Ukoo Wa Yesu Kristo

Kumbukumbu ya vizazi vya ukoo wa Yesu Kristo mwana wa Daudi na wa Abrahamu: Abrahamu alikuwa baba yake Isaka; Isaka alikuwa baba yake Yakobo; na Yakobo alikuwa baba yake Yuda na ndugu zake. Yuda alikuwa baba yake Peresi na Zera ambao mama yao alikuwa Tamari; Peresi alikuwa baba yake Esroni; Esroni alikuwa baba yake Aramu; Aramu alikuwa baba yake Aminadabu; Aminadabu alikuwa baba yake Nashoni; Nashoni alikuwa baba yake Salmoni; Salmoni alikuwa baba yake Boazi na mama yake Salmoni alikuwa Rahabu. Boazi alikuwa baba yake Obedi, ambaye mama yake alikuwa Ruti; Obedi alikuwa baba yake Yese; Yese alikuwa baba yake Daudi ambaye alikuwa mfalme. Daudi alikuwa baba yake Solomoni ambaye mama yake ni yule aliyekuwa mke wa Uria; Solomoni alikuwa baba yake Rehoboamu; Rehoboamu alikuwa baba yake Abiya; Abiya alikuwa baba yake Asa; Asa alikuwa baba yake Yehoshafati; Yehoshafati alikuwa baba yake Yoramu; Yoramu alikuwa baba yake Uzia; Uzia alikuwa baba yake Yothamu; Yothamu alikuwa baba yake Ahazi; Ahazi alikuwa baba yake Hezekia; 10 Hezekia alikuwa baba yake Manase; Manase alikuwa baba yake Amoni; Amoni alikuwa baba yake Yosia; 11 wakati wa uhamisho wa Babiloni, Yosia alimzaa Yekonia na ndugu zake; 12 na baada ya uhamisho wa Babiloni Yekonia alimzaa Shealtieli; Shealtieli alikuwa baba yake Zerubabeli; 13 Zeru babeli alikuwa baba yake Abihudi; Abihudi alikuwa baba yake Eliakimu ; Eliakimu alikuwa baba yake Azori; 14 Azori alikuwa baba yake Zadoki; Zadoki alikuwa baba yake Akimu; Akimu alikuwa baba yake Eliudi; 15 Eliudi alikuwa baba yake Elieza; Elieza alikuwa baba yake Matani; Matani alikuwa baba yake Yakobo; 16 Yakobo alikuwa baba yake Yosefu ambaye alikuwa mumewe Mar ia, aliyemzaa Yesu anayeitwa Kristo. 17 Basi, kulikuwepo vizazi kumi na vinne tangu Abrahamu mpaka wakati wa mfalme Daudi; na vizazi kumi na vinne tangu mfalme Daudi hadi wakati wa uhamisho wa Babiloni na vizazi kumi na vinne tangu wakati wa uhamisho hadi Kristo.

Kuzaliwa Kwa Yesu Kristo

18 Kuzaliwa kwake Yesu Kristo kulikuwa hivi: Maria mama yake, alikuwa ameposwa na Yosefu. Lakini kabla ya ndoa yao, Mar ia akiwa bado bikira, alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 19 Kwa kuwa Yosefu alikuwa mtu mwema hakutaka kumwaibisha mchumba wake Maria hadharani. Kwa hiyo aliamua kuvunja uchumba wao kwa siri. 20 Lakini alipokuwa bado anawaza juu ya jambo hili, malaika wa Bwana akamtokea katika ndoto akasema, “Yosefu mwana wa Daudi, usisite kumwoa Maria mchumba wako kwa maana mimba aliyo nayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Naye atamzaa mtoto wa kiume, nawe utamwita jina lake Yesu; kwa maana yeye ndiye atakayewaokoa watu wake kutoka katika dhambi zao.”

22 Hayo yote yalitokea ili kutimiza maneno ya Mungu yaliyos emwa na nabii wake: 23 “Tazama bikira atachukua mimba, naye atamzaa mtoto wa kiume nao watamwita Imanueli,” maana yake, “Mungu pamoja nasi”. 24 Yosefu alipoamka usingizini, alifanya kama alivyoagizwa na malaika wa Bwana; akamchukua mkewe Maria nyumbani kwake, 25 lakini hawakukaribiana mpaka Maria alipoji fungua mtoto wa kiume. Yosefu akamwita jina lake Yesu.

Wataalamu Wa Nyota Wafika Kumwona Mtoto Yesu

Basi Yesu alipozaliwa katika mji wa Betlehemu huko Yudea, wakati wa utawala wa mfalme Herode, wataalamu wa mambo ya nyota kutoka Mashariki walifika Yerusalemu wakawa wakiuliza, kutoka kwao kuhusu wakati kamili ambao ile nyota ilionekana.

Mfalme Herode alipopata habari hizi alifadhaika sana na watu wote wa Yerusalemu wakawa na hali ya wasiwasi. Herode akaitisha mkutano wa makuhani wakuu na waandishi, akawataka wamweleze mahali ambapo Kristo angezaliwa.

Wakamjibu, “Atazaliwa Betlehemu ya Yudea, kwa maana nabii aliandika hivi kuhusu jambo hili: ‘Nawe Betlehemu, katika nchi ya Yuda, wewe si wa mwisho miongoni mwa watawala wa Yuda; kwa maana atatoka mtawala kwako atakayetawala watu wangu Israeli.’ ”

Ndipo Herode akawaita wale wataaamu wa nyota kwa siri aka pata uhakikisho Halafu akawatuma Bethlehemu akiwaagiza, “Nendeni mkamtafute huyo mtoto kwa bidii, na mkishampata, mnile tee habari ili na mimi niende kumsujudia.”

Baada ya kumsikiliza mfalme, wale wataalamu wa nyota wakaendelea na safari, na mbele yao wakaiona ile nyota waliyoiona mashariki ikiwatangulia, nao wakaifuata mpaka iliposimama juu ya mahali pale alipokuwa mtoto. 10 Walipoiona ile nyota walijawa na furaha isiyoelezeka.

11 Walipoingia ndani ya ile nyumba walimwona mtoto na mama yake Mariamu, wakainama chini kwa heshima kubwa wakamwabudu. Kisha wakafungua mikoba yao, wakampa zawadi: dhahabu, uvumba na manemane. 12 Na baada ya kuonywa katika ndoto wasirudi kwa Her ode , wakarudi makwao kwa kupitia njia nyingine.

Yosefu, Maria Na Mtoto Yesu Wakimbilia Misri

13 Walipokwisha kuondoka, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto akamwambia, “Amka, umchukue mtoto na mama yake mkimbilie Misri na mkae huko mpaka hapo nitakapowaambia; kwa maana mfalme Herode ataanza msako wa kumtafuta huyu mtoto ili amwue.” 14 Kwa hiyo akaamka, akamchukua mtoto na mama yake usiku, wakaelekea Misri 15 na wakakaa huko mpaka Herode alipo fariki. Na hivyo likatimia neno alilosema Bwana hupitia nabii: ‘Nilimwita mwanangu kutoka Misri.’

16 Herode alipogundua kwamba wale wataalamu wa nyota wame mdanganya, alikasirika sana, akawatuma watu kuwaua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili kwenda chini katika mji wa Betlehemu na sehemu zote za jirani, kufuatana na ule muda ambao wale wataalamu walikuwa wamemhakikishia. 17 Ndipo maneno yaliy osemwa hupitia nabii Yeremia yakatimia kama alivyosema:

18 “Sauti ilisikika huko Rama, kilio cha uchungu na maom bolezo; Raheli akiwalilia wanae; hakukubali kufarijiwa kwa sababu walikuwa wamekufa.”

19 Lakini Herode alipofariki, malaika wa Bwana alimtokea Yosefu katika ndoto huko Misri, 20 akamwambia, “Amka mchukue mtoto na mama yake, mrudi katika nchi ya Israeli kwa sababu wale waliotaka kumwua mtoto wamefariki.”

21 Basi Yosefu akaamka, akamchukua mtoto na mama yake wakar udi nchi ya Israeli. 22 Lakini alipopata habari kwamba Arkelao alikuwa akimiliki huko Yudea mahali pa baba yake Herode, aliogopa kwenda huko; na baada ya kuonywa tena katika ndoto, aliondoka akaenda wilaya ya Galilaya. 23 Akaenda kuishi katika mji ulioitwa Nazareti, na hivyo yakatimia yale yaliyosemwa kupitia manabii kwamba, “Ataitwa Mnazareti.”

Mahubiri Ya Yohana Mbatizaji

Siku hizo Yohana Mbatizaji alitokea akihubiri katika nyika ya Yudea, akisema, “Tubuni, muache dhambi zenu, mumgeukie Mungu; kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.” Huyu ndiye aliyezungumzwa na nabii Isaya aliposema, “Sauti ya mtu anayeita kwa sauti kubwa huko nyikani, ‘Tayarisheni njia ya Bwana, nyoosheni sehemu zote atakazopitia.’ ”

Yohana Mbatizaji alivaa nguo zilizotengenezwa kwa manyoya ya ngamia na kiunoni mwake alijifunga mkanda wa ngozi; chakula chake kilikuwa nzige na asali mwitu. Watu walimwendea kutoka Yerusalemu, Yudea yote na bonde lote la mto Yordani. Nao walipoungama dhambi zao aliwabatiza katika mto Yordani. Lakini alipowaona Mafarisayo na Masadukayo wengi wakija ili awabatize, aliwaambia, “Ninyi watoto wa nyoka! Ni nani aliyewaonya muepuke ghadhabu inayokuja? Basi thibitisheni kwa mwenendo mwema kwamba mmeziacha dhambi zenu. Wala msidhani mnaweza kujitetea mkisema, ‘Sisi ni wana wa Ibrahimu 10 Na hata sasa shoka la hukumu ya Mungu limewekwa tayari katika mashina ya miti. Kila mti usiozaa matunda mazuri, utakatwa katwa na kutupwa motoni.

11 “Mimi nawabatiza kwa maji kama ishara kwamba mmetubu dhambi zenu. Lakini baada yangu anakuja aliye mkuu kuliko mimi, ambaye sistahili hata kuchukua viatu vyake. Yeye atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Pepeto lake liko mkononi, naye atasafisha pa kupepetea nafaka, na ngano yake ataiweka ghalani; lakini makapi atayachoma kwa moto usiozimika.”

Yesu Abatizwa

13 Kisha Yesu akaja kutoka Galilaya mpaka mto Yordani ili abatizwe na Yohana. 14 Yohana alitaka kumzuia akimwambia, “Mimi ndiye ninahitaji kubatizwa na wewe, mbona unakuja kwangu? ” 15 Lakini Yesu akamjibu, “Kubali iwe hivi kwa sasa; kwa maana inatupasa kutimiza haki yote.” Kwa hiyo Yohana akakubali.

16 Na Yesu alipokwisha kubatizwa alitoka kwenye maji, ghafla mbingu zilifunguka, akamwona Roho wa Mungu akishuka kama hua aka kaa juu yake. 17 Na sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ndiye

Yesu Ajaribiwa Na Shetani

Kisha Yesu akaongozwa na Roho Mtakatifu mpaka nyikani ili akajaribiwe na shetani. Akakaa huko siku arobaini akifunga, pasipo kula kitu cho chote mchana na usiku, hatimaye akaona njaa. Ndipo shetani akamjia akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

Mungu, amuru mawe haya yawe mikate.”

Lakini Yesu akamjibu, “Imeandikwa, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila neno analotamka Mungu.’ ”

Ndipo shetani akampeleka Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerus alemu, akamweka juu ya mnara wa Hekalu, akamwambia, “Kama wewe ni Mwana wa Mungu jitupe chini; kwa kuwa imeandikwa, ‘Atawaagiza malaika wake wakuhudumie,’ na, ‘Watakuinua juu mikononi mwao ili usijikwae mguu wako kwenye jiwe.’ ”

Yesu akamjibu, “Pia imeandikwa, ‘Usimjaribu Bwana Mungu wako.’ ”

Kwa mara nyingine shetani akamchukua Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima mrefu akamwonyesha milki zote za dunia na fahari zake, kisha akamwambia, “Nitakupa hivi vyote kama ukipiga magoti na kuniabudu.”

10 Yesu akamwambia, “Ondoka hapa shetani! Kwa maana imean dikwa, ‘Utamwabudu Bwana Mungu wako na utamtumikia yeye peke yake.’ ” 11 Ndipo shetani akamwacha, na malaika wakaja wakamhu dumia.

Yesu Aanza Kuhubiri

12 Yesu aliposikia kwamba Yohana Mbatizaji alikuwa ameka matwa na kuwekwa gerezani, alirudi Galilaya. 13 Akaondoka Nazareti akaenda kuishi Kapernaumu karibu na ziwa, katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14 Utabiri wa nabii Isaya ukatimia, kama alivyosema: 15 “Nchi ya Zabuloni na nchi ya Naftali, kuelekea baharini, ng’ambo ya Yordani, Galilaya ya watu wa mataifa - 16 watu wale waishio katika giza wameona nuru kuu; na kwa wale wanaoishi katika nchi ya giza la mauti, nuru imewaangazia.” 17 Tangu wakati huo, Yesu alianza kuhubiri akisema: “Tubuni, kwa maana Ufalme wa mbinguni umekaribia.”

Yesu Awaita Wanafunzi Wanne

18 Yesu alipokuwa akitembea kando kando ya ziwa la Galilaya aliwaona ndugu wawili, Simoni ambaye aliitwa Petro na Andrea ndugu yake. Walikuwa katika mashua wakitupa nyavu zao baharini kwa maana wao walikuwa wavuvi.

19 Yesu akawaambia, “Nifuateni, nami nitawafanya muwe wavuvi wa watu.” 20 Wakaziacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.

21 Alipoendelea mbele kidogo, aliwakuta ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana, wakiwa wamekaa kwenye mashua pamoja na baba yao Zebedayo wakishona nyavu zao; akawaita. 22 Wakaacha nyavu zao mara moja, wakamfuata.

Yesu Ahubiri Na Kuponya Wagonjwa

23 Yesu alizunguka Galilaya yote, akifundisha katika masi nagogi na kuhubiri Habari Njema ya Ufalme wa mbinguni, na kupo nya kila ugonjwa na kila udhaifu. 24 Kwa hiyo sifa zake zilienea sehemu zote za Siria. Nao wakamletea wagonjwa wote, waliosumbu liwa na maradhi mbalimbali na maumivu, watu waliopagawa na mashe tani, wenye kifafa na waliopooza, naye akawaponya.

25 Umati mkubwa wa watu ukamfuata kutoka Galilaya, Dekapoli, Yerusalemu, Yudea na kutoka ng’ambo ya mto Yordani.

Yerusalemu, Yudea na kutoka ng’ambo ya mto Yordani.

Yesu alipoona umati wa watu, alipanda mlimani akaketi chini. Wanafunzi wake wakamjia, naye akaanza kuwafundisha akisema:

“Wamebarikiwa walio maskini wa roho; maana Ufalme wa mbin guni ni wao. Wamebarikiwa wanaoomboleza; maana watafarijiwa. Wamebarikiwa walio wapole; maana watairithi nchi. Wamebari kiwa wenye hamu ya kutenda haki; maana wataridhishwa. Wamebari kiwa walio na huruma; maana nao watahurumiwa. Wamebarikiwa walio na moyo safi; maana watamwona Mungu. Wamebarikiwa walio wapatanishi; maana wataitwa wana wa Mungu. 10 Wamebarikiwa wanaoteswa kwa kutenda haki; maana Ufalme wa mbinguni ni wao.

11 Mmebarikiwa ninyi wakati watu watakapowatukana na kuwatesa na kuwasingizia maovu kwa ajili yangu. 12 Shangilieni na kufurahi, kwa maana zawadi yenu huko mbinguni ni kubwa; kwa kuwa ndivyo walivyowatesa manabii waliowatangulia ninyi.

13 “Ninyi ni chumvi ya ulimwengu. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezekani kuwa chumvi tena. Haifai kwa kitu cho chote, ila kutupwa nje ikanyagwe na watu.

14 “Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojengwa kwenye mlima haufichiki. 15 Wala hakuna mtu anayewasha taa kisha akaifunika. Badala yake, huiweka mahali pa juu ili itoe mwanga kwa kila mtu aliyemo ndani ya nyumba. 16 Hali kadhalika, nuru yenu iwaangazie watu ili waone matendo yenu mema wamtukuze Baba yenu aliye mbin guni.’

Mafundisho Kuhusu Sheria

17 “Msidhani kwamba nimekuja kufuta sheria ya Musa na mafundisho ya manabii. kwamba mpaka mbingu na dunia zitaka potoweka, hakuna hata herufi moja ya sheria itakayopotea mpaka shabaha yake ikamilike. 19 Kwa hiyo ye yote atakayelegeza hata mojawapo ya amri ndogo kuliko amri zote na akawafundisha wengine kufanya hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika Ufalme wa mbinguni. Sikuja kuzifuta bali kuzitimiza. 18 Kwa maana ninawaambia hakika Lakini atakayetii amri hizi na kuwafundisha wengine kuzitii a taitwa mkuu katika Ufalme wa mbinguni. 20 Kwa maana nawaambieni, ikiwa haki yenu haitazidi haki ya waandishi wa sheria na Mafari sayo, hamtaingia katika Ufalme wa mbinguni kamwe.”

Mafundisho Kuhusu Hasira

21 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usiue; na ye yote atakayeua atastahili hukumu.’ 22 Lakini mimi nawaambia kwamba, ye yote atakayemkasirikia ndugu yake atasta hili hukumu; na ye yote atakayemtukana ndugu yake, atashtakiwa katika baraza; na ye yote atakayemwambia ndugu yake, ‘Wewe mjinga,’ atastahili hukumu ya moto wa Jehena.

