Add parallel Print Page Options

Yesu Awalisha Watu Zaidi ya 4,000

(Mt 15:32-39)

Wakati mwingine katika siku zile kundi kubwa la watu lilikusanyika na halikuwa na chakula. Yesu akawaita wanafunzi wake na kuwaambia, “Nawahurumia watu hawa, kwa sababu hata sasa wamekuwa nami kwa siku tatu, na hawana kitu cha kula.”

Nikiwaacha waende majumbani mwao wakiwa na njaa, wataanguka njiani; na baadhi yao wametoka mbali.

Wanafunzi wake wakamjibu, “Wapi mtu yeyote atapata chakula cha kutosha mahali hapa jangwani cha kuwalisha watu hawa?”

Yesu akawauliza, “Mnayo mikate mingapi?” Wakajibu, “Saba.”

Kisha Yesu akaliagiza kundi la watu kuketi chini ardhini Akachukua mikate ile saba, akashukuru, akaimega na kuwapa wanafunzi wake waigawe. Nao wakaigawa kwenye kundi. Kulikuwapo pia samaki wadogo wachache. Yesu akawabariki wale samaki na kuwaambia waigawe nayo pia.

Watu walikula na kushiba. Wakakusanya vikapu saba vilivyojaa mabaki. Ilikuwa kama watu 4,000. Kisha Yesu akawaacha waende.

Read full chapter