Love C.S. Lewis? Sign up for daily inspiration today!

Ndipo Petro akaanza kuwaeleza mambo yote yalivyotokea akasema, “Nil ikuwa nikiomba katika mji wa Jopa, nikaona katika ndoto kitu kama shuka kubwa ikishushwa chini kwa ncha zake nne, kutoka mbinguni, nayo ikanifikia. Nilipotazama kwa makini nikaona wanyama wa kila aina, wanyama wa mwituni, wanyama watambaao na ndege wa angani. Nikasikia sauti ikiniambia, ‘Amka Petro, chinja, ule!’ Nami nikasema, ‘La, Bwana! Sijawahi kula kitu cho chote kili chokatazwa na sheria zetu.’ Lakini ile sauti kutoka mbinguni ikasema kwa mara ya pili, ‘Usiite kitu cho chote alichokitakasa Mungu kuwa ni uchafu.’ 10 Jambo hili lilitokea mara tatu ndipo vyote vikachukuliwa tena mpaka mbinguni. 11 Wakati huo huo watu watatu waliokuwa wametumwa kutoka Kaisaria wakawasili katika nyumba niliyokuwa nikikaa. 12 Roho akaniambia niende nao bila kusita. Nikaenda nao nikisindikizwa na hawa ndugu sita, tukaingia katika nyumba ya Kornelio. 13 Kornelio akatuambia jinsi malaika alivyomtokea akamwambia, ‘Tuma watu Jopa wakamwite Simoni aitwaye Petro. 14 Yeye anao ujumbe utakaokuokoa wewe na wote walio nyum bani mwako.’ 15 Nami nilipokuwa nikisema nao, Roho Mtakatifu akashuka juu yao kama alivyotushukia sisi mwanzoni. 16 Nami nikakumbuka jinsi Bwana alivyosema, ‘Yohana alibatiza kwa maji, lakini ninyi mtabatizwa kwa Roho Mtakatifu.’ 17 Basi kwa kuwa Mungu ndiye aliyewapa hawa watu karama ile ile aliyotupa sisi tulipomwamini Bwana Yesu, mimi ni nani hata nimpinge Mungu?”

Read full chapter