23 “Basi, kama ulikuwa tayari kutoa sadaka yako madhaba huni, ukakumbuka kuwa ndugu yako amekukasirikia, 24 acha sadaka yako hapo hapo, uende kwanza ukapatane naye, kisha urudi kumtolea Mungu sadaka yako. 25 “Mtu akikushtaki, patana naye kabla hamjafika mahaka mani; ili mshtaki wako asije akakukabidhi kwa hakimu, na hakimu akamwamuru askari akufunge gerezani; 26 nami nawaambia hakika, hutatoka huko mpaka deni lako lote litakapolipwa.”

Mafundisho Kuhusu Uzinzi

27 “Mmesikia walivyowafundisha watu wa zamani kwamba, ‘Usi zini’. 28 Lakini mimi nawaambia: ye yote atakayemwangalia mwa namke kwa kumtamani, amekwisha kuzini naye moyoni mwake. 29 Jicho lako la kulia likikufanya utende dhambi, ling’oe ulitu pilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena. 30 Na kama mkono wako wa kuume ukiku fanya utende dhambi, ukate uutupilie mbali. Ni afadhali upoteze sehemu ya mwili wako kuliko mwili mzima utupwe Jehena.

31 “Pia mliambiwa kwamba, ‘Mtu ye yote anayemwacha mkewe ampe talaka.’ 32 Lakini mimi nawaambia, ye yote atakayempa mkewe talaka isipokuwa kwa kosa la uasherati, anamfanya mkewe mzinzi. Na ye yote atakayemwoa mwanamke aliyepewa talaka anazini.”

Mafundisho Kuhusu Kuapa

33 “Tena mmesikia watu wa kale waliambiwa kwamba, ‘Usi vunje kiapo chako bali umtimizie Mungu kama ulivyoapa kutenda.’ 34 Lakini mimi nawaambia, msiape kabisa, ama kwa mbingu, kwa sababu ni kiti cha enzi cha Mungu, 35 au kwa ardhi, kwa sababu ndipo mahali pake pa kuwekea miguu, au kwa Yerusalemu kwa sababu ndio mji wa Mfalme mkuu. 36 Na msiape kwa vichwa vyenu kwa sababu hamwezi kugeuza hata unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi. 37 Ukisema ‘Ndio’ basi iwe ‘Ndio’; na ukisema ‘Hapana’ basi iwe ‘ Hapana.’ Lo lote zaidi ya haya hutoka kwa yule mwovu.”

Mafundisho Kuhusu Kulipiza Kisasi

38 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’ 39 Lakini mimi nawaambia, msishindane na mtu mwovu. Lakini mtu akikupiga kwenye shavu la kulia, mgeuzie na shavu la kushoto pia; 40 na kama mtu akitaka kukushtaki achukue shati lako, mwachie achukue na koti pia. 41 Na kama mtu akikulazimisha uende kilometa moja naye, fanya zaidi, nenda naye kilometa mbili. 42 Mtu akikuomba kitu mpe, na usikatae kumsaidia mtu anayetaka kukukopa.”

Wapendeni Maadui Zenu

43 “Mmesikia kuwa watu zamani walikuwa wakisema, ‘Umpende jirani yako na umchukie adui yako.’ 44 Lakini mimi ninawaambia, wapendeni maadui zenu na waombeeni wanaowatesa, 45 ili mpate kuwa watoto wa Baba yenu aliye mbinguni. Kwa maana yeye huwaanga zia jua lake watu waovu na watu wema; na pia huleta mvua kwa wenye haki na wasio haki. 46 Kama mkiwapenda wanaowapenda tu, mtapata thawabu gani? Hata wenye dhambi hufanyiana hivyo. 47 Na kama mkiwasalimu ndugu zenu tu, mnafanya nini zaidi ya wengine? Hata watu wa mataifa wasiomjua Mungu, hufanya hivyo. 48 Kwa hiyo inawapasa ninyi muwe wakamilifu kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.”

Kuwasaidia Maskini

“Angalieni msitende mema mbele ya watu ili muonekane na watu. Kwa maana mkifanya hivyo hamtapata thawabu itokayo kwa Baba yenu aliye mbinguni. “Kwa hiyo mnapowasaidia maskini msitangaze kwa tarumbeta kama wafanyavyo wanafiki katika masinagogi na mitaani ili wasi fiwe na watu. Nawaambia wazi, wao wamekwisha pata tuzo yao. Lakini ninyi mnapotoa sadaka, fanyeni kwa siri, hata mkono wako wa kushoto usijue mkono wako wa kulia unafanya nini; ili sadaka yako iwe ni siri. Naye Baba yako wa mbinguni anayeona sirini ata kupa thawabu.”

Mafundisho Kuhusu Sala

“Na mnaposali, msiwe kama wanafiki; maana wao wanapenda kusimama na kusali katika masinagogi na kando ya barabara ili waonekane na watu. Nawaambieni kweli, wao wamekwisha kupata tuzo yao. Unaposali, nenda chumbani kwako ufunge mlango na umwombe Baba yako aliye sirini. Na Baba yako aonaye sirini atakupa tha wabu.

“Mnaposali msirudie maneno yale yale kama wafanyavyo watu wa mataifa wasiomjua Mungu. Kwa maana wao hudhani kwamba watasi kilizwa kwa sababu ya wingi wa maneno yao. Msiwe kama wao, kwa sababu Baba yenu anajua mahitaji yenu hata kabla hamjaomba.” Basi msalipo ombeni hivi: ‘Baba yetu uliye mbinguni jina lako litukuzwe. 10 Ufalme wako uje, mapenzi yako yafanyike hapa duniani kama huko mbinguni. 11 Utupatie leo riziki yetu ya kila siku. 12 Na utusamehe makosa yetu kama sisi tulivyokwisha kuwa samehe waliotukosea. 13 Na usitutie majaribuni, bali utuokoe kutokana na yule mwovu,’ [Kwa kuwa Ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele. Amina.] 14 Kama mkiwasamehe watu makosa yao, Baba yenu wa mbinguni atawasamehe na ninyi; 15 lakini msipowasamehe watu makosa yao, Baba yenu hatawasamehe makosa yenu.

Mafundisho Kuhusu Kufunga

16 “Mnapofunga, msionyeshe huzuni kama wafanyavyo wanafiki. Maana wao hukunja nyuso zao ili kujionyesha. Nawaambieni kweli kwamba wao wamekwisha kupata tuzo yao. 17 Lakini mnapofunga, jipakeni mafuta kichwani na kuosha nyuso zenu 18 ili kufunga kwenu kusijulikane kwa mtu ila Baba yenu aliye sirini; na Baba yenu aonaye katika siri atawapa thawabu.” Akiba Ya Mbinguni. 19 “Msijiwekee mali nyingi duniani ambapo wadudu na kutu huharibu na wezi huvunja na kuiba. 20 Lakini jiwekeeni mali mbinguni ambapo wadudu na kutu hawaharibu na wezi hawavunji na kuiba. 21 Kwa sababu pale akiba yako ilipo ndipo moyo wako uta kapokuwa.”

Jicho Ni Taa Ya Mwili

22 “Jicho ni taa ya mwili. Kama jicho lako ni zuri, mwili wako wote utakuwa na nuru. 23 Lakini kama jicho lako ni bovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Kwa hiyo kama nuru iliyomo ndani yako ni giza, hakika utakuwa na giza la kutisha.”

Mungu Na Mali

24 “Hakuna mtu anayeweza kuwatumikia mabwana wawili, kwa sababu, ama atamchukia mmoja na kumpenda mwingine, au atamthami ni mmoja na kumdharau mwingine. Huwezi kumtumikia Mungu na mali.”

Msiwe Na Wasiwasi

25 “Kwa hiyo nawaambia, msiwe na wasiwasi kuhusu maisha yenu: mtakula nini au mtakunywa nini; au kuhusu miili yenu: mvae nini. Kwani maisha si zaidi ya chakula? Na mwili zaidi ya mavazi? 26 Waangalieni ndege wa angani: wao hawapandi wala kuvuna wala kuweka cho chote ghalani. Lakini Baba yenu wa mbinguni anawali sha. Je ninyi, si wa thamani zaidi kuliko ndege? 27 Ni nani kati yenu ambaye kwa kujihangaisha kwake anaweza kujiongezea hata saa moja zaidi kwenye maisha yake?

28 “Na kwa nini mnahangaikia mavazi? Angalieni maua ya mwi tuni yanavyostawi. Hayafanyi kazi wala hayashoni nguo. 29 Lakini nawaambia, hata mfalme Sulemani katika ufahari wake wote hakuwahi kuvikwa kama mojawapo la maua hayo. 30 Lakini ikiwa Mungu anay avisha hivi maua ambayo leo yapo na kesho yanatupwa motoni, je, hatawavisha ninyi vizuri zaidi, enyi watu wenye imani haba? 31 Kwa hiyo msiwe na wasiwasi mkisema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Mambo haya ndio yanay owahangaisha watu wa mataifa wasiomjua Mungu; na Baba yenu wa mbinguni anafahamu kwamba mnahitaji yote hayo. 33 Lakini uta futeni kwanza Ufalme wa mbinguni na haki yake, na haya yote mtaongezewa. 34 Kwa hiyo msihangaike kuhusu kesho, kwa sababu kesho itajihangaikia yenyewe. Kila siku ina shida zake za kutosha.”

Usihukumu Wengine

Usihukumu ili na wewe usihukumiwe. Kwa maana hukumu uta kayotamka juu ya wenzako ndio itakayotumiwa kukuhukumu, na kipimo utakachotoa ndicho utakachopokea. Kwa nini unaangalia kijiti kidogo kilichomo katika jicho la ndugu yako na wala huoni pande la mti lililoko jichoni mwako? Au unawezaje kumwambia ndugu yako, ‘Hebu nikutoe uchafu jichoni mwako,’ wakati jichoni mwako mna pande kubwa? Mnafiki wewe! Toa kwanza pande lililoko jichoni mwako, ndipo utaweza kuona vema, upate kukitoa kipande kilichoko ndani ya jicho la ndugu yako.

“Msiwape mbwa vitu vitakatifu; na msitupe lulu zenu mbele ya nguruwe wasije wakazikanyaga kanyaga na halafu wawageukie na kuwashambulia.”

Omba, Tafuta, Bisha Hodi

“Ombeni nanyi mtapewa. Tafuteni nanyi mtapata; bisheni hodi nanyi mtafunguliwa mlango. Kwa sababu kila aombaye hupewa; naye atafutaye hupata; na abishaye hodi atafunguliwa mlango.

“Au ni nani kati yenu ambaye kama mwanae akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki atampa nyoka? 11 Ikiwa ninyi mlio waovu mnafahamu jinsi ya kuwapa watoto wenu zawadi nzuri, ni mara ngapi zaidi Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vizuri wale wamwombao? 12 Kwa hiyo cho chote ambacho ungependa watu wakutendee, na wewe watendee vivyo hivyo. Hii ndio maana ya sheria ya Musa na Maandiko ya manabii.”

Njia Nyembamba Na Njia Pana

13 “Ingieni kwa kupitia mlango mwembamba; kwa maana mlango mpana na njia rahisi huelekea kwenye maangamizo, na watu wanaopitia huko ni wengi. 14 Lakini mlango mwembamba na njia ngumu huelekea kwenye uzima, na ni wachache tu wanaoiona.”

Manabii Wa Uongo

15 “Jihadharini na manabii wa uongo wanaowajia wakiwa wamevaa ngozi ya kondoo, kumbe ndani ni mbwa mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je, unaweza kuchuma zabibu kwenye miiba au tini kwenye michongoma? 17 Vivyo hivyo mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya na mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa katwa na kutupwa motoni. 20 Hivyo, mtawatambua kwa matunda yao.”

Mfuasi Wa Kweli

21 “Si kila mtu anayesema, ‘Bwana, Bwana,’ ambaye ataingia katika Ufalme wa mbinguni ila ni wale wanaofanya mapenzi ya Baba yangu aliye mbinguni. 22 Siku ile itakapofika wengi wata niambia, ‘Bwana, Bwana, hatukutoa unabii na kufukuza pepo kwa jina lako; na kufanya miujiza mingi ya ajabu kwa jina lako?’ 23 Ndipo nitawaambia wazi, ‘Sikuwafahamu kamwe. Ondokeni kwangu ninyi watenda maovu!’

Nyumba Iliyojengwa Kwenye Mwamba

24 “Basi, kila anayesikiliza haya maneno yangu na kuyate keleza, atafanana na mtu mwenye busara aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua ikanyesha, mafuriko yakaja na upepo uka vuma ukaipiga nyumba hiyo, lakini haikuanguka kwa sababu ili jengwa kwenye msingi imara juu ya mwamba. 26 Na kila anayesikia haya maneno yangu asiyafuate, atafanana na mtu mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua ikanyesha, yakatokea mafu riko, na upepo ukavuma ukaipiga hiyo nyumba, nayo ikaanguka kwa kishindo kikubwa.” 28 Na Yesu alipomaliza kusema maneno haya, umati wa watu waliomsikiliza walishangaa sana, 29 kwa sababu alifundisha kama mtu mwenye mamlaka, na si kama walimu wao wa sheria.

Yesu Amponya Mwenye Ukoma

Alipotoka mlimani, umati mkubwa wa watu walimfuata. Na mtu mmoja mwenye ukoma akaja akapiga magoti mbele yake akasema, “Bwana, kama ukipenda, unaweza kunitakasa.” Yesu akanyoosha mkono wake akamgusa, akamwambia, “Napenda. Takasika.” Wakati huo huo yule mtu akapona ukoma wake. Na Yesu akamwambia, “Usiseme cho chote kwa mtu ye yote, lakini nenda ukajionyeshe kwa kuhani na utoe sadaka aliyoamuru Musa, iwe uthibitisho kwa watu kwamba umepona.”

Yesu Amponya Mtumishi Wa Askari

Yesu alipoingia Kapernaumu, askari mmoja alikuja kumwomba msaada, akisema, “Bwana, mtumishi wangu amelala nyumbani ame pooza, tena ana maumivu makali.” Yesu akamwambia, “Nitakuja kumponya.” Lakini yule askari akamwambia, “Bwana, mimi sis tahili wewe uingie nyumbani kwangu; lakini sema neno tu, na mtumi shi wangu atapona. Mimi niko chini ya mamlaka, na ninao askari chini yangu. Nikimwambia askari mmoja ‘Nenda 10 Yesu aliposikia maneno haya, alishangaa, akawaambia wale waliomfuata, “Nawaambia kweli, hata katika Israeli sijaona imani ya namna hii. 11 Ninawahakikishia kwamba wengi watatoka mashar iki na magharibi nao wataketi mezani pamoja na Ibrahimu, Isaka na Yakobo katika Ufalme wa mbinguni. 12 Lakini wana wa ufalme watatupwa nje gizani, huko watu watalia na kusaga meno.” 13 Yesu akamwambia yule askari, “Nenda nyumbani, na yale uliy oamini yatimie kwako.” Na yule mtumishi akapona tangu wakati ule ule.

Yesu Aponya Wengi

14 Yesu alipoingia nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wake amelala akiwa ana homa. 15 Akamgusa mkono na homa ikam toka, akaamka akaanza kumhudumia. 16 Jioni ile walimletea watu wengi waliopagawa na pepo; naye akawafukuza pepo kwa neno lake, na akawaponya wagonjwa wote. 17 Miujiza hii ilitimiza yale yali yosemwa na nabii Isaya kwamba: “Alichukua udhaifu wetu, na kubeba magonjwa yetu.”

18 Yesu alipoona umati wa watu unazidi kuongezeka aliwaamuru wanafunzi wake wavuke, waende ng’ambo ya pili. 19 Na mwalimu mmoja wa sheria akamjia Yesu akamwambia, “Mwalimu, mimi nitaku fuata po pote utakapokwenda.” 20 Lakini Yesu akamjibu, “Mbweha wana mashimo yao, na ndege wa angani wana viota vyao, lakini mimi Mwana wa Adamu sina mahali pa kulaza kichwa changu.” 21 Mwana funzi mwingine akamwambia, “Bwana, niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.” 22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate, waache wal iokufa wawazike wafu wao.”

Yesu Atuliza Dhoruba

23 Alipoingia kwenye mashua wanafunzi wake walimfuata. 24 Mara dhoruba kali ikavuma na mawimbi yakakaribia kuzamisha ile mashua; lakini Yesu alikuwa amelala usingizi. 25 Wanafunzi wake wakaenda kumwamsha wakisema, “Bwana, tuokoe! Tunaangamia!”

26 Lakini Yesu akawajibu, “Enyi wenye imani haba, mbona mnaogopa?” Akasimama, akaikemea dhoruba na mawimbi; navyo vikat ulia, pakawa shwari kabisa. 27 Wanafunzi wake wakashangaa. Wakaulizana, “Ni mtu wa namna gani huyu, ambaye hata upepo na bahari vinamtii?”

28 Walipofika ng’ambo ya Genezareti, watuwawili wenye pepo walikutana naye. Watu hawa waliishi makaburini na walikuwa wanat isha, kiasi kwamba hakuna mtu aliyethubutu kupita njia ile. 29 Wakapiga kelele, “Unataka nini kwetu, wewe Mwana wa Mungu? Umekuja hapa kututesa kabla ya wakati kutimia?” 30 Mbali kidogo kulikuwa na kundi kubwa la nguruwe wakilisha. 31 Wale pepo wakamsihi Yesu, “Ukitufukuza, tafadhali turuhusu twende kwenye lile kundi la nguruwe.” 32 Akawaambia, “Nendeni”. Basi waka toka wakawaingia wale nguruwe; na kundi lote likatimka mbio kuelekea ukingoni mwa bahari, wakaangamia katika maji. 33 Wachungaji wa hao nguruwe wakakimbilia mjini wakaeleza kila kitu, na yaliyowatokea wale waliokuwa wamepagawa na pepo. 34 Watu wote wa mji huo wakatoka kwenda kukutana na Yesu. Wali pomwona wakamsihi aondoke kwenye nchi yao.

