ijapokuwa mimi mwenyewe ninazo sababu za kuweka matumaini katika mambo hayo. Kama mtu mwingine ye yote anadhani kuwa anazo sababu za kuweka matumaini yake katika mambo ya mwili, basi mimi ninazo sababu zaidi. Nilitahiriwa siku ya nane, mimi ni Mwis raeli wa kabila la Benjamini; Mwebrania halisi. Kuhusu mambo ya kushika sheria, mimi nilikuwa Mfarisayo; na kwa upande wa juhudi, mimi nilikuwa na bidii katika kutesa kanisa; na kuhusu haki ipatikanayo kwa kutii sheria, mimi nilikuwa sina hatia.

Lakini mambo hayo niliyoyaona mwanzo kuwa ni faida kwangu, sasa nayaona kuwa ni hasara kwa ajili ya Kristo. Zaidi ya hayo, nahesabu mambo yote kuwa hasara tupu yakilinganishwa na faida kubwa ninayopata kwa kumjua Kristo Yesu aliye Bwana wangu. Kwa ajili yake nilikubali kupoteza kila kitu na kuona mambo hayo yote kuwa ni takataka ili nipate faida ya kuwa na Kristo; na nikiwa kwake nisionekane kama mtu mwenye haki yake mwenyewe, inayotokana na kushika sheria, bali niwe na ile haki inayotokana na kumwamini Kristo, ambaye yeye ni haki itokayo kwa Mungu inayopatikana kwa imani.

Read full chapter