Walinzi Wa Kaburi

62 Siku iliyofuata, yaani siku iliyofuata ile siku ya Maan dalizi ya sabato, makuhani wakuu na Mafarisayo walimwendea Pilato 63 wakamwambia, “Tunakumbuka kwamba yule mwongo alisema, ‘Baada ya siku tatu nitafufuka.’ 64 Tunaomba uamuru kwamba kabu ri liwekewe ulinzi hadi siku ya tatu. Vinginevyo wanafunzi wake wanaweza wakaja wakauiba mwili wake na kuwaambia watu kwamba amefufuka. Jambo hili likitokea uongo huu wa mwisho utakuwa mbaya zaidi ya ule wa kwanza.” 65 Pilato akawaambia, “Ninyi mnao askari. Nendeni mkaweke ulinzi, mhakikishe pamekuwa salama kama mpendavyo.” 66 Wakaenda wakaweka ulinzi kaburini, wakaliwekea lile jiwe mhuri na kuwaweka askari walinzi.

Read full chapter

Kaburi la Yesu Lalindwa

62 Siku ile ilikuwa Siku ya Maandalizi. Siku iliyofuata, viongozi wa makuhani na Mafarisayo walimwendea Pilato. 63 Wakamwambia, “Mkuu, tunakumbuka kuwa yule mwongo alipokuwa hai alisema, ‘Nitafufuka kutoka kwa watu katika siku tatu.’ 64 Hivyo amuru ili kaburi lilindwe kwa siku tatu. Wafuasi wake wanaweza kuja na kujaribu kuiba mwili. Kisha wataweza kumwambia kila mtu kuwa alifufuka kutoka kwa wafu. Uongo huo utakuwa hatari zaidi ya hata waliyosema juu yake alipokuwa hai.”

65 Pilato akasema, “Chukueni baadhi ya askari, na mwende mkalinde kaburi kwa namna mnavyojua.” 66 Kisha walikwenda kaburini na kuliweka salama dhidi ya wezi. Walifanya hivi kwa kuliziba kwa jiwe langoni na kuwaweka askari wa kulinda kaburi.

Read full chapter