Yesu Amponya Mtu Aliyepooza

Yesu akaingia katika mashua akavuka ziwa, akafika katika mji wa kwao. Watu wakamletea mtu aliyepooza, akiwa amelazwa kwenye kitanda chake. Yesu alipoona imani yao, akamwambia yule mtu ali yepooza, “Mwanangu, jipe moyo; dhambi zako zimesamehewa.” Baadhi ya walimu wa sheria wakawaza moyoni mwao, “Huyu mtu anakufuru!” Lakini Yesu alifahamu mawazo yao. Akawaambia, “Kwa nini mnawaza maovu mioyoni mwenu? Kwani ni lipi lililo rahisi: kusema ‘Dhambi zako zimesamehewa Lakini, nitawathibitishia kwamba Mwana wa Adamu anayo mamlaka duniani kusamehe dhambi.” Akamwambia yule aliyepo oza, “Simama, chukua kitanda chako uende nyumbani.” Yule mtu akasimama, akaenda nyumbani. Watu walipoyaona haya, wakaogopa, wakamtukuza Mungu ambaye alitoa uwezo wa jinsi hii kwa wanadamu.

Yesu Amwita Mathayo

Yesu alipoondoka hapo, alimwona mtu mmoja jina lake Mathayo akiwa ameketi katika ofisi ya kukusanyia kodi. Akamwambia, “Nifuate”. Mathayo akainuka, akamfuata. 10 Wakati Yesu alipo kuwa ameketi mezani kula chakula katika nyumba fulani, watoza kodi wengi na wenye dhambi walikuja kula pamoja naye na wanafunzi wake. 11 Mafarisayo walipoona mambo haya wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula na watoza kodi na wenye dhambi?” 12 Lakini Yesu alipowasikia aliwaambia, “ Watu wenye afya hawahitaji daktari, lakini wagonjwa wanamhitaji. 13 Nendeni mkajifunze maana ya maneno haya, ‘Napenda huruma na wala sio sadaka za kuteketeza.’ Kwa maana sikuja kuwaita wenye haki, bali wenye dhambi.”

Yesu Aulizwa Kuhusu Kufunga

14 Wanafunzi wa Yohana Mbatizaji walikuja kwa Yesu wakamwuli za, “Mbona sisi na Mafarisayo tunafunga lakini wanafunzi wako hawafungi?”

Ukoo wa Yesu

(Lk 3:23-38)

Hii ni historia ya ukoo wa Yesu, Masihi.[a] Alitoka katika ukoo wa Daudi, aliyetoka katika ukoo wa Ibrahimu.

Ibrahimu alikuwa baba yake Isaka.

Isaka alikuwa baba yake Yakobo.

Yakobo alikuwa baba wa Yuda na ndugu zake.

Yuda alikuwa baba wa Peresi na Zera. (Mama yao alikuwa Tamari.)

Peresi alikuwa baba yake Hezroni.

Hezroni alikuwa baba yake Ramu.

Ramu alikuwa baba yake Aminadabu.

Aminadabu alikuwa baba yake Nashoni.

Nashoni alikuwa baba yake Salmoni.

Salmoni alikuwa baba yake Boazi. (Mama yake Boazi alikuwa Rahabu.)

Boazi alikuwa baba yake Obedi. (Mama yake Obedi alikuwa Ruthu.)

Obedi alikuwa baba yake Yese.

Yese alikuwa baba yake Mfalme Daudi.

Daudi alikuwa baba yake Sulemani. (Mama yake Sulemani alikuwa mke wa Uria.)

Sulemani alikuwa baba yake Rehoboamu.

Rehoboamu alikuwa baba yake Abiya.

Abiya alikuwa baba yake Asa.

Asa alikuwa baba yake Yehoshafati.

Yehoshafati alikuwa baba yake Yoramu.

Yoramu alikuwa baba yake Uzia.

Uzia alikuwa baba yake Yothamu.

Yothamu alikuwa baba yake Ahazi.

Ahazi alikuwa baba yake Hezekia.

10 Hezekia alikuwa baba yake Manase.

Manase alikuwa baba yake Amoni.

Amoni alikuwa baba yake Yosia.

11 Yosia alikuwa baba wa Yekonia[b] na ndugu zake.

Walioishi wakati ambao watu walipelekwa utumwani Babeli.

12 Baada ya uhamisho wa Babeli,

Yekonia akawa baba yake Shealtieli.

Shealtieli alikuwa babu wa Zerubabeli.

13 Zerubabeli alikuwa baba yake Abiudi.

Abiudi alikuwa baba yake Eliakimu.

Eliakimu alikuwa baba yake Azori.

14 Azori alikuwa baba yake Sadoki.

Sadoki alikuwa baba yake Akimu.

Akimu alikuwa baba yake Eliudi.

15 Eliudi alikuwa baba yake Eliazari.

Eliazari alikuwa baba yake Matani.

Matani alikuwa baba yake Yakobo.

16 Yakobo alikuwa baba yake Yusufu,

Yusufu alikuwa mume wa Mariamu.

Na Mariamu alimzaa Yesu, anayeitwa Masihi.

17 Kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Ibrahimu mpaka kwa Daudi. Na kulikuwa na vizazi kumi na nne kuanzia kwa Daudi mpaka wakati wa uhamisho wa Babeli. Na palikuwa na vizazi kumi na nne tangu uhamisho wa Babeli mpaka wakati alipozaliwa Yesu, Masihi.

Kuzaliwa kwa Yesu, Masihi

(Lk 2:1-7)

18 Kuzaliwa kwa Yesu Masihi, kulikuwa hivi: Mariamu mama yake alikuwa amechumbiwa na Yusufu. Kabla hawajaoana, Yusufu aligundua kuwa Mariamu alikuwa mja mzito. (Yeye alipata mimba kwa uweza wa Roho Mtakatifu.) 19 Kwa kuwa Yusufu alitaka kufanya kile kilichokuwa, alikusudia kumwacha Mariamu kwa siri bila ya kumvunjia heshima.

20 Lakini baada ya Yusufu kuliwazia jambo hili, Malaika wa Bwana alimjia katika ndoto na akamwambia, “Yusufu mwana wa Daudi, usiogope kumchukua Mariamu awe mke wako. Mimba aliyonayo ameipata kwa uweza wa Roho Mtakatifu. 21 Atamzaa mwana, nawe utamwita Yesu.[c] Utampa jina hilo Yesu kwa sababu yeye atawaokoa watu wake kutoka dhambi zao.”

22 Haya yote yalitokea ili kutimiza maneno ambayo Bwana aliyasema kupitia kwa nabii aliposema:

23 “Sikiliza! Msichana bikira atapata mimba
    na atazaa mtoto wa kiume.
    Mtoto huyo ataitwa Emanueli.”(A)

(Yaani “Mungu yu pamoja nasi”.)

24 Yusufu alipoamka alifanya kama alivyoelekezwa na Malaika wa Bwana. Alimuoa Mariamu. 25 Lakini hakukutana naye kimwili mpaka Mariamu alipomzaa mwana. Na Yusufu akamwita Yesu.

Wenye Hekima Waja Kumwona Yesu

Yesu alizaliwa katika mji wa Bethlehemu ya Uyahudi wakati Herode alipokuwa mfalme. Baada ya Yesu kuzaliwa, baadhi ya wenye hekima kutoka mashariki walikuja Yerusalemu. Walipofika wakawauliza watu, “Yuko wapi mtoto aliyezaliwa ili awe Mfalme wa Wayahudi? Tuliiona nyota ilipochomoza na kutuonesha kuwa amezaliwa. Nasi tumekuja ili tumwabudu.”

Mfalme Herode aliposikia haya, yeye pamoja na watu wote wakaao Yerusalemu walikasirika sana. Herode aliitisha mkutano wa wakuu wote wa makuhani wa Kiyahudi na walimu wa sheria. Akawauliza ni wapi ambapo Masihi angezaliwa. Wakamjibu, “Ni katika mji wa Bethlehemu ya Yuda kama ambavyo nabii aliandika:

‘Bethlehemu, katika nchi ya Yuda,
    wewe ni wa muhimu miongoni mwa watawala wa Yuda.
Ndiyo, mtawala atakayewaongoza
    watu wangu Israeli, atatoka kwako.’”(B)

Kisha Herode akawaita na kufanya mkutano wa siri na wenye hekima kutoka mashariki. Akaelewa kwa usahihi wakati walipoiona nyota. Kisha akawaruhusu waende Bethlehemu. Akawaambia, “Nendeni mkamtafute mtoto kwa makini na mtakapompata mrudi na kunipa taarifa mahali alipo, ili nami pia niende kumwabudu.”

Wenye hekima walipomsikiliza mfalme, waliondoka. Waliiona tena ile nyota waliyoiona hapo mwanzo na wakaifuata. Nyota ile iliwaongoza mpaka mahali alipokuwa mtoto na kusimama juu ya sehemu hiyo. 10 Wenye hekima walipoona kuwa nyota ile imesimama, walifurahi na kushangilia kwa furaha.

11 Wenye hekima hao kisha waliingia katika nyumba alimokuwamo mtoto Yesu pamoja na Mariamu mama yake. Walisujudu na kumwabudu mtoto. Kisha wakafungua masanduku yenye zawadi walizomletea mtoto. Wakampa hazina za dhahabu, uvumba na manemane. 12 Lakini Mungu aliwaonya wenye hekima hao katika ndoto kuwa wasirudi tena kwa Herode. Hivyo kwa kutii walirudi nchini kwao kwa kupitia njia nyingine.

Yesu Apelekwa Uhamishoni Misri

13 Baada ya wenye hekima kuondoka, malaika wa Bwana akamjia Yusufu katika ndoto na kumwambia, “Damka! Mchukue mtoto pamoja na mama yake ukimbilie Misri kwa sababu Herode amedhamiria kumwua mtoto na sasa atatuma watu kumtafuta. Na mkae Misri mpaka nitakapowaambia mrudi.”

14 Hivyo Yusufu alidamka na kutoka kwenda Misri akiwa na mtoto na mama yake. Nao waliondoka usiku. 15 Yusufu na familia yake walikaa huko Misri mpaka Herode alipofariki. Hili lilitukia ili maneno yaliyosemwa na nabii yatimie: “Nilimwita mwanangu atoke Misri.”(C)

Herode Aua Watoto wa Kiume Katika Mji wa Bethlehemu

16 Herode alipoona kuwa wenye hekima wamemfanya aonekane mjinga, alikasirika sana. Hivyo akatoa amri ya kuua watoto wote wa kiume wenye umri wa miaka miwili au chini ya miaka hiyo katika mji wa Bethlehemu na vitongoji vyake. Herode alifahamu kutoka kwa wenye hekima kwamba walikuwa wameiona nyota miaka miwili kabla. 17 Hili likatimiza yale yaliyosemwa na Mungu kupitia nabii Yeremia aliposema:

18 “Sauti imesikika Rama,
    sauti ya kilio na huzuni kuu.
Raheli akiwalilia watoto wake,
    na amekataa kufarijiwa
    kwa sababu watoto wake hawapo tena.”(D)

Yusufu na Familia Yake Warudi Kutoka Misri

19 Wakati Yusufu na familia yake wakiwa Misri, Herode alifariki. Malaika wa Bwana akamjia Yusufu katika ndoto 20 na akamwambia, “Damka! Mchukue mtoto na mama yake urudi Israeli, kwani waliojaribu kumwua mtoto wamekwisha kufa.”

21 Hivyo Yusufu alidamka na kumchukua mtoto Yesu na mama yake na kurudi Israeli. 22 Lakini Yusufu aliposikia kuwa Arkelao alikuwa mfalme wa Yuda baada ya baba yake kufa, aliogopa kwenda huko. Lakini baada ya kuonywa na Mungu katika ndoto, Yusufu aliondoka pamoja na familia yake akaenda sehemu za Galilaya. 23 Alikwenda katika mji wa Nazareti na kukaa huko. Hii ilitokea ili kutimiza maneno yale yaliyosemwa na manabii. Mungu alisema Masihi angeitwa Mnazareti.[d]

Yohana Atayarisha Njia kwa Ajili ya Yesu

(Mk 1:1-8; Lk 3:1-9,15-17; Yh 1:19-28)

Baadaye, kabla ya miaka mingi kupita, Yohana Mbatizaji alianza kuwahubiri watu ujumbe uliotoka kwa Mungu. Naye alihubiri kutokea maeneo ya nyikani huko Uyahudi. Yohana alisema, “Tubuni na kuibadili mioyo yenu, kwa sababu ufalme wa Mungu umekaribia.” Nabii Isaya alisema kuhusu habari za Yohana Mbatizaji pale aliposema,

“Kuna mtu anayeipaza sauti yake toka nyikani:
‘Tayarisheni njia kwa ajili ya Bwana;
    nyoosheni njia kwa ajili yake.’”(E)

Huyo Yohana alivaa mavazi yaliyofumwa kutokana na manyoya ya ngamia. Naye alijifunga mkanda wa ngozi kuzunguka kiuno chake, na alikula nzige na asali mbichi. Watu kutoka Yerusalemu na maeneo yote ya Uyahudi na wale kutoka maeneo yote yaliyo kando ya Mto Yordani walikwenda kwa Yohana Mbatizaji; huko waliungama matendo yao mabaya kwake naye akawabatiza katika Mto Yordani.

Mafarisayo na Masadukayo wengi walikwenda kwa Yohana ili wabatizwe. Yohana alipowaona, akasema, “Enyi ninyi nyoka! Ni nani amewaonya kuikimbia hukumu ya Mungu inayokuja? Muibadili mioyo yenu! Na muoneshe kwa vitendo kuwa mmebadilika. Ninajua mnachofikiri. Mnataka akasema kuwa, ‘lakini Ibrahimu ni baba yetu!’ Hiyo haijalishi. Ninawaambia Mungu anaweza kumzalia Ibrahimu watoto kutoka katika mawe haya. 10 Shoka limewekwa tayari kukata shina la mti katika mizizi yake. Kila mti[e] usiozaa matunda mazuri utakatwa vivyo hivyo na kutupwa motoni.

11 Mimi ninawabatiza kwa maji kuonesha kuwa mmebadilika mioyoni mwenu na pia maishani mwenu. Lakini yupo mwingine ajaye baada yangu, mwenye nguvu zaidi kuliko mimi, huyo atafanya mengi zaidi yangu. Nami niliye mtumwa wa chini kabisa sistahili hata kuinama na kufungua kamba za viatu vyake. Yeye huyo atawabatiza kwa Roho Mtakatifu na kwa moto. 12 Naye atakuja akiwa tayari kwa ajili ya kuisafisha nafaka. Atatenganisha nafaka nzuri kutoka kwenye makapi,[f] na kisha ataiweka nafaka nzuri kwenye ghala yake. Kisha atayachoma makapi kwa moto usiozimika.”

Yohana Ambatiza Yesu

(Mk 1:9-11; Lk 3:21-22)

13 Ndipo Yesu alitoka Galilaya na kwenda Mto Yordani. Alikwenda kwa Yohana, akitaka kubatizwa. 14 Lakini Yohana alijaribu kumzuia. Yohana akamwambia Yesu, “Kwa nini unakuja kwangu ili nikubatize? Mimi ndiye ninayepaswa kubatizwa na wewe!”

15 Yesu akajibu, “Acha iwe hivyo kwa sasa. Tunapaswa kuyatimiza mapenzi ya Mungu.” Ndipo Yohana akakubali.

16 Hivyo Yesu akabatizwa. Mara tu aliposimama kutoka ndani ya maji, mbingu zilifunguka na akamwona Roho Mtakatifu akishuka kutoka mbinguni kama hua[g] na kutua juu yake. 17 Sauti kutoka mbinguni ikasema, “Huyu ni Mwanangu, nimpendaye. Ninapendezwa naye.”

Yesu Ajaribiwa na Shetani

(Mk 1:12-13; Lk 4:1-13)

Kisha Roho Mtakatifu akamwongoza Yesu hadi nyikani ili akajaribiwe na Shetani. Baada ya Yesu kufunga kwa siku arobaini mchana na usiku, akaumwa njaa sana. Mjaribu[h] akamwendea na akasema, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, basi yaamuru mawe haya yawe mikate.”

Yesu akajibu, “Maandiko yanasema, ‘Mtu hataishi kwa mkate tu, ila kwa kila Neno linalotoka katika kinywa cha Mungu.’”(F)

Kisha Shetani alimwongoza Yesu mpaka mji mtakatifu wa Yerusalemu na akamweka juu ya mnara wa Hekalu. Akamwambia Yesu, “Ikiwa wewe ni Mwana wa Mungu, jirushe mpaka chini! Kwani Maandiko yanasema,

‘Mungu atawaamuru malaika zake wakusaidie,
na mikono yao itakupokea,
    ili usije ukajikwaa mguu wako kwenye jiwe.’”(G)

Yesu akamjibu, “Pia, Maandiko yanasema, ‘usimjaribu Bwana Mungu wako.’”(H)

Kisha Shetani akamwongoza Yesu mpaka kwenye kilele cha mlima ulio mrefu sana na kumwonyesha falme zote za ulimwengu na vitu vya kupendeza vilivyomo ndani. Shetani akamwambia Yesu, “Ukiinama na kuniabudu, nitakupa vitu hivi vyote.”

