34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Read full chapter

34 Lakini ninawaambia mnapoweka ahadi, msiape kwa jina la mbingu, kwa sababu mbingu ni kiti cha enzi cha Mungu. 35 Na usiape kwa jina la dunia kwa sababu, dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Wala msiape kwa jina la mji wa Yerusalemu, kwa sababu nao ni mali yake Mungu, aliye Mfalme Mkuu. 36 Pia usiape kwa jina la kichwa chako kana kwamba ni uthibitisho kuwa utatimiza kiapo, kwa sababu huwezi kuufanya hata unywele mmoja wa kichwa chako kuwa mweusi au mweupe. 37 Sema ‘ndiyo’ tu kama una maana ya ndiyo na ‘hapana’ tu kama una maana ya hapana. Ukisema zaidi ya hivyo, utakuwa unatoa kwa Yule Mwovu.

Read full chapter