Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria walimwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee wetu, na badala yake wa nakula kwa mikono najisi?”

Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa: ‘Watu hawa wanani heshimu kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.” Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu!

Read full chapter