10 Yesu akamjibu Shetani akamwambia, “Ondoka kwangu Shetani! Kwani Maandiko yanasema, ‘Umwabudu Bwana Mungu wako na umtumikie yeye peke yake!’”(I)

11 Baada ya hayo, Shetani akamwacha. Ndipo malaika wakaja kumhudumia.

Yesu Aanza Kazi yake Galilaya

(Mk 1:14-15; Lk 4:14-15)

12 Yesu aliposikia kuwa Yohana alikuwa amefungwa gerezani, alirudi katika wilaya ya Galilaya. 13 Lakini aliondoka Nazareti. Alikwenda kuishi Kapernaumu, mji ulio kando kando ya Ziwa Galilaya katika eneo la Zabuloni na Naftali. 14 Hili lilitokea ili kutimiza maneno aliyosema nabii Isaya:

15 “Sikilizeni, enyi nchi ya Zabuloni na Naftali,
    nchi iliyo kando ya barabara iendayo baharini,
    ng'ambo ya Mto Yordani!
    Galilaya, wanapokaa Mataifa.
16 Watu wanaoishi katika giza ya kiroho,
    nao wameiona nuru iliyo kuu.
Nuru hiyo imeangaza kwa ajili yao wale
    wanaoishi katika nchi yenye giza kama kaburi.”(J)

17 Tangu wakati huo Yesu alianza kuwaambia watu ujumbe wake unaosema, “Mbadili mioyo yenu na maisha yenu pia, kwa sababu Ufalme wa Mungu umewafikia.”

Yesu Achagua Baadhi ya Wafuasi

(Mk 1:16-20; Lk 5:1-11)

18 Yesu alipokuwa akitembea kando ya Ziwa Galilaya, aliwaona ndugu wawili, Simoni, aitwaye Petro na nduguye aitwaye Andrea. Ndugu hawa walikuwa wavuvi na walikuwa wanavua samaki kwa nyavu zao. 19 Yesu akawaambia, “Njooni, mnifuate, nami nitawafanya kuwa wavuvi wa aina nyingine. Nitawafundisha jinsi ya kukusanya watu badala ya samaki.” 20 Mara moja, Simoni na Andrea wakaziacha nyavu zao na kumfuata Yesu papo hapo.

21 Yesu akaendelea kutembea kutoka pale. Akawaona ndugu wengine wawili, Yakobo na Yohana wana wa Zebedayo. Walikuwa kwenye mashua pamoja na Zebedayo baba yao. Walikuwa wakiandaa nyavu zao za kuvulia samaki. Yesu akawaita wamfuate. 22 Mara moja wakaiacha mashua pamoja na baba yao na wakamfuata Yesu.

Yesu Afundisha na Kuponya Watu

(Lk 6:17-19)

23 Yesu alikwenda sehemu zote za Galilaya, akifundisha na akihubiri Habari Njema katika masinagogi kuhusu Ufalme wa Mungu. Aliponya magonjwa yote na madhaifu mengi ya watu. 24 Habari kuhusu Yesu zilienea katika nchi yote ya Shamu, na watu waliwaleta wale wote wenye kuteswa na magonjwa na maumivu mbalimbali. Baadhi yao walikuwa na mashetani, wengine walikuwa na kifafa na wengine walikuwa wamepooza. Yesu akawaponya wote. 25 Makundi makubwa ya watu walimfuata; watu kutoka Galilaya, na jimbo lililoitwa Miji Kumi,[i] Yerusalemu, Yuda na maeneo ng'ambo ya Mto Yordani.

Mafundisho ya Yesu Mlimani

(Lk 6:20-23)

Yesu alipoyaona makundi ya watu, alipanda kwenye kilima na kukaa chini. Wanafunzi wake walimjia Yesu. Kisha Yesu akaanza kuwafundisha watu kwa akasema:

“Heri[j] kwa walio maskini na wenye kujua kwamba wanamhitaji Mungu.[k]
    Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.
Heri kwa wenye huzuni sasa.
    Kwa kuwa watafarijiwa na Mungu.
Heri kwa walio wapole.
    Kwa kuwa watairithi nchi.[l]
Heri kwa wenye kiu na njaa ya kutenda haki.[m]
    Kwa kuwa Mungu ataikidhi kiu na njaa yao.
Heri kwa wanaowahurumia wengine.
    Kwa kuwa watahurumiwa pia.
Heri kwa wenye moyo safi,[n]
    Kwa kuwa watamwona Mungu.
Heri kwa wanaotafuta amani.[o]
    Kwa kuwa wataitwa watoto wa Mungu.
10 Heri kwa wanaoteswa kwa sababu ya kutenda haki.
    Kwa kuwa ufalme wa Mungu ni wao.

11 Heri kwenu ninyi pale watu watakapowatukana na kuwatesa. Watakapodanganya na akasema kila neno baya juu yenu kwa kuwa mnanifuata mimi. 12 Furahini na kushangilia kwa sababu thawabu kuu inawasubiri mbinguni. Furahini kwa kuwa ninyi ni kama manabii walioishi zamani. Watu waliwatendea wao mambo mabaya kama haya pia.

Ninyi ni Kama Chumvi na Nuru

(Mk 9:50; 4:21; Lk 14:34-35; 8:16)

13 Mnahitajika kama chumvi inavyohitajiwa na wale waliopo duniani. Lakini chumvi ikipoteza ladha yake, haiwezi kufanywa chumvi tena. Haina manufaa yo yote isipokuwa hutupwa nje na kukanyagwa na watu.

14 Ninyi ni nuru inayong'aa ili ulimwengu uweze kuiona. Ni kama mji uliojengwa juu ya kilima unavyoonekana wazi. 15 Watu hawawashi taa na kuificha kwenye chungu. Bali huiweka kwenye kinara cha taa ili nuru iangaze kwa kila mtu. 16 Kwa namna hiyo hiyo mnapaswa kuwa nuru kwa ajili ya watu wengine. Hivyo ishini katika namna ambayo watakapoyaona matendo yenu mema, watamtukuza Baba yenu wa mbinguni.

Yesu Afundisha Kuhusu Sheria ya Musa

17 Msifikiri kwamba nimekuja kuiharibu Sheria ya Musa au mafundisho ya manabii. Sikuja kuyaharibu mafundisho yao bali kuyakamilisha. 18 Ninawahakikishia kuwa hakuna jambo litakaloondolewa katika sheria mpaka mbingu na nchi zitakapopita. Hakuna hata herufi ndogo ama nukta katika Sheria ya Musa itakayotoweka mpaka hapo itakapotimizwa.

19 Kila mtu anapaswa kutii kila amri iliyo katika sheria, hata ile isiyoonekana kuwa ya muhimu. Kila atakayevunja mojawapo ya amri hizi ndogo na kuwafundisha wengine kuzivunja atahesabiwa kuwa ni mdogo sana katika ufalme wa Mungu. Lakini kila anayeitii na kuwafundisha wengine kuitii sheria atakuwa mkuu katika ufalme wa Mungu. 20 Ninawambia, ni lazima muitii sheria ya Mungu kwa kiwango bora kuliko kile cha walimu wa sheria na Mafarisayo. La sivyo, hamtaweza kuingia katika ufalme wa Mungu.

Yesu Afundisha Kuhusu Hasira

21 Mmesikia kuwa hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Usimwue yeyote. Na yeyote atakayeua atahukumiwa.’(K) 22 Lakini ninawaambia, msimkasirikie mtu yeyote kwa sababu mkifanya hivyo mtahukumiwa. Na mkimtukana mtu yeyote, vivyo hivyo mtahukumiwa na baraza kuu. Na ukimwita mtu kuwa ni mjinga, utakuwa katika hatari ya kutupwa kwenye moto wa Jehanamu.

23 Unapokwenda kutoa sadaka yako madhabahuni na ukakumbuka kuwa kuna mtu ana jambo dhidi yako. 24 Unapaswa kuiacha sadaka yako kwenye madhabahu na uende kupatana na mtu huyo. Ukiisha patana naye ndipo urudi na kuitoa sadaka hiyo.

25 Akiwepo mtu anayetaka kukushtaki, patana naye haraka. Jitahidi kufanya hivyo kabla ya kufika mahakamani, hata kama bado mpo njiani. Usipofanya hivyo anaweza kukupeleka kwa hakimu. Na hakimu atakupeleka kwa walinzi watakaokufunga gerezani. 26 Ninakuhakikishia kuwa hautatoka huko mpaka umelipa kila kitu unachodaiwa.

Yesu Afundisha Kuhusu Uzinzi

27 Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Usizini’.(L) 28 Lakini ninawaambia kuwa mwanaume akimwangalia mwanamke na akamtamani, amekwisha kuzini naye katika akili yake. 29 Jicho la kuume likikufanya utende dhambi, liondoe na ulitupe. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote ukatupwa Jehanamu. 30 Na mkono wako wa kuume ukikufanya utende dhambi, uukate na kuutupa. Ni bora kupoteza sehemu moja ya mwili wako kuliko mwili wako wote kutupwa Jehanamu.

Yesu Afundisha Kuhusu Talaka

(Mt 19:9; Mk 10:11-12; Lk 16:18)

31 Ilisemwa pia kuwa, ‘Kila anayemtaliki mkewe ni lazima ampe hati ya talaka.’(M) 32 Lakini ninawaambia kuwa, kila atakayemtaliki mkewe kutokana na sababu isiyohusiana na uzinzi, anamfanya mke wake kuwa mzinzi. Na kila atakayemwoa mwanamke aliyetalikiwa, atakuwa anazini.

Yesu Afundisha Kuhusu Kiapo

33 Pia, mmesikia hapo kale baba zetu waliambiwa, ‘Unaweka kiapo, usishindwe kutimiza kile ulichoapa kufanya. Timiza kiapo ulichoweka mbele za Bwana.’ 34 Lakini ninawaambia mnapoweka ahadi, msiape kwa jina la mbingu, kwa sababu mbingu ni kiti cha enzi cha Mungu. 35 Na usiape kwa jina la dunia kwa sababu, dunia ni mahali pa kuweka miguu yake. Wala msiape kwa jina la mji wa Yerusalemu, kwa sababu nao ni mali yake Mungu, aliye Mfalme Mkuu. 36 Pia usiape kwa jina la kichwa chako kana kwamba ni uthibitisho kuwa utatimiza kiapo, kwa sababu huwezi kuufanya hata unywele mmoja wa kichwa chako kuwa mweusi au mweupe. 37 Sema ‘ndiyo’ tu kama una maana ya ndiyo na ‘hapana’ tu kama una maana ya hapana. Ukisema zaidi ya hivyo, utakuwa unatoa kwa Yule Mwovu.

Yesu Afundisha Kuhusu Kisasi

(Lk 6:29-30)

38 Mmesikia ilisemwa, ‘Jicho kwa jicho na jino kwa jino.’(N) 39 Lakini ninawaambia msishindane na yeyote anayetaka kuwadhuru. Mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na la kushoto pia. 40 Mtu akitaka kukushitaki ili akunyang'anye shati, mpe na koti pia. 41 Askari akikulazimisha kwenda naye maili moja,[p] nenda maili mbili pamoja naye. 42 Mpe kila anayekuomba, usimkatalie anayetaka kuazima kitu kwako.

Wapende Adui Zako

(Lk 6:27-28,32-36)

43 Mmesikia ilisemwa kuwa, ‘Wapende rafiki zako(O) na wachukie adui zako.’ 44 Lakini ninawaambia wapendeni adui zenu na waombeeni wale wanaowatendea vibaya. 45 Mkifanya hivi mtakuwa watoto halisi walio kama Baba yenu wa mbinguni. Yeye huwaangazia jua watu wote, bila kujali ikiwa ni wema au wabaya. Huwanyeshea mvua wenye haki na wasio haki. 46 Ikiwa mnawapenda wale wanaowapenda ninyi, kwa nini mpate thawabu toka kwa Mungu? Hata watoza ushuru hufanya hivyo. 47 Na ikiwa mnakuwa wema kwa rafiki zenu tu, ninyi si bora kuliko wengine. Hata watu wasiomjua Mungu ni wakarimu kwa rafiki zao pia. 48 Ninalosema ni kuwa, mkue hata kufikia upendo kamili[q] alionao baba yenu wa Mbinguni kwa watu wote.

Yesu Afundisha Kuhusu Kutoa

Mnapofanya jambo jema, kuweni waangalifu msilifanye mbele za watu wengine ili wawaone. Mtakapofanya hivyo hamtapata thawabu kutoka kwa Baba yenu wa mbinguni.

Unapowapa maskini na wahitaji, usilipigie mbiu sana jambo hilo. Maana hivyo ndivyo wanavyofanya wanafiki kwenye makusanyiko.[r] Wao hupiga mbiu kabla ya kutoa ili watu wawaone, kwa kuwa hutaka kila mtu awasifu. Ukweli ni kuwa, hiyo ndiyo thawabu yote waliyokwishapata. Hivyo unapowapa maskini, mtu yeyote asijue unachofanya.[s] Kutoa kwako kunapaswa kufanyika sirini kwa kuwa Baba yako huona mambo yanayofanywa sirini, naye atakupa thawabu.

Yesu Afundisha Kuhusu Maombi

(Lk 11:2-4)

Mnapoomba, msiwe kama wanafiki. Wanapenda kusimama kwenye masinagogi na kwenye pembe za mitaa na kuomba kwa kupaza sauti. Wanapenda kuonwa na watu. Ukweli ni kuwa hiyo ndiyo thawabu yote watakayopata. Lakini unapoomba, unapaswa kuingia katika chumba chako cha ndani na ufunge mlango. Kisha mwombe Baba yako aliye mahali pa siri. Yeye anayaona mambo yanayofanyika katika siri na hivyo atakupa thawabu.

Na unapoomba usiwe kama watu wasiomjua Mungu. Wao kila wanapoomba wanarudia maneno yale yale, tena na tena, wakidhani kuwa wanapoyarudia maneno hayo mara nyingi watasikiwa na Mungu na kujibiwa maombi yao. Msiwe kama wao. Baba yenu anajua yale mnayohitaji kabla hamjamwomba. Hivyo, hivi ndivyo mnapaswa kuomba:

‘Baba yetu uliye mbinguni,
    Jina lako lipewe utukufu.
10 Ufalme wako uje.
Mapenzi yako yafanyike hapa dunia,
    kama yanavyofanyika huko mbinguni.
11 Utupe leo chakula tunachohitaji.
12 Utusamehe dhambi zetu,
    kama tunavyowasamehe wale wanaotukosea.
13 Usiruhusu tukajaribiwa,
    lakini utuokoe na Yule Mwovu.’[t]

14 Mkiwasemehe wengine makosa waliyowatendea, Baba yenu wa mbinguni naye atawasamehe makosa yenu pia. 15 Lakini msipowasamehe wengine, Baba Yenu wa mbinguni hatawasamehe ninyi.

Yesu Afundisha Kuhusu Kufunga

16 Mnapofunga, msijionyeshe kuwa na huzuni kama wanafiki wanavyofanya. Hukunja nyuso zao kwa kuonesha kuwa wana huzuni ili watu wawaone kuwa wamefunga. Ukweli ni kuwa wamekwishapata thawabu yao yote. 17 Hivyo unapofunga, nawa uso wako na ujiweke katika mwonekano mzuri, 18 ili watu wasijue kuwa umefunga, isipokuwa Baba yako, aliye nawe hata sirini. Anaweza kuona yanayofanywa sirini, naye atakupa thawabu.

Huwezi Kuwatumikia Mabwana Wawili

(Lk 12:33-34; 11:34-36; 16:13)

19 Msijiwekee hazina hapa duniani, mahali nondo na kutu[u] huiharibu. Na wezi wanaweza kuvunja nyumba yako na kuziiba. 20 Badala yake jiwekeeni hazina mbinguni ambako haziwezi kuharibiwa na nondo wala kutu na ambako wezi hawawezi kuvunja na kuziiba. 21 Kwa kuwa roho yako itakuwa mahali ilipo hazina yako.

22 Jinsi unavyowaangalia watu wengine ndivyo inavyoonyesha jinsi wewe mwenyewe ulivyo ndani yako. Ukiwaangalia watu kwa nia njema utajawa na nuru ndani yako. 23 Lakini ukiwaangalia watu kwa nia mbaya, utajawa na giza ndani yako. Na ikiwa yote yanayoonekana ndani yako ni giza peke yake, basi unalo giza baya zaidi![v]

24 Hamwezi kuwatumikia mabwana wawili kwa wakati mmoja. Mtamchukia mmoja na kumpenda yule mwingine au mtakuwa waaminifu kwa mmoja na kumdharau yule mwingine. Hamwezi kumtumikia Mungu pamoja na pesa.[w]

Utangulizeni Kwanza Ufalme wa Mungu

(Lk 12:22-34)

25 Kwa hiyo ninawaambia, msiyahangaikie mahitaji ya mwili; mtakula nini, mtakunywa nini au mtavaa nini. Uhai ni zaidi ya chakula na mavazi. 26 Waangalieni ndege wa angani. Hawapandi, hawavuni wala kutunza chakula ghalani, lakini Baba yenu wa mbinguni huwalisha. Je, hamjui kuwa ninyi mna thamani zaidi ya ndege? 27 Hamwezi kujiongezea muda wa kuishi kwa kujisumbua.

28 Na kwa nini mna wasiwasi kuhusu mavazi? Yaangalieni maua ya kondeni. Yatazameni namna yanavyomea. Hayafanyi kazi wala kujitengenezea mavazi. 29 Lakini ninawaambia kuwa hata Suleimani, mfalme mkuu na tajiri, hakuvikwa vizuri kama mojawapo ya maua haya. 30 Ikiwa Mungu anayafanya majani yanayoota mashambani kuwa mazuri mnafikiri atawafanyia ninyi kitu gani? Hayo ni majani tu, siku moja yako hai na siku inayofuata hutupwa katika moto. Lakini Mungu anajali kiasi cha kuyafanya kuwa mazuri ya kupendeza. Muwe na hakika basi atawapa ninyi mavazi mnayohitaji. Imani yenu ni ndogo sana!

