23 Maovu haya yote hutoka ndani ya mtu, na ndio yanayomfanya mchafu.”

Yesu Amponya Binti Ya Mama Mtaifa

24 Ndipo Yesu akaondoka hapo akaenda sehemu za Tiro. Akaingia nyumba moja, ambapo hakupenda mtu afahamu yupo. Lakini hakuweza kujificha. 25 Mama mmoja ambaye binti yake mdogo ali kuwa na pepo mchafu aliposikia habari za Yesu, alikuja mara moja akajiangusha miguuni pake. 26 Huyo mama hakuwa Myahudi, alikuwa Mgiriki aliyezaliwa Siria-Foinike. Akamsihi Yesu amtoe binti yake huyo pepo mchafu.

27 Yesu akamwambia, “Tuwaache watoto wale washibe kwanza, kwa maana si halali kuchukua chakula cha watoto na kuwatupia mbwa.”

28 Yule mama akajibu, “Ni kweli Bwana, lakini hata mbwa walio chini ya meza hula makombo ya watoto.” 29 Yesu akamjibu, “Kwa sababu ya jibu lako, unaweza kwenda nyumbani. Yule pepo ameshamtoka binti yako.”

30 Akaenda nyumbani akamkuta binti yake amelala kitandani, na pepo amemtoka.

Read full chapter