Yesu Alisha Zaidi Ya Watu Elfu Tano

13 Yesu aliposikia haya, aliondoka kwa mashua akaenda mahali pasipo na watu ili awe peke yake. Lakini watu wal ipata habari, wakamfuata kwa miguu kupitia nchi kavu, kutoka mij ini. 14 Yesu alipofika kando ya bahari aliona umati mkubwa wa watu, akawahurumia na akawaponya wagonjwa wao.

15 Ilipofika jioni, wanafunzi wake walimfuata wakamwambia, “Mahali hapa ni nyikani, na siku imekwisha. Waage watu waondoke ili wakajinunulie chakula vijijini.” 16 Yesu akasema, “Hakuna sababu ya wao kuondoka. Ninyi wapeni chakula.” 17 Wakamjibu, “Hapa tuna mikate mitano na samaki wawili tu.” 18 Akawaambia, “Leteni hapa.” 19 Akaagiza wale watu wakae chini kwenye nyasi. Akaichukua ile mikate mitano na wale samaki wawili, akainua macho yake akatazama mbinguni, akaibariki. Akaimega ile mikate akawapa wanafunzi wake, nao wakawapa watu. 20 Wote wakala, wakatosheka. Na wanafunzi wake wakakusanya vipande vipande vilivyosalia, waka jaza vikapu kumi na viwili. 21 Idadi ya watu waliokula, bila kuhesabu wanawake na watoto, ilikuwa kama wanaume elfu tano.

Read full chapter