Mafundisho Ya Kale

Mafarisayo na baadhi ya walimu wa sheria waliokuwa wametoka Yerusalemu walikusanyika mbele ya Yesu. Wakawaona baadhi ya wanafunzi wake wakila chakula bila kunawa kama ilivyotakiwa na sheria ya dini ya Wayahudi. Wayahudi, na hasa Mafarisayo, hawali chakula pasipo kunawa kwa kufuata mila za wazee wao. Na kwa sheria wanapotoka sokoni hawawezi kula pasipo kunawa. Pia kuna desturi nyingine nyingi wanazofuata kama vile jinsi ya kuosha vikombe, vyungu, na vyombo vya shaba.

Kwa hiyo wale Mafarisayo na walimu wa sheria walimwuliza Yesu, “Mbona wanafunzi wako hawafuati desturi za wazee wetu, na badala yake wa nakula kwa mikono najisi?”

Yesu akawajibu, “Nabii Isaya alisema ukweli alipotabiri juu yenu, ninyi wanafiki, kama ilivyoandikwa: ‘Watu hawa wanani heshimu kwa midomo yao, lakini mioyoni mwao wako mbali nami. Kuniabudu kwao ni bure. Wanafundisha watu amri zao badala ya sheria yangu.’ Ninyi mmeziacha amri za Mungu na kushikilia desturi za watu.” Akawaambia, “Mnaepuka kwa ujanja amri za Mungu ili mpate kutimiza desturi zenu! 10 Kwa mfano, Musa alisema, ‘Waheshimu baba yako na mama yako’ na ‘Ye yote amtuka naye baba au mama auawe.’ 11 Lakini ninyi mnasema mtu akimwambia baba yake au mama yake kuwa, “Msaada ambao ningekupa ni Kor bani,” yaani umetengwa kama sadaka kwa Mungu, 12 basi hawaji biki tena kumsaidia baba yake au mama yake. 13 Kwa njia hiyo mnadhalilisha neno la Mungu kwa taratibu zenu mlizojiwekea. Na mnafanya mambo mengi ya jinsi hii.”

Read full chapter