki Yesu
16 Maaskari wakampeleka Yesu hadi kwenye ukumbi wa ndani ya Ikulu iliyoitwa Praitoria, wakakusanya kikosi kizima cha askari. 17 Wakamvika Yesu vazi la zambarau, wakatengeneza taji ya miiba, wakamvika. 18 Wakaanza kumsalimu kwa dhihaka, “Salamu, Mfalme wa Wayahudi!” 19 Wakampiga kwa fimbo kichwani, wakamte mea mate. Wakamdhihaki kwa kupiga magoti kama vile wanamheshimu mfalme. 20 Walipokwisha kumdhihaki, walimvua lile vazi la zam barau, wakamvika nguo zake. Kisha wakamtoa nje wakamsulubishe.
Read full chapter© 2017 Bible League International
Copyright © 1989 by Biblica