31 Msijisumbue na kusema, ‘Tutakula nini?’ au ‘Tutakunywa nini?’ au ‘Tutavaa nini?’ 32 Haya ndiyo mambo ambayo watu wasiomjua Mungu huyawazia daima. Msiwe na wasiwasi, kwa sababu Baba yenu wa mbinguni anajua kuwa mnayahitaji haya yote. 33 Utafuteni kwanza ufalme wa Mungu na mambo yote ambayo Mungu anahesabu kuwa ni mema na yenye haki. Ndipo Mungu atakapowapa yote mnayohitaji. 34 Msiisumbukie kesho. Kwa kuwa kesho itajisumbukia yenyewe. Kila siku ina mahangaiko yake ya kutosha.

Iweni Waangalifu Mnapokosoa Wengine

(Lk 6:37-38,41-42)

Msiwahukumu wengine, ili Mungu asiwahukumu ninyi pia. Mtahukumiwa jinsi ile ile mnavyowahukumu wengine. Mungu atawatendea kama mnavyowatendea wengine.

Kwa nini unaona vumbi iliyo katika jicho la rafiki yako, na hujali kipande cha mti kilicho katika jicho lako? Kwa nini unamwambia rafiki yako, ‘Ngoja nitoe vumbi lililo katika jicho lako wakati wewe mwenyewe bado una kipande cha mti katika jicho lako?’ Ewe mnafiki! Ondoa kwanza kipande cha mti katika jicho lako mwenyewe, ndipo utaweza kuona vizuri na kutoa vumbi katika jicho la rafiki yako.

Msiwape mbwa kitu kitakatifu, watawageuka na kuwadhuru. Na msiwatupie nguruwe lulu zenu kwa kuwa watazikanyaga tu.

Mwombeni Mungu Kile Mnachohitaji

(Lk 11:9-13)

Endeleeni kumwomba Mungu, naye atawapa, endeleeni kutafuta nanyi mtapata, endeleeni kubisha nanyi mtafunguliwa mlango. Ndiyo, yeyote anayeendelea kuomba atapokea. Yeyote anayeendelea kutafuta atapata. Na yeyote anayeendelea kubisha atafunguliwa mlango.

Ni nani kati yenu aliye na mwana ambaye akimwomba mkate atampa jiwe? 10 Au akimwomba samaki, atampa nyoka? Bila shaka hakuna! 11 Ijapokuwa ninyi watu ni waovu, lakini bado mnajua kuwapa vitu vyema watoto wenu. Hakika Baba yenu wa mbinguni atawapa vitu vyema wale wamwombao.

Kanuni ya Muhimu Sana

12 Watendee wengine kama ambavyo wewe ungetaka wao wakutendee. Hii ndiyo tafsiri ya torati[x] na mafundisho ya manabii.

Wachache tu Ndiyo Huiona Njia ya Uzima

(Lk 13:24)

13 Unapaswa kuingia katika uzima wa kweli kupitia lango lililo jembamba. Kwa kuwa lango ni pana na njia inayoelekea katika uharibifu nayo ni pana na watu wengi wanaifuata njia hiyo. 14 Lakini lango la kuelekea katika uzima wa kweli ni jembamba. Na njia iendayo huko ni ngumu kuifuata. Na ni watu wachache wanaoiona.

Kile Wanachokifanya watu Kinadhihirisha jinsi gani Walivyo

(Lk 6:43-44; 13:25-27)

15 Mjihadhari na manabii wa uongo wanaokuja kwenu wakijifanya kondoo wasio na madhara ingawa ni watu hatari kama mbwa mwitu. 16 Mtawatambua watu hawa kwa matendo yao. Mambo mazuri hayatoki kwa watu wabaya, kama ambavyo zabibu haitokani na miiba, na tini hazitokani na mbigiri. 17 Vile vile, kila mti mzuri huzaa matunda mazuri na mti mbaya huzaa matunda mabaya. 18 Mti mzuri hauwezi kuzaa matunda mabaya, na wala mti mbaya hauwezi kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa matunda mazuri hukatwa na kutupwa kwenye moto. 20 Mtawatambua manabii hawa wa uongo kwa matendo yao.

21 Si kila aniitaye Bwana ataingia katika ufalme wa Mungu. Watakaoingia ni wale tu wafanyao yale ambayo Baba yangu wa mbinguni anataka. 22 Siku ya mwisho wengi wataniiita Bwana. Watasema, ‘Bwana, kwa nguvu za jina lako tulihubiri. Na kwa nguvu za jina lako tulitoa mashetani na kufanya miujiza mingi.’ 23 Ndipo nitawaambia waziwazi, ‘Ondokeni kwangu, ninyi waovu. Sikuwahi kuwajua.’

Aina Mbili za Watu

(Lk 6:47-49)

24 Kila anayeyasikia mafundisho yangu na kuyatii ni kama mwenye hekima aliyejenga nyumba yake kwenye mwamba. 25 Mvua kubwa iliponyesha na mafuriko yakaja, na upepo ukavuma sana, na kuipiga sana nyumba yake. Lakini, nyumba yake haikuanguka kwa sababu ilijengwa kwenye mwamba.

26 Lakini kila anayeyasikia mafundisho yangu na asiyatii ni kama mjinga aliyejenga nyumba yake kwenye mchanga. 27 Mvua kubwa iliponyesha na mafuriko kuja, na upepo ukavuma sana, nyumba yake ilianguka kwa kishindo kikuu.”

28 Yesu alipomaliza kufundisha, watu walishangaa sana namna alivyokuwa akifundisha. 29 Hakufundisha kama walimu wao wa sheria; alifundisha kwa mamlaka.[y]

Yesu Amponya Mgonjwa

(Mk 1:40-45; Lk 5:12-16)

Yesu alipotelemka kutoka kwenye kilima, umati mkubwa wa watu ulimfuata. Mtu mmoja mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi akamwendea, akainama mbele yake mpaka chini na akasema, “Bwana ukitaka una uwezo wa kuniponya.”

Yesu aliunyoosha mkono wake akamshika mtu yule mwenye ugonjwa mbaya sana wa ngozi. Akasema, “Hakika, ninataka kukuponya. Upone!” Mtu huyo akapona ugonjwa mbaya sana wa ngozi saa hiyo hiyo. Kisha Yesu akamwambia, “Usimwambie mtu yeyote kilichotokea, lakini nenda kwa kuhani akakuchunguze.[z] Na umtolee Mungu sadaka ambazo Musa aliamuru watu wanaoponywa watoe, ili iwe ushahidi kwa watu kwamba umepona.”

Yesu Amponya Mtumishi wa Afisa wa Jeshi

(Lk 7:1-10; Yh 4:43-54)

Yesu alikwenda Kapernaumu. Alipoingia mjini, afisa wa jeshi alimjia na kumwomba msaada. Akasema, “Bwana, mtumishi wangu ni mgonjwa sana nyumbani na amelala kitandani. Hawezi hata kutingishika na ana maumivu makali sana.”

Yesu akamwambia yule afisa, “Nitakwenda nimponye.”

Yule afisa akajibu, “Bwana, mimi si mwema kiasi cha wewe kuingia katika nyumba yangu. Toa amri tu, na mtumishi wangu atapona. Ninajua hii, kwa kuwa ninaelewa mamlaka. Kuna watu wenye mamlaka juu yangu, na nina askari walio chini ya mamlaka yangu. Nikimwambia askari mmoja ‘nenda’, huenda. Na nikimwambia mwingine ‘njoo’, huja. Pia nikimwambia mtumwa wangu ‘fanya hiki’, hunitii.”

10 Yesu aliposikia maneno hayo alishangaa. Akawaambia wale waliokuwa wakifuatana naye, “Ukweli ni kuwa, mtu huyu ana imani kuliko mtu yeyote niliyewahi kumwona katika Israeli. 11 Watu wengi watakuja kutoka mashariki na magharibi, nao wataketi na kula pamoja na Ibrahimu, Isaka, na Yakobo katika ufalme wa Mungu. 12 Na wale wanaopaswa kuwa katika ufalme watatupwa nje gizani. Na huko watalia na kusaga meno yao kwa sababu ya maumivu.”

13 Kisha Yesu akamwambia yule afisa, “Rudi nyumbani kwako. Mtumishi wako atapona kama unavyoamini.” Mtumishi wa afisa huyo akapona wakati ule ule.

Yesu Awaponya Watu Wengi

(Mk 1:29-34; Lk 4:38-41)

14 Yesu alipofika nyumbani kwa Petro, alimkuta mama mkwe wake Petro amelala kitandani akiwa na homa. 15 Akamgusa mkono wake na homa ikamwacha, kisha akasimama na kuanza kumhudumia.

16 Ilipofika jioni, watu wengi waliokaliwa na mashetani waliletwa kwa Yesu. Naye aliyaamuru mashetani hayo kuwaacha watu. Na aliowaponya wagonjwa wote. 17 Hii ilitokea ili kutimiza maneno yaliyosemwa na nabii Isaya aliposema:

“Aliyaondoa magonjwa yetu
    na kuyabeba madhaifu yetu.”(P)

Kumfuata Yesu

(Lk 9:57-62)

18 Yesu alipoona kundi la watu waliomzunguka, aliawaambia wafuasi waende upande mwingine wa ziwa. 19 Kisha, mwalimu wa sheria ya Musa akamwendea na kumwambia, “Mwalimu, nitakufuata kila mahali utakapokwenda.”

20 Yesu akamwambia, “Mbweha wana mashimo wanamoishi, ndege wana viota. Lakini Mwana wa Adamu hana mahali pa kupumzika.”

21 Mmoja wa wanafunzi wake akamwambia, “Bwana mimi pia nitakufuata, lakini niruhusu kwanza nikamzike baba yangu.”

22 Lakini Yesu akamwambia, “Nifuate mimi, na uwaache wale waliokufa wawazike wafu wao.”

Yesu Atuliza Dhoruba

(Mk 4:35-41; Lk 8:22-25)

23 Yesu alipanda mashua pamoja na wanafunzi wake. 24 Baada ya mashua kutoka pwani, upepo wenye nguvu sana ukaanza kuvuma ziwani. Mawimbi yakaifunika mashua. Lakini Yesu alikuwa amelala. 25 Wanafunzi wake wakamwendea, wakamwamsha. Wakamwambia, “Bwana tuokoe! Tutazama majini!”

26 Yesu akawaambia, “Kwa nini mnaogopa? Hamna imani ya kutosha.” Yesu akasimama akaukemea upepo na mawimbi, na ziwa likatulia.

27 Wanafunzi wake wakashangaa sana, wakasema, “Huyu ni mtu wa namna gani? Hata upepo na maji vinamtii!”

Yesu Afukuza Mashetani Kutoka Kwa Watu Wawili

(Mk 5:1-20; Lk 8:26-39)

28 Yesu alifika ng'ambo ya ziwa katika nchi walimoishi Wagadarini.[aa] Hapo wanaume wawili waliokuwa na mashetani ndani yao na kuishi makaburini walimwijia Yesu. Watu hao walikuwa hatari sana na watu hawakuitumia njia iliyopita karibu na makaburi yale. 29 Wakapaza sauti na akasema, “Unataka nini kwetu, Mwana wa Mungu? Umekuja kutuadhibu kabla ya wakati uliopangwa?”

30 Mbali kidogo na mahali hapo lilikuwepo kundi la nguruwe waliokuwa wanapata malisho yao. 31 Mashetani yakamsihi Yesu yakasema, “Ikiwa utatufukuza kutoka ndani ya watu hawa, tafadhali tuache tuwaingie wale nguruwe.”

32 Ndipo akawaamuru na akasema, “Nendeni!” Wale mashetani wakatoka ndani ya wale watu na kuwaingia nguruwe. Kisha kundi lote la nguruwe likaporomoka ziwani na nguruwe wote wakazama na kufa. 33 Wachungaji waliokuwa wakiwachunga wale nguruwe wakakimbia. Wakaenda mjini na kuwaambia watu kila kitu kilichotukia, hasa juu ya wanaume wale wawili waliokuwa na mashetani. 34 Kisha watu wote mjini walikwenda kumwona Yesu. Walipomwona, walimsihi aondoke katika eneo lao.

Yesu Amponya Aliyepooza

(Mk 2:1-12; Lk 5:17-26)

Yesu akapanda katika mashua na akasafiri kwa kukatisha ziwa kurudi kwenye mji wake. Baadhi ya watu wakamletea mtu aliyepooza akiwa amelala kwenye machela. Yesu alipoona imani waliyokuwa nayo, alimwambia yule mtu aliyepooza, “Changamka mtoto wangu! Dhambi zako zimesamehewa.”

Baadhi ya walimu wa sheria walisikia alichosema Yesu. Wakaambizana wao kwa wao, “Si anamtukana Mungu mtu huyu akasema hivyo!”

Yesu alipotambua walichokuwa wanafikiri, akasema, “Kwa nini mna mawazo maovu kama hayo mioyoni mwenu? Wakati akiwa duniani Mwana wa Adamu anayo mamlaka ya kusamehe dhambi. Lakini nitawezaje kulithibitisha hili kwenu? Pengine mnafikiri ilikuwa rahisi kwangu kumwambia mtu huyu aliyepooza, ‘Dhambi zako zimesamehewa.’ Kwa sababu hilo haliwezi kuthibitishwa kwamba hakika limetokea. Lakini vipi nikimwambia mtu huyu, ‘Simama! Beba kitanda chako na utembee’? Hapo ndipo mtakapoweza kuona kama kweli ninayo mamlaka hayo ama sina.” Kwa hiyo Yesu akamwambia mtu yule aliyepooza, “Nitalithibitishaje hili kwako? Ninakwambia hivi, ‘Inuka! Beba kitanda chako uende nyumbani!’”

Mtu yule akasimama na kwenda nyumbani. Watu walipoliona tukio hili wakashangaa. Wakamsifu Mungu kwa kuwapa watu mamlaka hii.

Mathayo Amfuata Yesu

(Mk 2:13-17; Lk 5:27-32)

Yesu alipokuwa anaondoka, alimwona mtu aliyeitwa Mathayo amekaa mahali pa kukusanyia ushuru. Yesu akamwambia, “Nifuate.” Hivyo Mathayo akasimama na kumfuata Yesu.

10 Baadaye Yesu alikula chakula nyumbani kwa Mathayo. Watoza ushuru wengi na watu wenye sifa mbaya walikuja na kula chakula pamoja na Yesu pamoja na wafuasi wake. 11 Mafarisayo walipoona kuwa Yesu anakula pamoja na watu hao, wakawauliza wanafunzi wake, “Kwa nini mwalimu wenu anakula pamoja na watoza ushuru na wenye dhambi wengine?”

12 Yesu alipowasikia wakisema hili, akawaambia, “Wagonjwa ndiyo wanaohitaji daktari si wenye afya. 13 Nendeni mkajifunze andiko hili linamaanisha nini: ‘Sihitaji dhabihu ya mnyama; Ninataka ninyi mwoneshe wema kwa watu.’(Q) Sikuja kuwaalika wema kujiunga nami, bali wenye dhambi.”

Swali Kuhusu Kufunga

(Mk 2:18-22; Lk 5:33-39)

14 Kisha wafuasi wa Yohana wakamjia Yesu na kusema, “Sisi na Mafarisayo tunafunga mara kwa mara, lakini wafuasi wako hawafungi. Kwa nini?”

15 Yesu akajibu, “Kwenye harusi marafiki wa bwana harusi hawana huzuni anapokuwa pamoja nao, hivyo hawawezi kufunga. Lakini wakati unakuja ambao bwana harusi ataondolewa kwao. Ndipo watakuwa na huzuni kisha watafunga.

16 Mtu anaposhona kiraka kwenye vazi la zamani, atatumia kiraka chakavu. Akitumia kiraka kipya vazi lake litachanika kwa sababu ya kusinyaa kwa kiraka hicho kipya. Kisha tundu litakuwa baya zaidi. 17 Pia, watu hawawaweki divai mpya kwenye viriba[ab] vya zamani. Wakifanya hivyo viriba vitapasuka, na divai itamwagika na viriba vitaharibika. Daima watu huweka divai mpya katika viriba vipya, ambavyo haviwezi kupasuka, na divai huwa salama.”

Yesu Anampa Uhai Msichana Aliyekufa na Kumponya Mwanamke Mgonjwa

(Mk 5:21-43; Lk 8:40-56)

18 Yesu alipokuwa bado anaongea, kiongozi wa sinagogi akamwendea. Kiongozi akainama chini mbele yake na akasema, “Binti yangu amekufa sasa hivi. Lakini ikiwa utakuja na kumgusa kwa mkono wako, atafufuka.”

19 Hivyo Yesu na wafuasi wake wakaenda na mtu huyo.

20 Wakiwa njiani, alikuwepo mwanamke aliyekuwa akitokwa damu kwa miaka kumi na mbili. Alimwendea Yesu kwa nyuma na akagusa sehemu ya chini ya vazi lake. 21 Aliwaza, “Ikiwa nitagusa tu joho lake, nitapona.”

22 Yesu aligeuka na kumwona mwanamke. Akasema, “Uwe na furaha, mwanamke. Imani yako imekuponya.” Kisha yule mwanamke akapona saa ile ile.

23 Yesu aliendelea kwenda na kiongozi wa Kiyahudi na kuingia nyumbani kwake. Aliwaona watu wapigao muziki kwa ajili ya mazishi pale. Na aliliona kundi la watu waliohuzunika sana. 24 Yesu akasema, “Ondokeni. Msichana hajafa. Amelala tu.” Lakini watu wakamcheka. 25 Baada ya watu kutolewa nje ya nyumba, Yesu aliingia kwenye chumba cha msichana. Aliushika mkono wa msichana na msichana akasimama. 26 Habari kuhusu jambo hili ilienea kila mahali katika eneo lile.

