Walimu Wa Uongo

10 Maana wapo wakaidi wengi, waliojaa maneno matupu na waongo, hasa kile kikundi cha tohara. 11 Hao ni lazima wanyamaz ishwe kwa sababu wanapotosha jamaa nzima kwa kufundisha mambo wasiyostahili kufundisha. Wanafanya hivyo kusudi wajipatie fedha. 12 Hata mmojawapo wa manabii wao amesema: “Wakrete ni waongo siku zote, ni kama wanyama wabaya, walafi na wavivu.” 13 Maneno hayo ni kweli kabisa. Kwa hiyo uwakemee kwa ukali ili wapate kuwa imara katika imani. 14 Wasiendelee kushikilia hadithi za Kiy ahudi au maagizo ya watu wanaokataa ukweli. 15 Kwa watu walio safi, kila kitu ni safi. Lakini kwa watu waovu na wasioamini, hakuna kilicho safi. Mawazo yao na dhamiri zao zimejaa uovu.

16 Wanajidai kuwa wanamjua Mungu lakini wanamkana kwa matendo yao. Ni watu wa kuchukiza, waasi, wasiofaa kwa jambo lo lote jema.

Read full chapter