29 “Ole wenu, walimu wa sheria na Mafarisayo, ninyi wana fiki! Mnajenga makaburi ya manabii na kupamba makaburi ya wenye haki 30 mkisema, ‘Kama tungaliishi wakati wa baba zetu tusingel ishiriki katika kuwaua manabii !’ 31 Kwa kusema hivyo mnakiri kwamba ninyi ni wana wa wale waliowaua manabii. 32 Haya basi, kamilisheni hiyo kazi waliyoianza baba zenu! 33 Ninyi nyoka, ninyi kundi la nyoka! Mtaepukaje hukumu ya Jehena? 34 Kwa sababu hiyo nawapelekea manabii na wenye hekima na walimu. Baadhi yao mtawaua na kuwatundika msalabani, wengine mtawapiga mijeledi katika masinagogi yenu na wengine mtawatesa toka mji mmoja hadi mji mwingine. 35 Na kwa hiyo damu ya wote wenye haki ambayo imemwagwa hapa duniani, tangu damu ya Abeli, ambaye alikuwa hana hatia, hadi damu ya Zakaria mwana wa Barakia ambaye mlimwua kati kati ya Patakatifu na madhabahu, itakuwa juu yenu. 36 Nawaambia kweli haya yote yatatokea wakati wa kizazi hiki.”

Read full chapter

29 Ole wenu walimu wa sheria na Mafarisayo! Ninyi ni wanafiki! Mnajenga makaburi ya manabii, na kuyaheshimu makaburi ya wenye haki waliouawa. 30 Na mnasema, ‘Ikiwa tungeishi nyakati za mababu zetu, tusingewasaidia kuwaua manabii hawa.’ 31 Hivyo mnathibitisha kuwa ninyi ni uzao wa wale waliowaua manabii. 32 Na mtaimalizia dhambi waliyoianza mababu zenu!

33 Enyi nyoka! Ninyi mlio wa uzao wa nyoka wenye sumu kali! Hamtaikwepa adhabu. Mtahukumiwa na kutupwa Jehanamu! 34 Hivyo ninawaambia: Ninawatuma manabii na walimu wenye hekima na wanaojua Maandiko. Lakini mtawaua, mtawatundika baadhi yao kwenye misalaba na kuwapiga wengine katika masinagogi yenu. Mtawafukuza kutoka katika mji mmoja hadi mwingine.

35 Hivyo mtakuwa na hatia kutokana vifo vyote vya watu wema wote waliouawa duniani. Mtakuwa na hatia kwa kumwua mtu wa haki Habili, na mtakuwa na hatia kwa kuuawa kwa Zakaria[a] mwana wa Barakia mliyemwua kati ya Hekalu na madhabahu. Mtakuwa na hatia ya kuwaua watu wote wema walioishi kati ya wakati wa Habili mpaka wakati wa Zakaria. 36 Niaminini ninapowaambia kuwa mambo haya yote yatawapata ninyi watu mnaoishi sasa.

Read full chapter

Footnotes

  1. 23:35 Habili, Zakaria Katika Agano la Kale la Kiebrania, hawa ni watu wa kwanza na wa mwisho kuuawa. Tazama Mwa 4:8-11 na 2 Nya 24:20-25.