Add parallel Print Page Options

Yesu Ajibu Swali Lenye Mtego

(Mt 22:15-22; Lk 20:20-26)

13 Viongozi wa Kidini wakamtumia baadhi ya Mafarisayo na Maherode ili kumkamata kama akisema chochote kimakosa. 14 Wale waliotumwa walifika na kumwambia, “Mwalimu tunajua, kwamba wewe ni mkweli, na tena hujali yale watu wanayoyafikiri kuhusu wewe, kwa sababu wewe hubabaishwi na wadhifa wa mtu. Lakini unafundisha ukweli wa njia ya Mungu. Tuambie ni haki kulipa kodi kwa Kaisari ama la? Je, tulipe au tusilipe?”

15 Lakini Yesu aliutambua unafiki wao na akawaambia, “Kwa nini mnanijaribu hivi? Mniletee moja ya sarafu ya fedha mnazotumia ili niweze kuiangalia.” 16 Hivyo wakamletea sarafu, naye akawauliza, “Je, sura hii na jina hili ni la nani?” Nao wakamwambia, “Ya Kaisari.”

17 Ndipo Yesu alipowaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vyake, na Mungu mpeni vilivyo vyake.” Wakastaajabu sana kwa hayo.

Read full chapter

13 Mafarisayo kadhaa na Maherode walitumwa kuja kumtega Yesu katika maneno yake. 14 Wakamjia, wakamwambia, “Mwalimu, tunafahamu kuwa wewe huwaambia watu ukweli pasipo kujali watu watasema nini. Wala hujali cheo cha mtu bali unafundisha njia ya Mungu kwa kweli. Je, ni halali au si halali kulipa kodi kwa Kais ari? 15 Tulipe kodi hiyo au tusilipe?” Lakini Yesu alitambua hila yao. Akawaambia, “Mbona mnajaribu kunitega? Nileteeni sar afu niione.” 16 Wakamletea. Akawauliza, “Hii ni picha ya nani na hii ni sahihi ya nani?” Wakamjibu, “Ni ya Kaisari.”

17 Basi Yesu akawaambia, “Mpeni Kaisari vilivyo vya Kais ari na vya Mungu mpeni Mungu.” Jibu hili liliwastaajabisha sana.

Read full chapter