Add parallel Print Page Options

13 Wengine wanafanana na mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye mawe. Ni watu ambao huyasikia mafundisho ya Mungu na kuyapokea kwa furaha, lakini kwa kuwa hawana mizizi yenye kina, huamini kwa muda mfupi. Majaribu yanapokuja, humwacha Mungu.

14 Zilizoanguka katika miiba, zinafanana na watu wanaoyasikia Mafundisho ya Mungu, lakini wanaruhusu wasiwasi, mali na anasa za maisha haya kuwasimamisha na hawaendelei kukua. Hivyo mafundisho hayazalishi matokeo mazuri katika maisha yao.[a] 15 Na zile zilizoangukia katika udongo mzuri, ni wale ambao huyasikia mafundisho ya Mungu kwa moyo safi na mnyoofu. Huyatii na kwa uvumilivu wao huzaa mazao mazuri.

Read full chapter

Footnotes

  1. 8:14 hayazalishi matokeo mazuri … yao Hayazalishi matokeo mazuri katika maisha yao ina maana ya, “kukua kiroho”, ama watu hawa hawafanyi mambo mazuri ambayo Mungu anataka wayafanye.

13 Ile miamba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na watu ambao hufurahia kusikia mahu biri lakini neno la Mungu halipenyi ndani ya mioyo yao. Hawa huamini kwa muda mfupi lakini wanapojaribiwa hupoteza imani yao. 14 Na ile miiba ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale wanaosikia neno la Mungu lakini baadaye imani yao inasongwa na mahangaiko ya maisha, utajiri, shughuli na anasa; wasiweze kukua. 15 Bali ule udongo mzuri ambamo mbegu nyingine zilianguka ni sawa na wale ambao hulisikia neno la Mungu na kulishika kwa moyo mwema na wa utii, wakavumilia na kuzaa matunda.”

Read full chapter