17 Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Leteni hapa.” 19 Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20 Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.

Read full chapter