Malaika wa tatu aliwafuata hao wawili akisema kwa sauti kuu, “Kama mtu ye yote anamwabudu yule mnyama na sanamu yake na kukubali kutiwa alama yake kwenye kipaji cha uso wake au kwenye mkono wake, 10 yeye naye atakunywa divai ya ghadhabu ya Mungu ambayo imemiminiwa katika kikombe cha ghadhabu yake bila kuchan ganywa na maji. Naye atateswa kwa moto na kiberiti mbele ya mal aika watakatifu na mbele za Mwana-Kondoo. 11 Moshi wa mateso yao hupanda juu milele na milele; wala hakuna nafuu, mchana au usiku, kwa wale wamwabuduo huyo mnyama na sanamu yake au kwa ye yote anayepokea alama ya jina lake.”

Read full chapter