Wagalatia 1:13-24
Neno: Bibilia Takatifu
13 Ninyi mmekwisha sikia juu ya maisha yangu ya zamani nilipokuwa katika dini ya Kiyahudi; jinsi nilivyolitesa kanisa la Mungu na kujaribu kuliangamiza. 14 Nami niliwashinda wengi miongoni mwa Wayahudi wenzangu kwa maana nilikuwa nimejawa na juhudi ya kushika mapo keo ya baba zetu. 15 Lakini yeye aliyenichagua hata kabla sijazaliwa na akaniita kwa neema yake, 16 alipopenda kumdhihiri sha Mwanae kwangu ili nimhubiri miongoni mwa watu wa mataifa, sikushauriana na mtu ye yote. 17 Sikwenda kwanza Yerusalemu kuonana na wale waliokuwa mitume kabla yangu, bali nilikwenda Arabuni, ndipo nikarudi Dameski. 18 Kisha baada ya miaka mitatu nilikwenda Yerusalemu kuo nana na Kefa na nilikaa naye siku kumi na tano. 19 Lakini siku waona wale mitume wengine isipokuwa Yakobo, ndugu yake Bwana. 21 Baadaye nilikwenda sehemu za Siria na Kilikia. 22 Lakini mimi binafsi sikujulikana kwa wakristo wa makanisa ya huko Uyahudi. 23 Ila walisikia wengine wakisema, “Yule mtu ambaye zamani alikuwa akitutesa sasa anahubiri imani ile ile aliyokuwa akitaka kuiangamiza.” 24 Kwa hiyo wakamtukuza Mungu kwa sababu yangu.
Read full chapterCopyright © 1989 by Biblica