Baadhi ya Mafarisayo wakamjia wakamtega kwa kumwuliza, “Ni halali mtu kumwacha mke wake kwa sababu yo yote ile?”

Akawajibu, “Hamjasoma kwamba aliyewaumba tangu mwanzo ali waumba mume na mke akawaambia, ‘Kwa sababu hii mtu atamwacha baba yake na mama yake na aambatane na mkewe; na hao wawili wata kuwa mwili mmoja’? Kwa hiyo hawawi wawili tena, bali ni mwili mmoja. Kwa hiyo alichokiunganisha Mungu, mwanadamu asikitengan ishe.”

Wakamwuliza, “Kwa nini basi Musa aliagiza kwamba mtu anaweza kumpa mkewe hati ya talaka na kumwacha?” Yesu akawa jibu, “Musa aliwaruhusu kuwaacha wake zenu kwa sababu mioyo yenu ni migumu. Lakini tangu mwanzo haikukusudiwa iwe hivyo. Nami nawaambieni, mtu ye yote anayemwacha mkewe, isipokuwa kwa sababu ya uasherati, akaoa mke mwingine, anazini.” [“Na mtu anayemwoa mwanamke aliyepewa talaka pia anazini.”]

10 Wanafunzi wake wakamwambia, “Kama hivi ndivyo hali ilivyo kati ya mume na mke, basi ni afadhali mtu asioe!” 11 Yesu akajibu, “Si kila mtu anaweza kupokea mafundisho haya isipokuwa wale ambao Mungu amewajalia. 12 Kwa maana wako watu wasioweza kuoa kwa sababu wamezaliwa na hali hiyo; na wengine wamefanywa hali hiyo na binadamu; na pia wako wengine ambao wameamua kutokuoa kwa ajili ya Ufalme wa mbinguni. Awezaye kuli pokea fundisho hili na alipokee.”

Read full chapter