Kisha akawaambia mambo mengi kwa mifano, akasema: “Mpanzi alikwenda kupanda mbegu. Alipokuwa akitawanya mbegu, baadhi zikaanguka njiani, ndege wakaja wakazila. Nyingine zikaanguka kwenye mawe, ambapo hapakuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka kwa sababu udongo ulikuwa kidogo. Lakini jua kali lilipowaka, mimea hiyo ilinyauka na kukauka kwa sababu mizizi yake haikwenda chini. Mbegu nyingine zilianguka kwenye miiba. Miiba hiyo ikakua ikazisonga. Mbegu nyingine zilianguka kwenye udongo mzuri zikatoa mazao, nyingine mara mia moja zaidi ya mbegu zilizopandwa, nyingine mara sitini na nyingine mara the lathini. Mwenye nia ya kusikia na asikie.”

Read full chapter