21 “Ole wenu watu wa Korazini! Ole wenu watu wa Bethsaida! Kwa maana kama matendo makuu yaliyofanyika kwenye miji yenu yangelifanyika Tiro na Sidoni, watu wa huko wangelikuwa wametubu tangu zamani na kuvaa magunia na kujipaka majivu, kudhihirisha kujuta kwao. 22 Lakini nawaambia, siku ile ya hukumu itakuwa nafuu kwa Tiro na Sidoni kuliko itakavyokuwa kwenu. 23 Na ninyi watu wa Kapernaumu, mnadhani mtainuliwa hadi juu mbinguni? Mtashushwa hadi kuzimuni. Kwa kuwa kama mambo makuu yaliyofanyika kwenu yangalifanyika huko Sodoma, mji huo ungalikuwapo hadi leo.

Read full chapter