12 Watu wote waliotenda dhambi pasipokuwa na sheria ya Musa wataangamia pasipo sheria; na wale wote waliotenda dhambi chini ya sheria ya Musa watahukumiwa kwa sheria iyo hiyo. 13 Kwa maana wanaohesabiwa haki mbele ya Mungu si wale wanaosikia bali ni wal ewanaotii maagizo ya sheria. 14 Watu wa mataifa mengine ambao hawana sheria ya Musa, wanapoamua kutenda yale ambayo yameagizwa na sheria kwa kuongozwa na dhamiri zao, wao wenyewe wanakuwa wamejiwekea sheria, ingawa hawana sheria ya Musa. 15 Kwa jinsi hii matendo yao yanaonyesha kwamba yale yaliyoagizwa katika she ria ya Musa yameandikwa ndani ya mioyo yao. Dhamiri zao pia hush uhudia hivyo; kwa maana mawazo yao mara nyingine huwashtaki na mara nyingine huwatetea. 16 Kwa hiyo, kama Habari Njema ninay ohubiri inavyosema, hivyo ndivyo itakavyokuwa siku ile ambayo Mungu, kwa njia ya Yesu Kristo, atayahukumu mawazo ya siri ya wanadamu.

Read full chapter

12 Watu walio na sheria na wote ambao hawajawahi kuisikia sheria, wote wako sawa wanapotenda dhambi. Watu wasio na sheria na ni watenda dhambi wataangamizwa. Vivyo hivyo, wale walio na sheria na ni watenda dhambi watahukumiwa kuwa na hatia kwa kutumia sheria. 13 Kuisikia sheria hakuwafanyi watu wawe wenye haki kwa Mungu. Wanakuwa wenye haki mbele zake, pale wanapotekeleza kile kinachoagizwa na sheria.

14 Fikirini kuhusu wasio Wahayudi ambao hawakukua wakiwa na sheria. Wanapotenda kama sheria inavyoamuru,[a] wanakuwa kielelezo cha sheria, ijapokuwa hawana sheria iliyoandikwa. 15 Wanaonesha kuwa wanafahamu kilicho sahihi na kibaya, kama sheria inavyoamuru na dhamiri zao zinakubali. Lakini wakati mwingine mawazo yao huwaambia kuwa wamekosea au wamefanya sahihi. 16 Hivi ndivyo itakavyokuwa siku ambayo Mungu atazihukumu siri za watu kupitia Yesu Kristo, sawasawa na Habari Njema ninayoihubiri.

Read full chapter

Footnotes

  1. 2:14 Wanapotenda kama sheria inavyoamuru Au “… hawana sheria. Lakini wanapotenda yale yanayoamriwa na sheria kwa kufuata utashi wa asili …”.