1 Timotheo 2
Agano Jipya: Tafsiri ya Kusoma-Kwa-Urahisi
Mungu Anataka Tumwombee Kila Mtu
2 Kwanza kabisa, ninakuagiza uwaombee watu wote. Uwaombee kwa Mungu ili awabariki na kuwapa mahitaji yao. Kisha umshukuru Yeye. 2 Unapaswa kuwaombea watawala na wote wenye mamlaka. Uwaombee viongozi hawa ili tuweze kuishi maisha yenye utulivu na amani, maisha yaliyojaa utukufu kwa Mungu na yanayostahili heshima. 3 Hili ni jambo jema na linampendeza Mungu Mwokozi wetu.
4 Mungu anataka kila mtu aokolewe na aielewe kweli kikamilifu. 5 Kuna Mungu mmoja tu, na kuna mwanadamu mmoja tu anayeweza kuwaleta pamoja wanadamu wote na Mungu wao. Huyo mtu ni Kristo Yesu kama mwanadamu. 6 Alijitoa mwenyewe kulipa deni ili kila mtu awe huru. Huu ni ujumbe ambao Mungu alitupa wakati unofaa. 7 Nami nilichaguliwa kama mtume kuwaambia watu ujumbe huo. Ninasema kweli. Sidanganyi. Nilichaguliwa kuwafundisha wasio Wayahudi na nimefanya kazi hii kwa imani na ukweli.
Maagizo Maalumu kwa Wanawake na Wanaume
8 Nataka wanaume walio kila mahali waombe. Ni lazima wawe watu wanaoishi kwa kumpendeza Mungu na wanaonyoosha mikono yao wanapoomba na wawe watu wasio na hasira na wanaopenda mabishano.
9 Na ninawataka wanawake wajipambe kwa namna inayofaa. Mavazi yao yawe yanayofaa na yanayostahili. Hawapaswi kuvutia watu kwa kutengeneza nywele zao kwa mitindo ya ajabu ama kwa kuvaa dhahabu, vito au lulu au nguo za gharama. 10 Lakini wajipambe na kuvutia kwa matendo mema wanayofanya. Hayo ndiyo yanayofaa zaidi kwa wanawake wanaosema kuwa wamejitoa kwa ajili ya Mungu.
11 Mwanamke anapaswa kujifunza akisikiliza kwa utulivu huku akiwa radhi kutii kwa moyo wake wote. 12 Simruhusu mwanamke kumfundisha mwanaume au kumwelekeza jambo la kufanya. Bali lazima asikilize kwa utulivu, 13 kwa sababu Adamu aliumbwa kwanza na Hawa akaumbwa baadaye. 14 Na Adamu hakudanganywa.[a] Bali mwanamke ndiye aliyedanganywa naye akatenda dhambi. 15 Lakini wanawake wataokolewa kwa jukumu lao la kuzaa watoto.[b] Wakiendelea kuishi katika imani, upendo, utakatifu na tabia njema.
Footnotes
- 2:14 Adamu hakudanganywa “Adamu siye aliyedanganywa” Shetani alimdanganya Hawa, naye Hawa alisababisha Adamu kutenda dhambi. Tazama Mwa 3:1-13.
- 2:15 kuzaa watoto Kwa maana ya kawaida, “Ataokolewa katika kazi yake ya kuzaa watoto.” Kuzaa watoto, inaweza kutumika hapa kama kielelezo cha maana ya “kuzaa sifa njema”, zinazofafanuliwa katika mstari unaofuata.
提摩太前书 2
Chinese New Version (Traditional)
要為萬人禱告
2 1-2 因此,我勸你最重要的是要為萬人、君王和一切有權位的懇求、禱告、代求和感恩,好讓我們可以敬虔莊重地過平靜安穩的日子。 3 在我們的救主 神看來,這是美好的,可蒙悅納的。 4 他願意萬人得救,並且充分認識真理。 5 因為 神只有一位,在 神和人中間也只有一位中保,就是降世為人的基督耶穌。 6 他捨了自己作萬人的贖價,到了適當的時候,這事就證實了。 7 為了這事,我也被派作傳道的和使徒(我說的是真話,不是謊言),在信仰和真理上作外族人的教師。
敬畏 神的女人
8 因此,我願意男人沒有忿怒,沒有爭論,舉起聖潔的手隨處禱告。 9 照樣,我也願意女人以端正、嫻淑、自律為裝飾;不要以鬈髮、金飾、珠寶,或名貴衣裳為裝飾, 10 卻要以善行作裝飾,這才配稱為敬畏 神的女人。 11 女人應該安靜而又完全順服地學習。 12 我不准女人教導,或轄制男人;女人總要安靜。 13 因為先造的是亞當,後造的是夏娃; 14 不是亞當受了引誘,而是女人受了引誘,陷在過犯裡面。 15 然而女人要是常常存著信心、愛心、聖潔自律,在她生育的事上必定得救。
© 2017 Bible League International
Chinese New Version (CNV). Copyright © 1976, 1992, 1999, 2001, 2005 by Worldwide Bible Society.