Yesu Awaponya Watu Watatu

27 Yesu alipokuwa anaondoka kutoka pale, wasiyeona wawili walimfuata. Walisema kwa sauti, “Mwana wa Daudi, uwe mwema kwetu.”

28 Baada ya Yesu kuingia ndani, wasiyeona wakamwendea. Akawauliza, “Mnaamini kuwa ninaweza kuwafanya muone?” Wakajibu, “Ndiyo, Bwana, tunaamini.”

29 Kisha Yesu akayagusa macho yao na akasema, “Kwa kuwa mnaamini kuwa ninaweza kuwafanya muone, hivyo itatokea.” 30 Ndipo wakaweza kuona. Yesu akawaonya kwa nguvu. Akasema, “Msimwambie yeyote kuhusu hili.” 31 Lakini waliondoka na kutawanya habari kuhusu Yesu kila mahali katika eneo lile.

32 Watu hawa wawili walipokuwa wanaondoka, baadhi ya watu walimleta mtu mwingine kwa Yesu. Mtu huyu alikuwa haongei kwa sababu alikuwa na pepo ndani yake. 33 Yesu akamtoa nje pepo na mtu yule aliweza kuongea. Watu walishangaa na akasema, “Hakuna mtu yeyote aliyewahi kuona kitu kama hiki katika Israeli.”

34 Lakini Mafarisayo walisema, “Mtawala wa mashetani ndiye anayempa nguvu ya kuyatoa mashetani.”

Mwombeni Mungu Atume Watenda Kazi Zaidi

35 Yesu alisafiri akipita katika miji yote na vijiji. Alifundisha katika masinagogi yao na kuwaeleza watu Habari Njema kuhusu ufalme wa Mungu. Aliponya kila aina ya magonjwa na udhaifu. 36 Yesu aliona watu wengi na kuwahurumia kwa sababu walikuwa wanakandamizwa na hawakuwa na tumaini; kama kondoo bila mchungaji wa kuwaongoza. 37 Yesu akawaambia wafuasi wake, “Kuna mavuno mengi ya watu ya kuleta. Lakini kuna wafanyakazi wachache wa kusaidia kuwavuna. 38 Mungu anamiliki mavuno. Mwombeni atume wafanyakazi wengi zaidi wa kusaidia kukusanya mavuno yake.”

Yesu Awatuma Kazi Mitume Wake

(Mk 3:13-19; 6:7-13; Lk 6:12-16; 9:1-6)

10 Yesu aliwaita pamoja wafuasi wake kumi na mbili. Akawapa uwezo juu ya pepo wabaya ili waweze kuwafukuza na pia kuponya kila aina ya magonjwa na maradhi. Haya ni majina ya mitume kumi na wawili:

Simoni (ambaye pia aliitwa Petro),

Andrea, kaka yake Petro,

Yakobo, mwana wa Zebedayo,

Yohana, kaka yake Yakobo,

Filipo,

Bartholomayo,

Thomaso,

Mathayo, mtoza ushuru,

Yakobo, mwana wa Alfayo,

Thadayo,

Simoni Mzelote,

Yuda Iskariote (yule ambaye baadaye alimsaliti Yesu).

Yesu aliwatuma mitume hawa kumi na wawili pamoja na maelekezo haya: “Msiende kwa watu wasio Wayahudi. Na msiingie katika miji ambako Wasamaria wanaishi. Lakini nendeni kwa watu wa Israeli. Wako kama kondoo waliopotea. Mtakapokwenda, waambieni hivi: ‘Ufalme wa Mungu umekaribia.’ Waponyeni wagonjwa. Fufueni waliokufa. Waponyeni watu wenye magonjwa mabaya sana ya ngozi. Na toeni mashetani kwa watu. Ninawapa nguvu hii bure, hivyo wasaidieni wengine bure. Msibebe pesa pamoja nanyi; dhahabu au fedha au shaba nyekundu. 10 Msibebe mikoba. Chukueni nguo na viatu mlivyovaa tu. Na msichukue fimbo ya kutembelea. Mfanyakazi anastahili kupewa anachohitaji.

11 Mnapoingia katika mji, tafuteni kwa makini hadi mumpate mtu anayefaa na mkae katika nyumba yake mpaka mtakapoondoka mjini. 12 Mtakapoingia katika nyumba hiyo, semeni, ‘Amani iwe kwenu.’ 13 Ikiwa watu katika nyumba hiyo watawakaribisha, wanastahili amani yenu. Wapate amani mliyowatakia. Lakini ikiwa hawatawakaribisha, hawastahili amani yenu. Ichukueni amani mliyowatakia. 14 Na ikiwa watu katika nyumba au mji watakataa kuwapokea au kuwasikiliza, basi ondokeni mahali hapo na mkung'ute mavumbi kutoka katika miguu yenu. 15 Ninaweza kuwathibitishia kuwa siku ya hukumu itakuwa vibaya sana kwa mji huo kuliko watu wa Sodoma na Gomora.[ac]

Yesu Aonya Kuhusu Matatizo

(Mk 13:9-13; Lk 21:12-17)

16 Sikilizeni! Ninawatuma, nanyi mtakuwa kama kondoo katikati ya mbwa mwitu. Hivyo muwe na akili kama nyoka. Lakini pia muwe kama njiwa na msimdhuru yeyote. 17 Muwe waangalifu! Wapo watu watakaowakamata na kuwapeleka ili kuwashitaki mbele ya mabaraza ya mijini. Watawachapa ndani ya masinagogi yao. 18 Mtasimamishwa mbele ya magavana na wafalme. Watu watawafanyia ninyi hivi kwa sababu mnanifuata. Mtakuwa mashahidi wangu mbele za wafalme na magavana hao na kwa watu wa mataifa mengine. 19 Mtakapokamatwa, msisumbuke kuhusu nini mtakachosema au namna gani mtakavyosema. Katika wakati huo mtapewa maneno ya kusema. 20 Si ninyi mtakaoongea; Roho wa Baba Mungu wenu atakuwa anaongea kupitia ninyi.

21 Ndugu watakuwa kinyume cha ndugu zao wenyewe na kuwapeleka kwenda kuuawa. Baba watawapeleka watoto wao wenyewe kuuawa. Watoto watapigana kinyume na wazazi wao na watawapeleka kuuawa. 22 Kila mtu atawachukia kwa sababu mnanifuata mimi. Lakini atakayekuwa mwaminifu mpaka mwisho ataokolewa. 23 Mnapotendewa vibaya katika mji mmoja, nendeni katika mji mwingine. Ninawaahidi kuwa hamtamaliza kwenda katika miji ya Israeli kabla Mwana wa Adamu hajarudi.

24 Wanafunzi si wazuri kuliko mwalimu wao. Watumwa si wazuri kuliko bwana wao. 25 Inatosha kwa wanafunzi kuwa kama walimu wao na watumwa kuwa kama bwana wao. Iwapo watu hao wananiita ‘mtawala wa pepo’, na mimi ni kiongozi wa familia, basi ni dhahiri kwa kiasi gani watawatukana ninyi, mlio familia yangu!

Mwogopeni Mungu, Siyo Watu

(Lk 12:2-7)

26 Hivyo msiwagope watu hao. Kila kitu kilichofichwa kitaoneshwa. Kila kilicho siri kitajulikana. 27 Ninayowaambia ninyi faraghani myaseme hadharani. Kila ninachowanong'oneza nawataka mkiseme kwa sauti kila mtu asikie.

28 Msiwaogope watu. Wanaweza kuua mwili, lakini hawawezi kuiua roho. Mnapaswa kumwogopa Mungu, anayeweza kuuharibu mwili na roho jehanamu. 29 Ndege wanapouzwa, ndege wawili wadogo hugharimu senti moja tu. Lakini hakuna hata mmoja wa ndege hao wadogo anaweza kufa bila Baba yenu kufahamu. 30 Mungu anafahamu idadi ya nywele katika vichwa vyenu. 31 Hivyo msiogope. Mna thamani kuliko kundi kubwa la ndege.

Msiionee Haya Imani Yenu

(Lk 12:8-9)

32 Iwapo mtawaambia watu wengine kuwa mnaniamini, nitamwambia Baba yangu aliye mbinguni kuwa ninyi ni wangu. 33 Lakini ikiwa mtasimama mbele ya wengine na kusema kuwa hamniamini, nitamwambia Baba yangu aliye mbinguni kuwa ninyi si wangu.

Kumfuata Yesu Kunaleta Matatizo

(Lk 12:51-53; 14:26-27)

34 Msidhani kuwa nilikuja duniani kuleta amani. Sikuja kuleta amani. Nilikuja kuleta vita. 35 Nimekuja ili hili litokee:

‘Mwana atamgeuka baba yake.
    Binti atamgeuka mama yake.
Binti mkwe atamgeuka mama mkwe wake.
36     Hata watu wa familia zenu watakuwa adui zenu.’(R)

37 Wale wanaowapenda baba zao au mama zao kuliko wanavyonipenda mimi hawana thamani kwangu. Na wale wanaowapenda wana wao au binti zao kuliko wanavyonipenda mimi hawastahili kuwa wafuasi wangu. 38 Wale ambao hawataupokea msalaba waliopewa wanaponifuata hawastahili kuwa wanafunzi wangu na kunifuata. 39 Wale wanaojaribu kuyatunza maisha waliyonayo, watayapoteza. Lakini wale wanaoyaacha maisha yao kwa ajili yangu watapata uzima halisi.

Mungu Atawabariki Wanaowakaribisha Ninyi

(Mk 9:41)

40 Yeyote anayewakubali ninyi ananikubali mimi. Na yeyote anayenikubali anamkubali yule aliyenituma. 41 Yeyote anayemkubali nabii kwa sababu ni nabii atapata ujira wa nabii. Na yeyote anayemkubali mwenye haki kwa sababu ni mwenye haki atapata ujira anaoupata mwenye haki. 42 Yeyote anayemsaidia mmoja wa wafuasi wangu hawa wanyenyekevu kwa sababu ni wafuasi wangu hakika atapata ujira, hata ikiwa wanawapa tu kikombe cha maji baridi.”

Yohana Atuma Watu Kumwuliza Yesu Swali

(Lk 7:18-35)

11 Yesu alipomaliza maelekezo haya kwa wafuasi wake kumi na wawili wa karibu, aliondoka mahali pale. Akaenda katika miji ya Galilaya kuwafundisha watu na kuwaeleza ujumbe wa Mungu.

Yohana alipokuwa gerezani, alisikia kuhusu mambo yaliyokuwa yanatokea; mambo ambayo Masihi angefanya. Hivyo akawatuma baadhi ya wafuasi wake kwa Yesu. Wakamuuliza, “Wewe ni yule tuliyekuwa tunamngojea, au tumsubiri mwingine?”

Yesu akajibu, “Rudini mkamwambie Yohana yale mliyosikia na kuona: Vipofu wanaona. Viwete wanatembea. Watu wenye magonjwa ya ngozi wanaponywa. Wasiyesikia wanasikia. Wafu wanafufuliwa. Na habari njema inahubiriwa kwa maskini. Heri ni kwa wale wasio na shida kunikubali.”

Wafuasi wa Yohana walipoondoka, Yesu alianza kuongea na watu kuhusu Yohana. Alisema, “Ninyi watu mlikwenda jangwani kuona nini? Mtu aliye dhaifu, kama unyasi unaoyumbishwa na upepo? Hakika, ni nini mlichotarajia kuona? Aliyevaa mavazi mazuri? Hakika si hivyo. Watu wote wanaovaa mavazi mazuri wanapatikana katika ikulu za wafalme. Hivyo mlitoka kuona nini? Nabii? Ndiyo, Yohana ni nabii. Lakini ninawaambia, Yeye ni zaidi ya hilo. 10 Andiko hili liliandikwa kuhusu Yohana:

‘Sikiliza! Nitamtuma mjumbe mbele yako.
    Yeye ataandaa njia kwa ajili yako.’(S)

11 Ukweli ni kuwa Yohana Mbatizaji ni mkuu kuliko yeyote aliyewahi kuja katika ulimwengu huu. Lakini hata mtu asiye wa muhimu katika ufalme wa Mungu ni mkuu kuliko Yohana. 12 Tangu wakati wa Yohana Mbatizaji ulipokuja mpaka sasa, Ufalme wa Mungu umekabiliwa na mashambulizi. Watu wenye nguvu wamejaribu kuudhibiti ufalme huu.[ad] 13 Kabla ya Yohana kuja, Sheria ya Musa na manabii wote wamesema kuhusu mambo ambayo yangetokea. 14 Na ikiwa mnaamini waliyosema, basi Yohana ni Eliya. Ndiye waliyesema angekuja. 15 Ninyi watu mnaonisikia, sikilizeni!

16 Ninaweza kusema nini kuhusu watu wanaoishi leo? Watu siku ya leo ni kama watoto wanaokaa katika masoko. Kundi moja la watoto linaliambia kundi lingine,

17 ‘Tuliwapigia filimbi,
    lakini hamkucheza;
tuliimba wimbo wa maziko,
    lakini hamkuhuzunika.’

18 Kwa nini ninasema watu wako hivyo? Kwa sababu Yohana alikuja na hakula vyakula vya kawaida na kunywa divai, na watu walisema, ‘Ana pepo ndani yake.’ 19 Mwana wa Adamu amekuja akila na kunywa, na watu husema, ‘Mwangalie! Hula sana na kunywa divai nyingi. Ni rafiki wa wakusanya kodi na wenye dhambi wengine.’ Lakini hekima inaonesha kuwa sahihi kutokana na yale inayotenda.”

Maonyo Kwa Wanaomkataa Yesu

(Lk 10:13-15)

20 Kisha Yesu akaanza kuikosoa miji ambako alifanya miujiza yake mingi. Aliikosoa miji hii kwa sababu watu katika miji hii hawakubadili maisha yao na kuacha kutenda dhambi. 21 Yesu alisema, “Itakuwa vibaya kwako Korazini! Itakuwa vibaya kwako Bethsaida![ae] Ikiwa miujiza hii hii ingetokea Tiro na Sidoni,[af] watu huko wangeshabadili maisha yao kitambo. Wangekwishavaa magunia na kujimwagia majivu kuonesha kuwa wanasikitikia dhambi zao. 22 Lakini ninawaambia, siku ya hukumu itakuwa vibaya zaidi kwako kuliko Tiro na Sidoni.

23 Nawe Kapernaumu, utakwezwa mpaka mbinguni? Hapana! Utatupwa chini mpaka Kuzimu. Nimetenda miujiza mingi ndani yako. Iwapo miujiza hii ingetokea Sodoma,[ag] watu huko wangeacha kutenda dhambi na ungekuwa bado ni mji hata leo. 24 Lakini ninakuambia, itakuwa vibaya kwako siku ya hukumu kuliko Sodoma.”

Yesu Awapa Pumziko Watu Wake

(Lk 10:21-22)

25 Kisha Yesu akasema, “Ninakusifu wewe, Baba, Bwana wa mbinguni na duniani. Ninashukuru kwa sababu umeyaficha mambo haya kwa wale wanaofikiri kuwa ni wenye hekima na werevu sana. Lakini umeyaonesha haya kwa watu walio kama watoto wadogo.[ah] 26 Ndiyo, Baba, ulifanya hivi kwa sababu hakika ndivyo ulivyotaka kufanya.

27 Baba yangu amenipa kila kitu. Hakuna amjuaye Mwana isipokuwa Baba peke yake. Na hakuna amjuaye Baba isipokuwa Mwana ndiye anayemjua Baba. Na watu pekee watakaomjua Baba ni wale ambao Mwana atachagua kuwaonesha.

28 Njooni kwangu ninyi nyote mliochoka kutokana na mizigo mizito mnayolazimishwa kubeba. Nitawapa pumziko. 29 Chukueni nira yangu,[ai] jifunzeni kutoka kwangu. Mimi ni mwema na mnyenyekevu katika roho. Nanyi mtaweza kupumzika. 30 Ndiyo, nira yangu ni rahisi. Mzigo ninaowapa muubebe ni mwepesi.”

Yesu ni Bwana Juu ya Siku ya Sabato

(Mk 2:23-28; Lk 6:1-5)

12 Katika wakati huo huo, Yesu alikuwa anasafiri akipita katika mashamba ya nafaka siku ya Sabato. Wafuasi wake walikuwa pamoja naye, na walikuwa na njaa. Hivyo walianza kuchuma nafaka na kula. Mafarisayo walioliona hili, wakamwambia Yesu, “Tazama! Wafuasi wako wanafanya kitu ambacho ni kinyume na sheria yetu kufanya katika siku ya Sabato.”

Yesu akawaambia, “Mmekwisha soma alichofanya Daudi wakati yeye na wale waliokuwa pamoja naye walipokuwa na njaa. Daudi aliingia katika nyumba ya Mungu. Yeye na wale waliokuwa pamoja naye walikula mkate uliotolewa kwa Mungu. Ilikuwa kinyume cha sheria kwa Daudi au wale waliokuwa pamoja naye kula mkate huo. Makuhani pekee ndio walioruhusiwa kuula. Na mmekwisha soma katika Sheria ya Musa kuwa katika kila Sabato makuhani kwenye Hekalu wanavunja Sheria kwa kufanya kazi Siku ya Sabato. Lakini hawakosei kwa kufanya hivyo. Ninawaambia kuwa kuna kitu hapa ambacho ni kikuu kuliko Hekalu. Maandiko yanasema, ‘Sihitaji dhabihu ya wanyama; Ninataka ninyi muoneshe wema kwa watu.’(T) Hakika hamjui hilo linamaanisha nini. Iwapo mngelielewa, msingewahukumu wale ambao hawajafanya chochote kibaya.

Mwana wa Adamu ni Bwana juu ya siku ya Sabato.”

Yesu Amponya Mtu Siku ya Sabato

(Mk 3:1-6; Lk 6:6-11)

Kutoka hapo Yesu alikwenda katika sinagogi lao. 10 Ndani ya sinagogi alikuwemo mtu aliyepooza mkono. Baadhi ya Mafarisayo waliokuwa pale walikuwa wanatafuta sababu ya kumshitaki Yesu kwa kutenda kitu kibaya, hivyo walimuuliza, “Je, ni halali kuponya siku ya Sabato?”

11 Yesu akajibu, “Ikiwa mmoja wenu ana kondoo na akatumbukia shimoni siku ya Sabato, utamsaidia kumtoa yule kondoo katika shimo. 12 Hakika mtu ni bora kuliko kondoo. Hivyo ni sawa kutenda wema siku ya Sabato.”

13 Kisha Yesu akamwambia mtu mwenye mkono uliopooza, “Unyooshe mkono wako.” Mtu yule akaunyoosha mkono wake, na ukawa mzima tena, kama mkono mwingine. 14 Lakini Mafarisayo waliondoka na wakaweka mipango ya kumuua Yesu.

Yesu ni Mtumishi Aliyechaguliwa na Mungu

15 Yesu alitambua kuwa Mafarisayo walikuwa wanapanga kumuua. Hivyo aliondoka mahali pale na watu wengi walimfuata. Akawaponya wote waliokuwa wagonjwa, 16 lakini aliwaonya wasiwaambie wengine yeye alikuwa nani. 17 Hii ilikuwa ni kuthibitisha kile ambacho nabii Isaya alisema alipozungumza kwa niaba ya Mungu:

18 “Hapa ni mtumishi wangu,
    niliyemchagua.
Ndiye ninayempenda,
    na ninapendezwa naye.
Nitamjaza Roho yangu,
    naye ataleta haki kwa mataifa.
19 Hatabishana au kupiga kelele;
    hakuna atakayesikia sauti yake mitaani.
20 Hatavunja wala kupindisha unyasi.
    Hatazimisha hata mwanga hafifu.
Hatashindwa mpaka ameifanya haki kuwa mshindi.
21     Watu wote watatumaini katika yeye.”(U)

Nguvu ya Yesu Inatoka kwa Mungu

(Mk 3:20-30; Lk 11:14-23; 12:10)

22 Kisha baadhi ya watu wakamleta mtu kwa Yesu. Mtu huyu alikuwa asiyeona na hakuweza kuzungumza, kwa sababu alikuwa na pepo ndani yake. Yesu akamponya na akaweza kuzungumza na kuona. 23 Watu wote walikishangaa kile Yesu alichotenda. Walisema, “Pengine ni Mwana wa ahadi wa Daudi!”

24 Mafarisayo waliposikia hili, walisema, “Mtu huyu anatumia nguvu za Shetani[aj] kufukuza mashetani kutoka kwa watu. Beelzebuli ni mtawala wa mashetani.”

25 Yesu alijua kile Mafarisayo walikuwa wanafikiri. Hivyo akawaambia, “Kila ufalme unaopigana wenyewe utateketezwa. Na kila mji au familia iliyogawanyika haiwezi kuishi. 26 Hivyo ikiwa Shetani anayafukuza mashetani[ak] yake mwenyewe, anapigana kinyume chake yeye mwenyewe, na ufalme wake hautaishi. 27 Mnasema kuwa ninatumia nguvu za Shetani kuyatoa mashetani. Ikiwa hiyo ni kweli, sasa ni nguvu gani watu wenu hutumia wanapoyafukuza mashetani? Hivyo watu wenu wenyewe watathibitisha kuwa mmekosea. 28 Lakini ninatumia nguvu ya Roho wa Mungu kuyafukuza mashetani, na hili linaonesha kuwa Ufalme wa Mungu umekuja kwenu. 29 Watu wowote wanaotaka kuingia katika nyumba ya mtu mwenye nguvu na kuiba vitu vyake lazima wamfunge kwanza. Kisha wanaweza kuiba vitu kutoka katika nyumba yake. 30 Yeyote ambaye hayuko pamoja nami yu kinyume nami. Na yeyote ambaye hakusanyi pamoja nami hutawanya.

31 Hivyo ninawaambia, Mungu atawasamehe watu kila dhambi wanayotenda au kila jambo baya wanalosema kinyume naye. Lakini yeyote anayesema kinyume na Roho Mtakatifu hatasamehewa. 32 Unaweza kusema kinyume na Mwana wa Adamu na ukasamehewa. Lakini yeyote anayesema kinyume na Roho Mtakatifu hatasamehewa; si sasa au baadaye.

Yale Unayofanya Yanaonesha Jinsi Ulivyo

(Lk 6:43-45)

33 Ikiwa unataka matunda mazuri, ni lazima uutunze mti vizuri. Ikiwa mti wako siyo mzuri, utakuwa na matunda mabaya. Mti unajulikana kutokana na aina ya matunda inaozalisha. 34 Ninyi nyoka! Ni waovu sana. Mnawezaje mkasema chochote kilicho chema? Kile ambacho watu husema kwa midomo yao kinatoka katika yale yaliyojaa katika mioyo yao. 35 Walio wema wana vitu vizuri vilivyotunzwa katika mioyo yao. Ndiyo maana husema mambo mazuri. Lakini wale walio waovu wana mioyo iliyojaa uovu, na ndiyo sababu husema mambo maovu. 36 Ninawaambia kuwa kila mmoja atajibu kwa ajili ya mambo yasiyo ya maana waliyosema. Hili litatokea siku ya hukumu. 37 Maneno yenu yatatumika kuwahukumu ninyi. Uliyosema yataamua ikiwa una haki mbele za Mungu au unahukumiwa na Mungu.”

Baadhi ya Watu Wawa na Mashaka na Mamlaka ya Yesu

(Mk 8:11-12; Lk 11:29-32)

38 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria wakamjibu Yesu. Wakasema, “Mwalimu, tunataka kukuona ukifanya miujiza kama ishara kuwa unatoka kwa Mungu.”

39 Yesu akajibu, “Watu wenye dhambi na wasio na imani hutafuta kuona muujiza kama ishara kutoka kwa Mungu. Lakini hakuna muujiza utakaofanyika kudhibitisha chochote kwao. Yona[al] ni ishara pekee itakayotolewa kwenu ninyi mlio wa kizazi kiovu cha leo. 40 Yona alikuwa ndani ya tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu, mchana na usiku. Vivyo hivyo, Mwana wa Adamu atakuwa kaburini kwa siku tatu, mchana na usiku. 41 Siku ya hukumu, ninyi watu mnaoishi leo mtalinganishwa na watu wa Ninawi, nao watakuwa mashahidi watakaoonyesha namna mlivyokosea. Kwa nini ninasema hivi? Kwa sababu Yona alipowahubiri watu hao, walibadili maisha yao. Na aliye mkuu kuliko Yona, yupo hapa lakini mnakataa kubadilika!

42 Pia, siku ya hukumu, Malkia wa Kusini[am] atasimama pamoja na wale wanaoishi sasa, atasababisha mhukumiwe kuwa na makosa. Ninasema hivi kwa sababu alisafiri kutoka mbali, mbali sana kuja kusikiliza mafundisho yenye hekima ya Sulemani. Nami Ninawaambia aliye mkuu zaidi ya Sulemani yuko hapa, lakini hamnisikii!

Hatari ya Kuwa Mtupu

(Lk 11:24-26)

43 Roho chafu inapotoka kwa mtu, husafiri katika sehemu kavu ikitafuta mahali pa kupumzika, lakini haipati mahali pa kupumzika. 44 Inapokosa mahali pa kupumzika, husema, ‘Nitarudi katika nyumba niliyotoka.’ Inaporudi, ikakuta nyumba hiyo bado ni tupu, ikiwa safi na nadhifu, 45 hutoka nje na kuleta roho zingine saba zilizo chafu zaidi yake. Huingia na kuishi humo, na mtu huyo anakuwa na matatizo mengi kuliko mwanzo wakati roho chafu moja iliishi ndani yake. Ndivyo ilivyo kwa kizazi hiki cha watu wanaoishi leo.”

Wafuasi wa Yesu ni Familia Yake Halisi

(Mk 3:31-35; Lk 8:19-21)

46 Yesu alipokuwa akiongea na watu, mama yake na ndugu zake walikuwa nje. Walitaka kuongea naye. 47 Mtu mmoja akamwambia, “Mama yako na wadogo zako wanakusubiri nje. Wanataka kuongea nawe.”

48 Yesu akajibu, “Mama yangu ni nani? Ndugu zangu ni nani?” 49 Kisha akanyoosha kidole kwa wafuasi wake na akasema, “Unaona! Watu hawa ni mama yangu na ndugu zangu. 50 Kaka yangu, dada yangu na mama yangu halisi ni yule afanyaye yale Baba yangu wa mbinguni anataka.”

Simulizi Kuhusu Mkulima Aliyepanda Mbegu

(Mk 4:1-9; Lk 8:4-8)

13 Siku hiyo hiyo Yesu alitoka nje ya nyumba na kukaa kando ya ziwa. Kundi kubwa wakakusanyika kumzunguka. Hivyo akapanda mtumbwini na kuketi. Watu wote wakabaki ufukweni. Kisha Yesu akatumia simulizi kuwafundisha mambo mengi. Akawaambia simulizi hii:

“Mkulima alitoka kwenda kupanda mbegu. Alipokuwa anatawanya mbegu, baadhi ziliangukia njiani. Ndege wakaja na kuzila zote. Mbegu zingine ziliangukia kwenye ardhi yenye mawe, ambako hakukuwa na udongo wa kutosha. Zikakua haraka pale, kwa sababu udongo haukuwa na kina. Lakini jua lilipowaka, likaichoma mimea. Mimea ikafa kwa sababu haikuwa na mizizi mirefu. Baadhi ya mbegu ziliangukia katikati ya miiba. Miiba ikakua na kusababisha mimea mizuri kuacha kukua. Lakini baadhi ya mbegu ziliangukia kwenye udongo wenye rutuba. Hapo zikakua na kuzaa nafaka. Baadhi ya mimea ikazaa nafaka mara mia zaidi, baadhi mara sitini na baadhi mara thelathini zaidi. Ninyi watu mnaoweza kunisikia, nisikilizeni!”

Kwa nini Yesu Alitumia Simulizi Kufundisha

(Mk 4:10-12; Lk 8:9-10)

10 Wafuasi wake wakamwendea Yesu na kumuuliza, “Kwa nini unatumia simulizi hizi kuwafundisha watu?”

11 Yesu akawajibu, “Mungu amewapa ninyi ujuzi wa kuelewa siri za ufalme wa Mungu, lakini hajawapa watu hawa wengine ujuzi huu. 12 Kisha akawaambia, ‘Zingatieni kwa makini kile mnachokisikia. Kwani jinsi mnavyosikiliza kwa makini, ndivyo mtakavyoelewa na kuzidi kuelewa. Kwa kuwa kila aliye na uelewa kidogo ataongezewa zaidi. Lakini wale wasiosikiliza kwa makini watapoteza hata ule uelewa mdogo walio nao.’ 13 Ndiyo sababu ninatumia simulizi hizi kuwafundisha watu: Wanaona, lakini hakika hawaoni. Wanasikia, lakini hakika hawasikii au kuelewa. 14 Hiyo inathibitisha alichosema nabii Isaya kuhusu wao kuwa kweli:

‘Ninyi watu mtasikia na kusikia,
    lakini hamtaelewa.
Mtatazama na kutazama,
    lakini hakika hamtaona.
15 Ndiyo, akili za watu hawa sasa zimefungwa.
    Wana masikio, lakini hawasikii vizuri.
Wana macho, lakini wameyafumba.
    Iwapo akili zao zisingekuwa zimefungwa,
wangeona kwa macho yao;
    wangesikia kwa masikio yao;
Iwapo wangeelewa kwa akili zao.
    Kisha wangenigeukia na kuponywa.’(V)

16 Bahati gani mliyonayo ninyi. Mnaelewa mnachokiona kwa macho yenu. Na mnaelewa mnachosikia kwa masikio yenu. 17 Ninaweza kuwathibitishia, manabii na watakatifu wengi walitaka kuona mnayoyaona. Lakini hawakuyaona. Walitaka kusikia mnayosikia sasa. Lakini hawakuyasikia.

Yesu Afafanua Simulizi Kuhusu Mbegu

(Mk 4:13-20; Lk 8:11-15)

18 Hivyo sikilizeni maana ya simulizi hiyo kuhusu mkulima:

19 Vipi kuhusu mbegu zilizoangukia njiani? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho kuhusu ufalme wa Mungu lakini hawauelewi. Mwovu huja na kuyachukua yaliyopandwa katika mioyo yao.

20 Na vipi kuhusu mbegu zilizoangukia kwenye udongo wenye mawe? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho haraka na kwa furaha huyapokea. 21 Lakini hawaruhusu mafundisho kutawala maisha yao. Huyatunza kwa muda mfupi. Mara tatizo au mateso yanapokuja kwa sababu ya mafundisho waliyoyapokea, wanaacha kuyafuata.

22 Na vipi kuhusu mbegu zilizoanguka katikati ya miiba? Hizo zinafanana na watu wanaosikia mafundisho lakini huyaruhusu mahangaiko ya maisha na kutaka utajiri, hufanya mafundisho yasikue. Hivyo mafundisho hayazai mazao mazuri katika maisha yao.

23 Lakini vipi kuhusu mbegu zilizoanguka kwenye udongo wenye rutuba? Hizo ni sawa na watu wanaosikia mafundisho na kuyaelewa. Hukua na kuzaa mazao mazuri, wakati mwingine mara mia, wakati mwingine mara sitini, na wakati mwingine mara thelathini zaidi.”

Simulizi Kuhusu Ngano na Magugu

24 Kisha Yesu akatumia simulizi nyingine kuwafundisha. Yesu akasema, “Ufalme wa Mungu unafanana na mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba lake. 25 Usiku ule, kila mtu alipokuwa amelala, adui wa yule mtu akaja na kupanda magugu katikati ya ngano kisha akaondoka. 26 Baadaye, ngano ikakua na vichwa vya nafaka vikaota juu ya mimea. Kisha mtumishi akayaona magugu. 27 Watumwa wa mwenye shamba wakaja na akasema, ‘Bwana ulipanda mimea mizuri kwenye shamba lako. Magugu yametoka wapi?’

28 Yule mtu akajibu, ‘Adui alipanda magugu.’

Wale watumwa wakauliza, ‘Je, unataka twende na kung'oa magugu?’

29 Akajibu, ‘Hapana, kwa sababu mtakapokuwa mnang'oa magugu, mtaweza pia kung'oa ngano. 30 Yaacheni magugu na ngano vikue pamoja mpaka wakati wa mavuno. Wakati wa mavuno nitawaambia wafanyakazi hivi: Kwanza, yakusanyeni magugu na kuyafunga pamoja ili myachome. Kisha kusanyeni ngano na kuileta ghalani mwangu.’”

Simulizi Nyingine ya Ufalme

(Mk 4:30-34; Lk 13:18-21)

31 Kisha Yesu akawaambia watu simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na mbegu ya mharadali ambayo mtu alipanda katika shamba lake. 32 Ni mbegu ndogo sana kuliko mbegu zote. Lakini unapokua, ni kubwa kuliko mimea yote ya bustanini. Unakuwa mti mkubwa unaotosha ndege kuja na kutengeneza viota kwenye matawi yake.”

33 Kisha Yesu akawaambia simulizi nyingine: “Ufalme wa Mungu unafanana na chachu ambayo mwanamke huichanganya katika bakuli kubwa la unga ili atengeneze mkate. Chachu hufanya kinyunya chote kiumuke.”

34 Yesu alitumia simulizi akasema mambo yote haya kwa watu. Daima alitumia simulizi kuwafundisha. 35 Hii ilikuwa kuweka wazi maana halisi kama manabii walivyosema:

“Nitazungumza kwa kutumia simulizi;
    Nitayasema mambo ambayo yamekuwa siri
    tangu ulimwengu ulipoumbwa.”(W)

Yesu Afafanua Simulizi Kuhusu Magugu

36 Kisha Yesu akawaacha watu na kuingia katika nyumba. Wafuasi wake wakamwendea na akasema, “Tufafanulie maana ya simulizi kuhusu magugu ndani ya shamba.”

37 Akajibu, “Mtu aliyepanda mbegu nzuri katika shamba ni Mwana wa Adamu. 38 Shamba ni ulimwengu. Mbegu nzuri ni watoto katika ufalme wa Mungu. Magugu ni watu wa Yule Mwovu. 39 Na adui aliyepanda mbegu mbaya ni ibilisi. Mwisho wa nyakati ndiyo wakati wa mavuno. Wafanyakazi wanaokusanya ni malaika wa Mungu.

40 Magugu hung'olewa na kuchomwa motoni. Itakuwa vivyo hivyo nyakati za mwisho. 41 Mwana wa Adamu atawatuma malaika zake, nao watawatafuta watu wanaosababisha dhambi na wale wote watendao maovu. Malaika watawatoa watu hao katika ufalme wa Mungu. 42 Watawatupia katika tanuru la moto. Huko watu watakuwa wakilia na kusaga meno kwa maumivu. 43 Kisha wenye haki watang'aa kama jua. Watakuwa katika ufalme wa baba yao. Ninyi watu, mlio na masikio, sikilizeni!

Simulizi Kuhusu Hazina na Lulu

44 Ufalme wa Mungu unafanana na hazina iliyofichwa shambani. Siku moja mtu alipoiona aliificha tena; na kwa sababu alikuwa na furaha sana alikwenda kuuza kila kitu alichonacho na kulinunua shamba.

45 Pia, ufalme wa Mungu unafanana na mchuuzi anayetafuta lulu safi. 46 Siku moja alipoipata, alikwenda na akauza kila kitu alichokuwa nacho ili kuinunua.

