Yohana 3:3-7
Neno: Bibilia Takatifu
3 Yesu akamjibu, “Ninakwambia hakika, mtu asipozaliwa mara ya pili, hawezi kuuona Ufalme wa Mungu.”
4 Nikodemo akasema, “Inawezekanaje mtu mzima azaliwe? Anaweza kuingia tena katika tumbo la mama yake na kuzaliwa mara ya pili?”
5 Yesu akamwambia, “Ninakuambia hakika, kama mtu hakuzaliwa kwa maji na kwa Roho hawezi kuingia katika Ufalme wa Mungu. 6 Mtu huzaliwa kimwili na wazazi wake, lakini mtu huzaliwa kiroho na Roho wa Mungu. 7 Kwa hiyo usishangae ninapokuambia kwamba huna budi kuzaliwa mara ya pili.
Read full chapter
Yohana 3:16
Neno: Bibilia Takatifu
16 “Kwa maana Mungu aliupenda ulimwengu kiasi cha kumtoa Mwanae pekee, ili kila mtu amwaminiye asipotee, bali awe na uzima wa milele.
Read full chapter
1 Petro 1:23-25
Neno: Bibilia Takatifu
23 Maana mmezaliwa upya, si kwa mbegu iharibikayo, bali kwa mbegu isiyoharibika, kwa neno la Mungu lililo hai na linalodumu hata milele. 24 Maana, “Binadamu wote ni kama nyasi na utukufu wao ni kama ua la mwituni. Nyasi hunyauka na ua huanguka, 25 lakini neno la Mungu hudumu milele.” Na neno hilo ni Habari Njema ambayo mlihubiriwa.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica