34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Read full chapter