Simulizi Kuhusu Wavu wa Kuvulia Samaki

47 Pia, ufalme wa Mungu unafanana na nyavu kubwa iliyowekwa katika ziwa. Nyavu ile ikavua aina nyingi tofauti ya samaki. 48 Ikajaa, hivyo wavuvi wakaivuta mpaka pwani. Wakakaa chini na kutoa samaki wote wazuri na kuwaweka kwenye kikapu. Kisha wakawatupa samaki wabaya. 49 Itakuwa hivyo wakati wa mwisho. Malaika watakuja na kuwatenganisha waovu na watakatifu. 50 Watawatupa waovu katika tanuru la moto. Huko watu watalia na kusaga meno yao kwa sababu ya maumivu.”

51 Kisha Yesu akawauliza wafuasi wake, “Mnaelewa mambo yote haya?”

Wakasema, “Ndiyo, tunaelewa.”

52 Kisha Yesu akawaambia wafuasi wake, “Hivyo kila mwalimu wa sheria aliyejifunza kuhusu ufalme wa Mungu ana baadhi ya vitu vizuri vya kufundisha. Ni kama mmiliki wa nyumba, aliye na vitu vipya na vya zamani nyumbani mwake. Na huvitoa nje vipya na vya zamani.”

Yesu Aenda Kwenye Mji wa Kwao

(Mk 6:1-6; Lk 4:16-30)

53 Yesu alipomaliza kufundisha kwa simulizi hizi, aliondoka pale. 54 Alikwenda katika mji wa kwao. Aliwafundisha watu katika sinagogi lao, nao walishangaa. Walisema, “Mtu huyu alipata wapi hekima na nguvu hii ya kutenda miujiza? 55 Je, yeye si mwana wa seremala tunayemfahamu? Je, jina la mamaye si Mariamu na wadogo zake ni Yakobo, Yusufu, Simoni na Yuda? 56 Na dada zake bado wanaishi hapa katika mji huu? Anawezaje kutenda mambo haya?” 57 Hivyo wakawa na mashaka kumpokea.

Lakini Yesu akawaambia, “Watu kila mahali huwaheshimu manabii, lakini katika mji wake au katika nyumba yake nabii hapati heshima yoyote.” 58 Yesu hakufanya miujiza mingi huko, kwa sababu watu hawakumwamini.

Herode Adhani Yesu ndiye Yohana Mbatizaji

(Mk 6:14-29; Lk 9:7-9)

14 Katika wakati huo, Herode, mtawala wa Galilaya, alisikia ambacho watu walikuwa wanasema kuhusu Yesu. Hivyo akawaambia watumishi wake, “Nadhani hakika mtu huyu ni Yohana Mbatizaji. Lazima amefufuka kutoka kwenye kifo, na ndiyo sababu anaweza kutenda miujiza hii.”

Kifo cha Yohana Mbatizaji

Kabla ya wakati huu, Herode alimkamata Yohana. Akamfunga kwa minyororo na kumweka gerezani. Alimkamata Yohana kwa sababu ya Herodia, mke wa Filipo, kaka yake Herode. Yohana alikuwa amemwambia, “Si sahihi kwako kumwoa Herodia.” Herode alitaka kumwua, lakini aliwaogopa watu. Waliamini kuwa Yohana alikuwa nabii.

Siku ya kuzaliwa Herode, bintiye Herodia[an] alicheza mbele yake na kundi lake. Herode alifurahishwa naye sana. Hivyo aliapa kuwa atampa kitu chochote atakachotaka. Herodia alimshawishi binti yake kitu cha kuomba. Hivyo bintiye akamwambia Herode, “Nipe hapa kichwa cha Yohana Mbatizaji kwenye sahani kubwa.”

Mfalme Herode alihuzunika sana. Lakini alikuwa ameahidi kumpa binti kitu chochote alichotaka. Na watu waliokuwa wakila pamoja na Herode walikuwa wamesikia ahadi yake. Hivyo Herode aliamuru kitu ambacho alikuwa ameomba apatiwe. 10 Akawatuma wanaume gerezani, ambako walikikata kichwa cha Yohana. 11 Na watu wakakileta kichwa cha Yohana kwenye sahani kubwa na kumpa yule msichana. Kisha yeye akakipeleka kichwa kwa mama yake, Herodia. 12 Wafuasi wa Yohana wakaja na kuuchukua mwili wa Yohana na kuuzika. Kisha wakaenda na kumwambia Yesu kilichotokea.

Yesu Awalisha Watu Zaidi ya 5,000

(Mk 6:30-44; Lk 9:10-17; Yh 6:1-14)

13 Yesu aliposikia kilichotokea kwa Yohana, aliondoka kwa kutumia mtumbwi. Alikwenda peke yake mpaka mahali ambapo hakuna aliyekuwa akiishi. Lakini watu walisikia kuwa Yesu alikuwa ameondoka. Hivyo waliondoka katika miji na kumfuata. Walikwenda mahali alikokwenda kupitia nchi kavu. 14 Yesu alipotoka katika mtumbwi, aliwaona watu wengi. Akawahurumia, na kuwaponya waliokuwa wagonjwa.

15 Baadaye mchana huo, wafuasi walimwendea Yesu na kusema, “Hakuna anayeishi katika eneo hili. Na tayari muda umepita, hivyo waage watu ili waende katika miji na kujinunulia chakula.”

16 Yesu akasema, “Watu hawahitaji kuondoka. Wapeni ninyi chakula wale.”

17 Wafuasi wakajibu, “Lakini tuna mikate mitano na samaki wawili tu.”

18 Yesu akasema, “Leteni kwangu mikate na samaki.” 19 Kisha akawaambia watu waketi chini kwenye nyasi. Akaichukua mikate mitano na samaki wawili. Akatazama mbinguni na akamshukuru Mungu kwa ajili ya chakula. Kisha akaivunja mikate katika vipande, akawapa wafuasi wake nao wakawapa watu chakula. 20 Kila mmoja alikula mpaka akashiba. Walipomaliza kula, wafuasi walijaza vikapu kumi na mbili vya vipande vilivyosalia. 21 Walikuwepo wanaume 5,000, pamoja na wanawake na watoto waliokula.

Yesu Atembea Juu ya Maji

(Mk 6:45-52; Yh 6:16-21)

22 Mara baada ya hili Yesu akawaambia wafuasi wake wapande kwenye mtumbwi. Akawaambia waende upande mwingine wa ziwa. Aliwaambia angekuja baadaye, alikaa pale ili kuwaaga watu. 23 Baada ya Yesu kuwaaga watu, alikwenda kwenye vilima peke yake kuomba. Ikawa jioni na alikuwa pale peke yake. 24 Wakati huu mtumbwi ilikuwa mbali kutoka pwani. Kwa kuwa upepo ulikuwa unavuma kinyume na mtumbwi, mtumbwi ulikuwa unapata msukosuko kwa sababu ya mawimbi.

25 Kati ya saa tisa na saa kumi na mbili asubuhi, wafuasi wa Yesu walikuwa bado ndani ya mtumbwi. Yesu akaenda kwao akitembea juu ya maji. 26 Iliwatisha walipomwona anatembea juu ya maji. Wakapiga kelele kwa woga “Ni mzuka!”

27 Lakini haraka Yesu akawaambia, “Msihofu! Ni mimi! Msiogope.”

28 Petro akasema, “Bwana, ikiwa hakika ni wewe, niambie nije kwako juu ya maji.”

29 Yesu akasema, “Njoo, Petro.”

Kisha Petro akauacha mtumbwi na kutembea juu ya maji kumwelekea Yesu. 30 Lakini Petro alipokuwa anatembea juu ya maji, aliyaona mawimbi na upepo. Aliogopa na kuanza kuzama katika maji. Akapiga kelele, “Bwana, niokoe!”

31 Haraka Yesu akamshika Petro kwa mkono wake. Akasema, “Imani yako ni ndogo. Kwa nini ulisita?”

32 Baada ya Petro na Yesu kuingia kwenye mtumbwi, upepo ukakoma. 33 Kisha wafuasi wakamwabudu Yesu na kusema, “Hakika wewe ni Mwana wa Mungu.”

Yesu Awaponya Watu Wengi Wagonjwa

(Mk 6:53-56)

34 Baada ya kuvuka ziwa, wakafika pwani katika eneo la Genesareti. 35 Baadhi ya watu pale wakamwona Yesu na wakamtambua kuwa ni nani. Hivyo wakatuma ujumbe kwa watu wengine katika eneo lote kuwa Yesu amekuja. Watu wakawaleta wagonjwa wao wote kwake. 36 Walimsihi Yesu awaruhusu waguse tu upindo wa vazi lake ili waponywe. Na wagonjwa wote waliogusa vazi lake waliponywa.

Sheria ya Mungu na Desturi za Kibinadamu

(Mk 7:1-23)

15 Kisha baadhi ya Mafarisayo na walimu wa sheria kutoka Yerusalemu walimjia Yesu na kumwuliza, “Kwa nini wafuasi wako hawatii desturi tulizorithi kutoka kwa viongozi wetu wakuu walioishi hapo zamani? Wafuasi wako hawanawi mikono kabla ya kula!”

Yesu akajibu, “Na kwa nini mnakataa kutii amri ya Mungu ili muweze kuzifuata desturi zenu? Mungu alisema, ‘Ni lazima umtii baba na mama yako.’(X) Na Mungu alisema pia kuwa, ‘Kila anayemnenea vibaya mama au baba yake lazima auawe.’(Y) Lakini mnafundisha kuwa mtu anaweza kumwambia baba au mama yake, ‘Nina kitu ninachoweza kukupa kukusaidia, Lakini sitakupa, bali nitampa Mungu.’ Mnawafundisha kutowatii baba zao. Hivyo mnafundisha kuwa si muhimu kufanya kile alichosema Mungu. Mnadhani ni muhimu kufuata mila na desturi zenu mlizonazo. Enyi wanafiki! Isaya alikuwa sahihi alipozungumza kwa niaba ya Mungu kuhusu ninyi aliposema:

‘Watu hawa wananiheshimu kwa maneno tu,
    lakini mimi si wa muhimu kwao.
Ibada zao kwangu hazina maana.
    Wanafundisha kanuni za kibinadamu tu.’”(Z)

10 Yesu akawaita watu. Akasema, “Sikieni na mwelewe nitakachosema. 11 Si chakula kinachoingia mdomoni kinachomtia mtu unajisi,[ao] bali kile kinachomtoka mdomoni mwake.”

Footnotes

  1. 1:1 Masihi Kwa maana ya kawaida, “Kristo”, tafsiri ya Kiyunani kwa neno “Masihi”. Tazama Kristo na Masihi katika Orodha ya Maneno. Pia katika mstari wa 16-17 na katika kitabu chote hiki.
  2. 1:11 baba wa Yekonia Mfalme Nebukadneza aliuangusha mji wa Yerusalemu na kuvunja hekalu mwaka 586 KK na kuwapeleka Babeli wakiwa mateka watu Mashuhuri pamoja na vyombo vya thamani vilivyokuwa hekaluni. Tazama 1 Nya 3:15-16.
  3. 1:21 Yesu Jina la Yesu maana yake “Bwana anayeokoa”.
  4. 2:23 Mnazareti Mtu anayetoka katika mji wa Nazareti. Jina hili linafanana na neno la Kiebrania linalomaanisha “tawi”. Hivyo inawezekana Mathayo anamaanisha ahadi ya “tawi” la ukoo wa Daudi. Tazama Isa 11:1. Yer 23:5; 33:15; Zek 3:8; 6:12.
  5. 3:10 mti Watu wasiomtii Mungu ni kama “miti” itakayokatwa.
  6. 3:12 Atatenganisha nafaka … makapi Inamaanisha kuwa Yesu atawatenganisha watu wema na waovu.
  7. 3:16 hua Ndege mfano wa njiwa, aendaye kwa kasi au “njiwa pori”, “tetere”.
  8. 4:3 Mjaribu Kwa maana ya kawaida, “Shetani”.
  9. 4:25 Miji Kumi Jimbo hili lilikuwa mashariki ya Ziwa la Galilaya na wakazi wake hawakuwa Wayahudi. Miji Kumi imejulikana pia kama Dekapoli.
  10. 5:3 Heri Maana yake ni baraka kuu.
  11. 5:3 maskini … wanamhitaji Mungu Kwa maana ya kawaida, “maskini wa roho”, ama wenye uhitaji wa kiroho.
  12. 5:5 watairithi nchi Wataurithi ulimwengu ujao yaani ufalme wa Mungu unaokuja.
  13. 5:6 wenye kiu na njaa ya kutenda haki Kwa maana ya kawaida, “wenye njaa na kiu ya kutenda haki zaidi ya kitu kingine chochote”.
  14. 5:8 wenye moyo safi Au wenye mawazo safi ama wenye kukusudia mema moyoni, ama wenye nia njema moyoni.
  15. 5:9 wanaotafuta amani Au “wapatanishi wa watu waliofarakana”.
  16. 5:41 maili moja Kama kilomita moja na nusu.
  17. 5:48 kamili Neno “kamilifu”, hapa lina maana “imeendelezwa kwa ukamilifu”, na inaelezea aina ya upendo ambao watoto wanaweza kujifunza kutoka kwa baba.
  18. 6:2 makusanyiko Au “masinagogi”.
  19. 6:3 asijue unachofanya Kwa maana ya kawaida, “Mkono wako wa kushoto usijue kile ambacho mkono wako wa kushoto unafanya.”
  20. 6:13 Nakala zingine za Kiyunani zimeongeza: “Kwa kuwa ufalme na nguvu na utukufu ni vyako milele na milele. Amina.”
  21. 6:19 nondo na kutu Pia katika mstari wa 20.
  22. 6:22-23 Kwa maana ya kawaida, 22 Taa ya mwili ni jicho. Hivyo, jicho lako likiwa safi, mwili wako wote utakuwa na nuru tele. 23 Lakini jicho lako likiwa na uovu, mwili wako wote utakuwa na giza. Hivyo ikiwa nuru ndani yako ni giza, giza hilo ni linatisha.
  23. 6:24 pesa Au “mamona”, neno la Kiaramu linalomaanisha “utajiri”.
  24. 7:12 torati Au “Sheria ya Musa”.
  25. 7:29 mamlaka Hakuhitaji mamlaka yoyote zaidi ya kwake. Kinyume chake waandishi daima waliwanukuu walimu wa kale wa Kiyahudi kama mamlaka ya mafundisho yao.
  26. 8:4 kuhani akakuchunguze Sheria ya Musa (torati) ilisema kuhani ni lazima aamue ikiwa mtu amepona ukoma.
  27. 8:28 Wagadarini Nakala zingine za Kiyunani zina “Wagerasi” na zingine zina “Wagergesini”.
  28. 9:17 viriba Kibuyu au chombo cha kuhifadhia divai au maji kilichotengenezwa kwa ngozi.
  29. 10:15 Sodoma na Gomora Miji ambayo Mungu aliiangamiza kwa sababu watu waliokuwa wakiishi pale walikuwa waovu sana. Tazama Mwa 19.
  30. 11:12 Herode Antipa alimkamata na kisha kumwua Yohana Mbatizaji na pia alijaribu kumzuia Yesu na wanafunzi wake kwa nguvu. Tazama Herode katika Orodha ya Maneno.
  31. 11:21 Korazini, Bethsaida Miji ya Kiyahudi iliyokuwa kando kando mwa Ziwa Galilaya ambapo Yesu alifanya miujiza mingi kudhihirisha mamlaka yake yanayotoka kwa Mungu. Pamoja na hili, watu walikataa kubadili maisha waliyoishi yasiyokuwa na Mungu.
  32. 11:21 Tiro na Sidoni Miji iliyojaa ibada ya sanamu ambayo ilijulikana sana kwa uovu uliokuwemo humo.
  33. 11:23 Sodoma Mji ambao Mungu aliuangamiza, pamoja na Jiji la Gomora, kwa sababu watu walioishi walikuwa waovu sana. Tazama Mwa 19.
  34. 11:25 kama watoto wadogo Maana wale ambao hawajaenda shule bado.
  35. 11:29 nira yangu Nira iliwekwa shingoni mwa mnyama anayefanya kazi ili kuvuta mzigo. Ilikuwa pia ni alama ya Kiyahudi kwa sheria. Tazama Mdo 15:10; Gal 5:1. Ilikuwa pia alama ya kutawaliwa na taifa katili la kigeni, kama vile Ufalme wa Rumi.
  36. 12:24 Shetani Jina la Mwovu lenye maana “Adui”. Kwa maana ya kawaida, “Beelzebuli” kwa Kiyunani (mwovu). Pia katika mstari wa 27.
  37. 12:26 ikiwa Shetani … mashetani Kwa maana ya kawaida, “ikiwa Shetani atamfukuza Shetani.”
  38. 12:39 Yona Au “Nabii Yona”, nabii katika Agano la Kale. Baada ya kukaa katika tumbo la samaki mkubwa kwa siku tatu alitoka akiwa mzima, kisha akaenda kwenye mji uliojaa uovu wa Ninawi kuwaonya watu huko kama alivyotumwa na Mungu. Kwa njia hiyo hiyo, Yesu angetoka kaburini siku ya tatu, ishara ya kuthibitisha ukweli wa ujumbe wake kutoka kwa Mungu.
  39. 12:42 Malkia wa Kusini Au “Malkia wa Sheba.” Alisafiri kama maili 1,000 (kilomita 1,600) ili kujifunza hekima ya Mungu kutoka kwa Sulemani. Tazama 1 Fal 10:1-13.
  40. 14:6 Herodia Josephus, Mwana historia wa Kiyahudi anamwita binti huyu Salome.
  41. 15:11 unajisi Yaani, “kichafu” au “kisicho safi”, maana yake kisichokubaliwa na Mungu. Pia katika mstari wa 18,20.