10 Na hata sasa shoka la hukumu ya Mungu limewekwa tayari katika mashina ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa katwa na kutupwa motoni.

11 “Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Pepeto lake liko mkononi, naye atasafisha pa kupepetea nafaka, na ngano yake ataiweka ghalani; lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

Read full chapter

10 Shoka limewekwa tayari kukata shina la mti katika mizizi yake. Kila mti[a] usiozaa matunda mazuri utakatwa vivyo hivyo na kutupwa motoni.

11 Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Naye atakuja akiwa tayari kwa ajili ya kuisafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri kutoka kwenye makapi,[b] na kisha ataiweka nafaka nzuri kwenye ghala yake. Kisha atayachoma makapi kwa moto usiozimika.”

Read full chapter

Footnotes

  1. 3:10 mti Watu wasiomtii Mungu ni kama “miti” itakayokatwa.
  2. 3:12 Atatenganisha nafaka … makapi Inamaanisha kuwa Yesu atawatenganisha watu wema na waovu.