Yesu Anamponya Mtu Aliyepooza Mkono

Yesu alipoondoka hapo, aliingia katika sinagogi lao. Huko alikuwepo mtu aliyepooza mkono . 10 Wakitafuta sababu ya kumsh taki, wakamwuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya sabato?” 11 Yesu akawajibu, “Ni nani kati yenu ambaye kondoo wake aki tumbukia shimoni siku ya sabato hatamtoa? 12 Mtu ana thamani kubwa sana kuliko kondoo. Kwa hiyo ni halali kutenda mema siku ya sabato.”

13 Ndipo akamwambia yule mtu, “Nyoosha mkono wako.” Akau nyoosha, nao ukapona ukawa mzima kama ule mwingine. 14 Lakini Mafarisayo wakatoka nje wakashauriana jinsi ya kumwangamiza

Mtumishi Aliyechaguliwa Na Mungu

15 Lakini Yesu akiyafahamu mawazo yao, aliondoka mahali hapo. Na watu wengi walimfuata naye akawaponya wote. 16 Akawa kataza wasimtangaze. 17 Hii ilikuwa ili yatimie maneno aliyosema nabii Isaya: 18 “Mtazameni mtumishi wangu niliyemchagua, mpendwa wangu ambaye moyo wangu unapendezwa naye. Nitaweka Roho yangu juu yake , naye atatangaza haki kwa watu wa mataifa. 19 Hatabishana wala hatapiga kelele, sauti yake haitasikika mitaani. 20 Hataponda unyasi uliochubuliwa wala hatazima mshumaa unaokaribia kuzima, mpaka atakapoifanya haki ipate ushindi; 21 na watu wa mataifa wataweka tumaini lao katika jina lake.”

Read full chapter