Mfano Wa Wana Wawili

28 ‘Lakini mwaonaje? Mtu mmoja alikuwa na watoto wawili wa kiume. Akamwendea yule wa kwanza akamwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ 29 Yule mwanae akasema, ‘Siendi,’ lakini baadaye akabadili mawazo akaenda. 30 Kisha yule baba akamwendea yule mwanae mwingine akamwambia vile vile. Yeye akajibu, ‘Nitakwenda baba,’ lakini asiende. 31 Ni yupi kati yao aliyetimiza alivyotaka baba yake?” Wakamjibu, “Yule wa kwanza.” Yesu akawaambia, “Nawaambieni kweli, watoza ushuru na makahaba wanawatangulia kuingia katika Ufalme wa Mungu.

32 Kwa maana Yohana alikuja kwenu kuwaonyesha njia ya haki, lakini hamkumwamini, ila watoza ushuru na makahaba walimwamini. Nanyi hata mlipoona hayo, baadaye hamkutubu na kum wamini.”

Read full chapter

Yesu Atumia Simulizi Kuhusu Wana Wawili

28 “Niambieni mnafikiri nini kuhusu hili: Alikuwepo mtu mwenye wana wawili. Alimwendea mwanaye wa kwanza na kumwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’

29 Mwanaye akasema, ‘Siendi.’ Lakini baadaye akabadili uamuzi wake na akaenda.

30 Kisha baba akamwendea mwanaye mwingine na kumwambia, ‘Mwanangu, nenda ukafanye kazi kwenye shamba la mizabibu leo.’ Akajibu, ‘Sawa baba, nitakwenda kufanya kazi.’ Lakini hakwenda.

31 Ni yupi kati ya wana hawa wawili alimtii baba yake?”

Viongozi wa Kiyahudi wakajibu, “Ni mwana wa kwanza.”

Yesu akawaambia, “Ukweli ni huu, ninyi ni wabaya kuliko watoza ushuru na makahaba. Ukweli ni kuwa hao wataingia katika ufalme wa Mungu kabla yenu. 32 Yohana alikuja akiwaonesha njia sahihi ya kuishi, na hamkumwamini. Lakini watoza ushuru na makahaba walimwamini Yohana. Mliona yaliyotokea, lakini hamkubadilika na mlikataa kumwamini.

Read full chapter